Tatizo la marefa wa Tanzania linatokana na mafunzo duni au vyuo

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
5,885
13,263
Hivi kuna refa wa Tanzania ameenda kusomea urefa nje kweli au kupata mafunzo nje ya Tanzania?

Ukiangalia karibia wote ni sawa hamna mwenye uafadhali, mwingine unakuta mchezo mzima anaharibu,mwingine atachezesha vizuri lakini kuna sehemu anakuja kuchemka.

Labda hawana elimu tunalaumu kupewa bahasha na upenzi wa hizi timu kubwa.

Naomba kufahamu ni vyuo gani au taasisi gani inatoa marefa wajinga hivi hapa Tanzania? Mfano hai ni Kayoko unaweza ukadhani ni refa makini na serious lakini umakini wake ni kukodoa macho tu lakini haoni.

Wizara iwapeleke nje hata watu 20 hivi wakasomee kozi fupi nje halafu warudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiria baada ya ccm kujiingiza kwenye mpira wa Simba na yanga marefa wameziba macho ili kuwafurahisha!!!! Athari zake umeziona IVORY COST hakuna refa wenu
 
Tatizo la marefa wa Tz ni mashabiki. Timu zao zinaponufaika na makosa ya refa wanachekelea na kukaa kimya. Timu zao zikiminywa ndo unawasikia wanabweka. Ila siku mashabiki wote wakiungana na kuukataa huu upuuzi wa marefa watabadilika tu. Pigeni kelele hata pale timu yako inapobebwa na makosa ya mwamuzi
 
Tangu msimu wa ligi ya NBC uanze , Simba Ndio timu iliyofaidika na makosa ya uamuzi kuliko timu yoyote apa Nchini.

Walibeba Ngao kwa hisani ya tatu Malogo, walifaidika kwa kupata point wasizo stahili kwa makosa ya kibinadamu dhidi ya Prison, Singida, KMC n.k Leo nao wanalalamikia refa, ni unafiq wa kiwango Cha juu.
Wakumbuke karma itawatafuna tu.
 
Hivi kuna refa wa Tanzania ameenda kusomea urefa nje kweli au kupata mafunzo nje ya Tanzania?

Ukiangalia karibia wote ni sawa hamna mwenye uafadhali, mwingine unakuta mchezo mzima anaharibu,mwingine atachezesha vizuri lakini kuna sehemu anakuja kuchemka.

Labda hawana elimu tunalaumu kupewa bahasha na upenzi wa hizi timu kubwa.

Naomba kufahamu ni vyuo gani au taasisi gani inatoa marefa wajinga hivi hapa Tanzania? Mfano hai ni Kayoko unaweza ukadhani ni refa makini na serious lakini umakini wake ni kukodoa macho tu lakini haoni.

Wizara iwapeleke nje hata watu 20 hivi wakasomee kozi fupi nje halafu warudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mara ya Kwanza Leo nimekusikia unaongea ambacho wenzio tunasema mara Kwa mara
Ulichosema ni sahihi . Kasoro yenu wengi mnalaumu marefa timu mnazoshabikia zinapoonewa. Chukua Mechi mbili za mwisho za NBC PL. Anza na Mechi ya Yanga vs Mashujaa. Refa wa hii Mechi alistahili kuchezesha UMISETA na siyo PL. Alikuwa na makosa mengi ambayo yamezibwa na ushindi wa Yanga, lakini wangedroo kelele zingekuwa nyingi sana kutokana na makosa ya dhahiri aliyoonyesha.
Njoo Sasa mechi ya Simba vs Azam, Kwa ukubwa na ubora anaopewa Rama sidhani kama ni sahihi kwake Mechi ya Simba na Azam kuonekana kubwa kwake. Ni dhahiri alikuwa na makosa na mengi aliyaona na kuamua tofauti lakini kiujumla alikuwa na madhaifu kwenye;
Angle of view.
Proximity
Proper decision.
 
Urefa wa bongo ukishafuzu tu COPA test...ukawa unakimbia kwa muda uliowekwa na kuweza kupuliza filimbi tayari ushafuzu na unatafutiwa beji ya FIFA au CAF inakuwa imeisha hiyo
 
Tangu msimu wa ligi ya NBC uanze , Simba Ndio timu iliyofaidika na makosa ya uamuzi kuliko timu yoyote apa Nchini.

Walibeba Ngao kwa hisani ya tatu Malogo, walifaidika kwa kupata point wasizo stahili kwa makosa ya kibinadamu dhidi ya Prison, Singida, KMC n.k Leo nao wanalalamikia refa, ni unafiq wa kiwango Cha juu.
Wakumbuke karma itawatafuna tu.
Ngao hajachezesha Tatu ni Jonesia
 
Kwa mara ya Kwanza Leo nimekusikia unaongea ambacho wenzio tunasema mara Kwa mara
Ulichosema ni sahihi . Kasoro yenu wengi mnalaumu marefa timu mnazoshabikia zinapoonewa. Chukua Mechi mbili za mwisho za NBC PL. Anza na Mechi ya Yanga vs Mashujaa. Refa wa hii Mechi alistahili kuchezesha UMISETA na siyo PL. Alikuwa na makosa mengi ambayo yamezibwa na ushindi wa Yanga, lakini wangedroo kelele zingekuwa nyingi sana kutokana na makosa ya dhahiri aliyoonyesha.
Njoo Sasa mechi ya Simba vs Azam, Kwa ukubwa na ubora anaopewa Rama sidhani kama ni sahihi kwake Mechi ya Simba na Azam kuonekana kubwa kwake. Ni dhahiri alikuwa na makosa na mengi aliyaona na kuamua tofauti lakini kiujumla alikuwa na madhaifu kwenye;
Angle of view.
Proximity
Proper decision.
Mkuu kote uongee kiswahili hapo mwisho ndio uweke angle proximity na hiko kingine anaetaka kuelewa kuhusu udhaifu wa kayoko inakuwa Bure endapo hajui Kingereza
 
Hatujawah kuwa serious kwenye mambo ya msingi... Kibaya zaid Adharani tunapondana sirini tunasifiana. Hao marefa ni kielelezo tuu cha jamii tuliyonayo
 
Kwa mara ya Kwanza Leo nimekusikia unaongea ambacho wenzio tunasema mara Kwa mara
Ulichosema ni sahihi . Kasoro yenu wengi mnalaumu marefa timu mnazoshabikia zinapoonewa. Chukua Mechi mbili za mwisho za NBC PL. Anza na Mechi ya Yanga vs Mashujaa. Refa wa hii Mechi alistahili kuchezesha UMISETA na siyo PL. Alikuwa na makosa mengi ambayo yamezibwa na ushindi wa Yanga, lakini wangedroo kelele zingekuwa nyingi sana kutokana na makosa ya dhahiri aliyoonyesha.
Njoo Sasa mechi ya Simba vs Azam, Kwa ukubwa na ubora anaopewa Rama sidhani kama ni sahihi kwake Mechi ya Simba na Azam kuonekana kubwa kwake. Ni dhahiri alikuwa na makosa na mengi aliyaona na kuamua tofauti lakini kiujumla alikuwa na madhaifu kwenye;
Angle of view.
Proximity
Proper decision.
Kwani kosa la refa jana ni lipi hadi mpigizane kelele hivi?
FB_IMG_1707543855443.jpg
 
Back
Top Bottom