Tatizo la Foleni Dar es Salaam LAISHA

Tatizo la Foleni Dar es Salaam LAISHA

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
409
Reaction score
31
Wakuu,

Foleni Dar es Salaam ilikuwa inasababishwa na askari wa Usalama Barabarani. Toka juzi tarehe 14/05/2013, natumaini wengi mtakuwa mmeona mabadiliko makubwa kuhusu uwepo wa askari wa usalama barabarani katika njia tofauti hapa jijini Dar es Salaam. Natumaini mkakati huu utaendelea kutumika na kuheshimiwa na TAA ZA BARABARANI KUWACHWA ZIFANYE KAZI YAKE.
 
Unajua wewe ni JF member toka 2006, yaani ni mzoefu wa Jukwaa sasa unapopost huna buni kuonyesha uzoefu kidoggo ulionao; wengine hatuko dar lakini tuna interest zetu dar hivyo lazima tufuatilie kila tukio. Ni nini kimetokea, ni mabadiliko makubwa ya namna gani yaliyotokea? kama ni mkakati kwa nini usiuelezee mkakati wenyewe tukaujua kama una nia ya ku-share ulichonacho
 
sio kweli,
askari wana msaada sana tena sana.

Kama unakumbuka miaka ya nyuma sikukumbuki lini kakini nadhani ni mid-2000s watu walilalamika hivi hivi, kwamba foleni inasababishwa na askari barabarani, then kwa kuitikia mwito huu askari waliondolewa barabrano na kuachia taa ziongoze mgari. Kilichotokea ni chaos na disaster, watu wenyewe waliomba askari warudi especially during peak hours.

Sasa hii ya kwako leo napingana nayo coz majuzi, jana na leo kwa nia ninayopitaga kuna skrai full karibu katika kila junction na kwenye taa.

Kwa hiyo nadhani huu wako ni uzushi otherwise show the source au authenticity ya taarifa yako hii
 
Hahahahahaha!
Foleni Dar iishe?thubutu yako!
Ukitoka huku kwetu Ukonga saa12 asbh unafika k,koo saa1.30-2.00 asbh.
Na kwa jinsi walivyofunga mitaa ya barabarani kuanzia njia panda segerea,airport,jet,vingunguti,tazara,chang'ombe basi tabu tupu.
 
hatukatai kuwa polisi wanasaidia kuondoa msongamano wa magari lakini in most case wao huwa wanasababisha msongamano wa magari especially unafika mataa unashinda hapo lisaa limoja bado hamruhusiwi na magari yanavutwa upande aliopokea rushwa yeye tu. hivi waliogundua yale mataa ya kuongozea magari ni wajinga? polisi wawepo mataa kusimamia tu kuwa magari yanavuka ipasavyo co yeye kujichukulia majukumu ya taa. hebu ona kinachiendelea jijini sa hivi polisi barabarani kibao hiyo foleni sasa duu.
 
Kesho mtawaita tena bongo bwana!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Unajua wewe ni JF member toka 2006, yaani ni mzoefu wa Jukwaa sasa unapopost huna buni kuonyesha uzoefu kidoggo ulionao; wengine hatuko dar lakini tuna interest zetu dar hivyo lazima tufuatilie kila tukio. Ni nini kimetokea, ni mabadiliko makubwa ya namna gani yaliyotokea? kama ni mkakati kwa nini usiuelezee mkakati wenyewe tukaujua kama una nia ya ku-share ulichonacho

Welcome jijini Dar es salaam
Jiji la umbea bugha na miangaiko ya kila aina
Dar es salaama ghalama ukindishwa kuishi ama
 
Hahahahahaha!
Foleni Dar iishe?thubutu yako!
Ukitoka huku kwetu Ukonga saa12 asbh unafika k,koo saa1.30-2.00 asbh.
Na kwa jinsi walivyofunga mitaa ya barabarani kuanzia njia panda segerea,airport,jet,vingunguti,tazara,chang'ombe basi tabu tupu.

labda huyu bwana anaishi magomeni, lakini sisi tunaokaa njia hii...
 
Subiri Msafara wa Pinda kutoka Airport akitokea Dodoma , ndiyo utafahamu hakuna foleni au la !
 
hatukatai kuwa polisi wanasaidia kuondoa msongamano wa magari lakini in most case wao huwa wanasababisha msongamano wa magari especially unafika mataa unashinda hapo lisaa limoja bado hamruhusiwi na magari yanavutwa upande aliopokea rushwa yeye tu. hivi waliogundua yale mataa ya kuongozea magari ni wajinga? polisi wawepo mataa kusimamia tu kuwa magari yanavuka ipasavyo co yeye kujichukulia majukumu ya taa. hebu ona kinachiendelea jijini sa hivi polisi barabarani kibao hiyo foleni sasa duu.
Sidhani kama wanapokea rushwa.Tatizo ni misafara isiyopungua ya wenye nchi, vigogo na vibosile
 
Mhh foleni gani zilizopungua? Au mwenzetu umehama Dar? Na pia trafic kuwepo wanapunguza sana tatizo la foleni. Nakushauri kajipangu na uje na data za kutushawishi!
 
Watu wengine bana angalia mida ya post...saa saba....
 
Nawashukuruni wote kwa michango yenu.

Kwa wale wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi naamini watakubaliana nami kuwa foleni imepungua sana katika barabara hiyo toka tarehe 14/05/2013.

Mkakati wenyewe unahitaji mambo makubwa mawili

1. Askari wa barabarani hawatakiwi kuwepo barabarani na kuingilia mfumo wa magari na taa za barabarani.

2. Taa za barabarani ziachwe zifanye kazi yake. Askari wetu wa barabarani wasaidie tu katika makutano ya barabara ambapo taa hazifanyi kazi.

Hili linatakiwa lifanyike katika barabara zote. Kwa barabara ambazo bado ziko kwenye matengenezo, hali ya foleni inaeleweka.
 
sio kweli,
askari wana msaada sana tena sana.

Kama unakumbuka miaka ya nyuma sikukumbuki lini kakini nadhani ni mid-2000s watu walilalamika hivi hivi, kwamba foleni inasababishwa na askari barabarani, then kwa kuitikia mwito huu askari waliondolewa barabrano na kuachia taa ziongoze mgari. Kilichotokea ni chaos na disaster, watu wenyewe waliomba askari warudi especially during peak hours.

Sasa hii ya kwako leo napingana nayo coz majuzi, jana na leo kwa nia ninayopitaga kuna skrai full karibu katika kila junction na kwenye taa.

Kwa hiyo nadhani huu wako ni uzushi otherwise show the source au authenticity ya taarifa yako hii

Asante kwa post yako. Kutokana na madereva wengi kuwategemea askari wa barabarani kuwaongoza kwenye taa, wengi hujisahau na kutofuata mfumo wa taa. Naomba muelewe kuwa uwepo wa askari wa barabarani kila baada ya mita chache ni tatizo na ndiyo chanzo kikuu cha foleni hapa Dar ukiondoa barabara ambazo bado zina matengenezo makubwa.
 
leo watu wameenda temeke kuangalia mpira wa yanga.
 
Back
Top Bottom