Tatizo la kula/kutafuna kucha

Tatizo la kula/kutafuna kucha

Duh! Nitajaribu kufanya hivyo akija likizo, akirudi kutoka shule ndio utazionea hadi huruma, kucha mbaya
Jaribu kufanya hilo, lakini naye ajiandae maana wengine anaweza kuwa anatafuna big g na kucha ipo mdomoni.
 
Kuna Rafiki yangu Huyo yeye huwa anazinyofoa kope kwenye macho,
Yaani mpaka sasa hana hata kope moja,
yani anasema ikiota japo moja yeye huisi inamuwasha na kuamua kuinyofoa, Kipindi cha vumbi huwa anapata tabu sana machoni,
Alafu hata kucha pia anatafuna tena saana,
Sijui amemkosea nini Mungu cuz weakness zote anazo,
kuna kipindi tulikuwa tunamcheka akiwa anyofoa kope na akapunguza kiasi flani kwa kuona aibu, ila kwenye kucha ndo huna cha kumwambia,
 
Binti yangu alikuwa na kuchagua nzuri sana, zimeharibika sababu ya kuziuma, nilishaongea hadi nimechoka. Je akifanikiwa kuacha kuzing'ata zitarudi kuwa nzuri?
ram cha muhimu sana kwasasa ni kujitahidi aache hiyo tabia, kucha ni kitu kinachoota kwahiyo with time zitaota tena Usiwe na shaka
 
  • Thanks
Reactions: ram
Yaani mimi nimeona huu uzi nimefurahi sana,nakula kucha mpaka najisikia vibaya mimi mwenyewe!Kwetu tumezaliwa watatu na wote tunakula kucha ile mbaya na nakumbuka pia kumwona baba yangu akila kucha sasa huwa na waza tuliiga au tuliridhi kutoka kwake.Kuna saa huwa ni tamu mpaka nakimbia kukaa mahali peke yangu mtu asinione halafu nakula kwa raha zangu na enjoy sana.Nikiwa mja mzito nakula mpaka natoka damu.Jamani hii kitu nikiweza kuacha nitafurahi sana yaani mpaka kucha zimepinda na kuwa nyeusi.Mume wangu amepambana na mimi mpaka amesanyoosha mikono.Mshana jr asante sana kwa hili somo nitaanza sasa kuacha na nitawapa mrejesho kabla na baada!
Pole Sana hili ni tatizo la kizalia kama ilivyo pumu nk...uwe unazipaka vitu vyenye harufu usiyopenda kabisa kuisikia baadae mdomo/meno yata adopt na kuacha kabisa..
 
Du! I see kuna rafiki yangu anatafuna kucha hadi namuonea huruma. Hata yeye anasema huwa hakumbuki chochote wakati anapozitafuna na ameishajizuia kuacha hiyo tabia bila mafanikio. Afanyeje?
Kuna mahali nimemjibu UPOPO hebu pita hapo
 
Duh mimi ni mhanga mkubwa sana wa kula kucha hata za miguuni nakula
 
Mshana jr, vipi unatoa tiba mkuu, kuna dogo langu yani huwa nampiga mingumi ila hasikii, huyu ni mgonjwa type gani chronic ama?[/QUOTE pole mpeleke kwa wanasaikolojia au mpeleke kwa chris mauki atamsaidia kuondokana na tatizo hilo
 
Toka darasa la kwanza nang'ata kucha huwa najitahidi kuacha ila nashindwa
 
Mchumba wangu hili ni tatizo kubwa linamsumbua...ila yeye haoni.. anatafuna kucha sana za mikono. na hana msongo wala wasiwasi wowote..ni miaka tokea mdogo.. na ananyonya nyonya saa kidogo kikubwa cha mkono wa kulia hadi kimekonda kabisaa..
 
Uchunguzi umebaini ulaji kucha/unyonyaji vidole una faida kwa watoto "Ripoti mpya inasema watoto wanaonyonya vidole au kung'ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani" BBC. Kwa lugha nyingine sio rahisi wala kucha kupata allergies na hili linathibitika wengi ninaowajua wa namna hii huwa hawaumwi umwi na kila kitu wao wanakula tu

Unyonyaji kidole unafaida kwa watoto- Utafiti - BBC Swahili
 
Hicho ni kizalia
 
Hizi tafiti nyingine za wazungu hizi kuna wakati huwa nadhani wanafanya makusudi kutuongopea ama la watakuwa wanaumwa ugonjwa wa akili
....! Nilikumbuka ule utafiti wa maziwa ya mende ni dawa....! Nathibitisha bila shaka kuwa kuna tatizo kubwa mahali
 
Hicho ni kizalia

Dawa yake ni nn..? Sbb ananikera sana..makucha yameharibika.. na hadi sasa hv namfundisha kunyonya koni aache kunyonya kidole chake kikubwa.. nambana sana aache lakini wapi.. sasa nimeamua nimwekee kucha za bandia for a while labda ataacha.. of which kucha za bandia sizipendi.. sbb she is soooo cuteeee... whiteee... bootyfull.. but i hv no any other choice..
 
mimi nimeathirika kweli kweli,mpaka leo,zikikuwa tu,uwa sina mpango wa kutafuta kiwembe,mwendo wa meno tu,kuna wakati nilikuwa nakula kucha,zikiwa fupi,nakula na ile ngozi ya ncha za kucha,kazi ilikuwa kwenye kula ugali wa moto,nilikuwa NAKOMA
Du pole sana mkuu.
 
Kwenye hili la kucha nakubaliana nao kabisa. Nawajua watu kadhaa wa karibu walaji kucha waliobobea kitu kimoja kuhusu hawa jamaa huwa hawaumwi na kila kitu wao wanakula tu. Kama umesoma article inasema ulaji kucha kwa watoto ina maana watakula na uchafu na hatimaye mwili wao kujenga immunity ili kupambana na magojwa hivyo immunity zao kuwa strong zaidi. Nadhani ni very reasonable
 
Dawa yake ni nn..? Sbb ananikera sana..makucha yameharibika.. na hadi sasa hv namfundisha kunyonya koni aache kunyonya kidole chake kikubwa.. nambana sana aache lakini wapi.. sasa nimeamua nimwekee kucha za bandia for a while labda ataacha.. of which kucha za bandia sizipendi.. sbb she is soooo cuteeee... whiteee... bootyfull.. but i hv no any other choice..
Kwanza ni lazima akubali kubadilika ili muweze kushirikiana kutatua tatizo. ..awe anapaka/au unampaka vidoleni/kuchani vitu vyenye harufu asiyopenda
Pili epuka kucha za bandia madhara yake ni makubwa zaidi kwakuwa zinazuia juhudi za ujuaji wa kucha ambazo tayari ziko mahututi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom