Tatizo la kuku kugombania mayai

Newword

JF-Expert Member
Dec 2, 2019
326
299
Wadau.

Samahani nina kuku wangu wameanza kutaga kwa mpigo sasa wanatabia ya kugombania mayai wakati wa kutaga.

Naomba mnisaidie njia ya kutatua tatizo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app

------------------------------------
Baadhi ya Michango

sehemu za kutagia zipo za kutosha? Maana mimi kuku wangu karibu 6 walikuwa wanataga sehemu moja nikatafuta tu madishi 4 nikatengeneza vitu vizuri mbona tatizo kiliisha mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Mkuu ngoja nijaribu njia hiyo.Hafu kwa vifaranga wa wiki 2 naweza wapa chanjo gani muhimu????

Sent using Jamii Forums mobile app
CHANJO ZA KUKU - RATIBA MAALUM
1. SIKU 1.
Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins na OTC plus
Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe
2. SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baa
da ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa vitamini
3. SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu kama hapo pichani
4. Siku ya 21 (wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri)
5. SIKU 28 (Mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
6. SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.
7. WIKI 8 - 10
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8. WIKI YA 12
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna huu ugonjwa wa kusinzia vifaranga na kutetemeka vina week 2 niwape dawa gani??

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole mkuu ila licha ya hizo dalili 2 fatilia kama kuku wako wanadalili za kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia,kuharisha
Kama ndiyo basi kuku watakuwa na dalili za Gumboro......

Tumia dawa inaitwa oxytetracycline sikumbuki bei yake lakin haizidi elfu 7 mkuu....kuku wangu wakianza kuwa na dalili kama zako ila dawa ilisaidia sana na ingawa wanasema Gumboro haina tiba ila kwangu alikufa mmoja tu wengine wakapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom