Tatizo la kuchukia watu bila sababu

Haiwezekani Kumchukia Mtu bila sababu......................Jitafakari vizuri utajua kwa nini Unachukia....................!!!! Kuna mwenzio alisema hivyo hivyo, alipobanwa zaidi akafunguka ya kuwa anamchukia kwa vile ile Midomo yake eti imebinuka kwa hiyo anahisi kama vile ANAJIDAI................ndiyo maana yeye anamchukia.....................!!!
Hahahahahahaha
kusema kweli mm sioni sababu
 
Inaweza kuwa ni wivu, kama amekuzidi ama kawa na kitu fulani bora zaidi yako.
Kingine pengine inaweza kuwa ni kawa na tabia huipendi ama hakuwa nayo awali.
et eeh
maana nna rafiki yangu Wa Tangu
primary...
tukaja tukafaulu wote secondary moja tukasoma
tumekua kama ndugu sasa
hajanikosea chochote Tuko zaidi ya miaka 15 lakini jamani saivi najikuta simpendi mpaka najishangaa yani sababu hakuna
 
Ni ngumu sana kumchukia mtu bila ya sababu, lazima huenda kuna sababu ambayo inakuwa ngumu kuitambua.

Labda sura yake au sauti yake au muonekano wake au uvaaji wake unakukumbusha kitu kibaya hapo nyuma.

Mfano, kuna mtu alikufanyia ukatili hapo nyuma kisha baadae unakutana na mtu mwingine tofauti kabisa, lakini kuongea kwake au muonekano kunafania na yule aliyekufanyia kitu kibaya hapo nyuma. Hivyo inakukumbusha juu yake na hivyo unaanza kumchukia bila sababu.

Au kuna wengine wale wenye nguvu za ziada, kwa kumtazama mtu tu, anatambua kuwa huyu mtu ni mbaya hata kama hajawahi kumtenda au hata kuzungumza naye. Hivyo anajikuta anamchukia tu bila sababu za Msingi.

Jichunguze vema, lazima kuna sababu inayokufanyia umchukie.
mimi hii kitu nnakuaga nayo sana.
kuna shangazi yangu tuliishi nae sana hapa kwetu..
nikawa namchukia jamani,hata akinisemesha natamani kumtafuna
sikuwa na sababu yoyote, akaja kuondoka akakaa kwake kama miezi mi2 akaua watt wake wawili kwa sumu....

mwezi wa6 nimeenda kumuona jela musoma mjini, unajua moyo wangu umesuuzika mpaka najishangaa nmemuona tu nmelia...

kuna mwingine alikuaga wifi yangu best nikaja nikamchukia sana,gafla hakukaa sana miezi mi2 akaiba mil7 ya kazini kwao akatokomea...
 
Inaitwa INFERIORITY COMPLEXION. Una shida ya kupenda kujilinganisha na watu unaokutana nao kwa uzuri, mali na hata social acceptance. Unafanya haya bila kujijua na pale unapoona mtu huyo amekuzidi kwenye hilo unalojilinganisha naye na hakuna unaloweza kufanya, unamjengea chuki.

Believe me, huwachukii bila sababu.
Jibu pekee nililoliona

Salute to you
 
maranyingi huwa kunakitu kinafanya umchukie mfano, yawezekana kuvaa kwake, au life style yake, au kunakitu ulisikia au kuona kwake ambacho kikaingia ndani ya kichwa chako then unakuta we hupendi kitu ka hicho so huwa kunavitu vidogo vidogo ambavyo hutokea sema huvigundui kisa hujaamua kufuatilia kwa kina tatizo ni nini
Najitahidi kutafuta sababu....
siioni, ila nitajitahidi zaidi
 
Ipo namna flani kiimani,unahitajika kufanyiwa maombi,yawezekana una majinubi,au una roho ya chuki ambayo umerithi kutoka kwenye ukoo wenu,jaribu pia kufuatilia ndani ya ukoo wenu kama kuna mtu mwenye tabia kama hizo,ila kwa yote hayo kwa Yesu hayana nafasi..
Sinaga chuki
imenitokea kwa mtu huyu
 
Inaitwa INFERIORITY COMPLEXION. Una shida ya kupenda kujilinganisha na watu unaokutana nao kwa uzuri, mali na hata social acceptance. Unafanya haya bila kujijua na pale unapoona mtu huyo amekuzidi kwenye hilo unalojilinganisha naye na hakuna unaloweza kufanya, unamjengea chuki.

Believe me, huwachukii bila sababu.
kusema kweli
sijilinganishagi
halafu nawakubali sana wanawake wenzangu kiasi hata akipendeza namwambia wewe mzuri,umependeza nk

mpaka nmelileta hapa means linanisumbua
labda nijitahidi kuchimba ukweli
 
Hii pia huwa inasababishwa na mambo ya kiroho, unapaswa luwa MTU wa MAOMBI na kusali ukikemea hiyo hali na itaisha hats Mimi nilikuwa hvyo
Afadhali atleast umenisaidia wengine hawanielewi
 
Iyo roho mbaya inakusumbua ,,na unapoelekea utakua mchawi ,,kwa sababu hasira inatokana na ibiriss ,(sheitwani) ,mbaya
 
Back
Top Bottom