Unaweza ukaacha kutafuna kucha "kama utataka". Hakuna aliezaliwa akitafuna kucha isipokuwa hayo ni matokeo ya kimazingira.
Tatizo la kutafuna kucha tena "mpaka kuitwa tatizo" si kidogo. Kwa wenzetu wanasaikolojia wanaliita "tatizo la kitabia" na kwa watafunaji wengi, huwa kuna mazingira linatokea; mfn. Unapokuwa na stress, huna kazi ya kufanya, una matatizo ya ulaji n.k.
Katika umri mkubwa hali hii huwa ni mbaya sana kwa muathirika kwani unakuta mtu hawezi kupitisha dk 5 bila kuweka kidole aama vidole mdomoni na kuanza kung'ata kucha hata kaama ni fupi mno.
Ni kweli hali hii huleta fedhesha kwa mtafunaji hasa pale anapokuwa mbele za watu wa kuheshimika ama anapofanya presentation ya kitu fulani.
UNAWEZAJE KUACHA.
Kuacha si rahisi kama "hutatia nia ya kufanya hivyo". Utafunaji wa kucha ni tabia na mtu hujifunza tabia fulani na huamua kuiacha pia (a behavior can be learnt or unlearnt).
Kama alivyosema msemaji mmoja hapo juu njia moja wapo ni KUPAKA VITU VICHUNGU KWENYE KUCHA ZAKO ambavyo vitakufanya ushinde kuzitafuna kucha zako
Pili, kuviwekea "nail clip" vidole vyako.
Kuweka kitu kwenye meno ya upande wa juu mbele ambavyo vitasaidia kuzuia ukataji wa kucha.
Tatu, kujitahidi kujiepusha na vitu vinavyoweza pelekea kutafuna kucha (najua utakuwa unajua ni mazingira gani huwa unatafuna kucha zako)
Kutafuta kitu mbadala ambacho kitakufanya uwe bize nacho (kama gums) hivyo kutojishughulisha na kucha zako, ingawa nazo si nzuri.
Jitahidi kujizuia hata kwa kuvifunika vidole vyako kwa vitambaa ama gause kwani ukiweze kufanya moja ya mambo hayo kwa muda wa miezi miwili ama zaidi, hakika utaondokana na tatizo la kutaka kutafuna kucha'zo.
Dawa ya kuondoa tatizo linalokusumbua kwanza ni kama ulivyofanya "kuliona tatizo na kulikubali" na pili "kuchukua hatua" kwa kudhamiria kufaaanya hivyo.
All the best dear!