Tathmini ya kisayansi juu ya matokeo ya uchaguzi mkuu Novemba 2020

Mm ni mwanaccm asili ila kwa uchambuzi wako juu Lusu tumeshafeli kwani kumbuka tumeshajisahau kunadi sera zetu na kuanza kucopy za upinzani issue ya Bima na m engine. Inainyesha hatukujiandaa au hatukujua kama upepo ungetuvumia vibaya kiasi cha kubaki kumjibu Lisu. Huku kazi ya Katibu Mku na Mwenezi hazijulikani. Kwa mfano Polepole amesahau kazi yake na kuamua Mc
 
Sayansi na Teknolojia vikitumika vizuri vina uwezo wa kutoa majibu ya wakati ujao,uliopo na uliopita kwa uhakika wa asilimia 99.9%.

Katika andiko langu hili nitatumia taarifa za kisayansi zilizopo kuweza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 2020.

Tathmini hii isitumike kuwabwetesha wale ambao tathmini itawaonesha wanaweza kushinda ila iwe chachu ya kuwafanya wafanye vizuri zaidi.

Pia kwa wale ambao itaonesha watashindwa nao iwe chachu kwao kujiandaa na kujitahidi kushinda katika maeneo ambayo wananguvu ya kushinda na endapo itatokea kushindwa, kushindwa huko kuwe kwa kiwango cha kawaida.

Lengo kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi kupitia mfumo ambao sote tumeuridhia wa demokrasia ya vyama vingi.

Mazingira ya tathmini hii, yamezingatia kuwa vyama vya upinzani vitaungana vyote nchini na kumsimamisha mgombea mmoja chini ya mwamvuli wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Tanzania (MVUTA) dhidi ya chama tawala CCM.

Tukumbuke kuwa uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 ulihusisha baadhi ya vyama vya upinzani (UKAWA).Pili tume ya uchaguzi ifanye kazi zake kwa uadilifu na umahiri mkubwa kuhakikisha uchaguzi ni wa amani,huru na wa haki.

Tathmini yangu ina anza na idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni hamsini na nne nukta mbili (54.2 milioni).

Idadi hii ina asilimia 50% (27.1 milioni) ya watoto ambao ni chini ya umri wa miaka 18,na watu wazima wanaoruhusiwa kupiga kura asilimia 50% (27.1 milioni) ambao kati yao asilimia 70% (18.97 milioni) wanaoishi vijijini na wanajishughukisha na kilimo na ufugaji pamoja na uchuuzi.

Asilimia 30% ambao (8.13 milioni ) wanaishi mijini ambao wengi wanajishughulisha na kazi mbalimbali.

Kwa mantiki hii ni wazi kuwa chama ili kiweze kupata ushindi mkubwa kinatakiwa kijiimarishe zaidi vijijini ambapo kuna idadi kubwa ya watu ukilinganisha na maeneo ya mijini ambapo kuna idadi ndogo ya watu.

Kwa taarifa na takwimu zilizopo CCM imejiimarisha zaidi vijijini ukilinganisha na muunganiko wa vyama vyote vya upinzani.

Hii inatokana na mambo mengi,moja uwepo wa wajumbe wa nyumba kumikumi,uwepo wa ofisi za chama katika maeno ya vijijini, uwepo wa viongozi wa chama na wale wa serikali wanaojishughulisha na kazi za chama, uwepo wa sherehe mbalimbali kama mwenge, uchumi wa chama na kadhalika.

Katika maeneo ya mijini kwa mijibu wa takwimu na hali ya kisiasa kwa kipindi cha nyuma, wimbi kubwa la vijana hasa wachuuzi (kwa jina maarufu la wamachinga) walivutiwa na sera za upinzani.

Huku idadi kubwa ya kinamama na wazee ikiwa na msimamo wao na imani yao kwa CCM. Kwa baadhi ya vijana sera hizi ziliwavutia kutokana na kukithiri mambo mbalimbali ya kifisadi, kunyimwa fursa za kujipatia kipato kwa kuondolewa sehemu za mijini na kutowajibika kwa serikali kwa wananchi, mgawanyiko ndani ya CCM na kuhama kwa Mh. Edward Lowasa kutoka CCM kwenda UKAWA.

Kundi hili la vijana baada ya kuonekana ni tishio kwa CCM limekumbatiwa na linaweza kuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020.

Tangia siku ya kwanza ya Raisi Magufuli kuingia madarakani, makundi tofauti ya wanachi kuanzia wachuuzi, wafanyakazi, wakulima, vijana na kina mama wamepewa fursa na uhuru mkubwa wa kufanya kazi halali zinazowaingizia kipato.

Hivyo basi kurejesha imani yao kwa chama kupita uaminifu aliofanya Raisi wa kutekeleza ilani ya chama sawasawa.

Vile vile ili kuweza kupata idadi ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 turejee takwimu za uchaguzi mkuu uliopita wa Octoba 2015 kama ifuatavyo.

Jumla ya idadi ya Wapiga kura nchi nzima walikua ni 23.3 milioni,kati ya hao asilimia 53% walikua wanawake na 47% ni wanaume.

Idadi kubwa ya wanawake nchini walimuunga mkono Raisi Magufuli ukilinganisha na ile ya wanaume.

Katika historia ya vyama vingi nchini Tanzania, ni uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 pekee uliokuwa na hamasa kubwa kutoka kwa vijana wanaoishi mijini juu ya mabadiliko ya uongozi kutoka chama tawala CCM kwenda muungano wa vyama vya upinzani kwa jina la UKAWA.

Uchaguzi huu ulitoa matokeo ambayo kwa tahmini ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini ni ushindi mkubwa kwa upinzani ambao hautaweza kujirudia.

Figure 1. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015

Viashiria vya kushindwa kwa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 2020 vinaonekana katika nyanja zifuatazo:-

1. Muundo wa serikali na mabadiliko katika utendaji wa watumishi wa umma.

Serikali ya awamu ya tano imeundwa na aina tatu za viongozi,ambazo ni viongozi vijana, viongozi wataalamu na wachapa kazi,viongozi waadilifu na wachamungu.

Tabia hizi za viongozi wa serikali zimesaidia kuleta matumaini makubwa kwa wananchi na kurejesha imani yao kwa serikali chini ya chama tawala.

Mh Rais amekuwa akisafisha mara kwa mara serikali yake bila kumuonea haya mtu yeyote kwa maslahi ya taifa. Utoaji wa huduma kwa wanachi umekuwa wa haraka na unaofuta maadili ya utumishi wa umma.

2. Maendeleo yanayoonekana katika awamu ya tano, kauli zilizokuwa zimezoeleka za serikali ipo katika mchakato zimeondoka na kauli zakiutekelezaji zimetawala.

Jambo ambalo limekua na matokeo mazuri katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile miundombinu, upatikanaji wa pembejeo, maji, uimarishaji wahuduma za afya na elimu, kukamilisha miradi ya kimkakati katika kuinua uchumi, kuanzisha viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania.

3. Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Kubweteka na kupelekea kushindwa kukidhi masharti kwa wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani na baadhi kutoka chama tawala kulipelekea wagombea wengi kuenguliwa katika nafasi za kugombea Uenyekiti wa serikali za mitaa.

Maandalizi makubwa yaliyofanywa na chama tawala yalipelekea kuwepo kwa idadi ndogo ya wagombea walio enguliwa katika mchakato hivyo kuipa ushindi mkubwa katika uchaguzi huo.

Viongozi wa serikali za mitaa wanomchango mkubwa katika kuipa ushindi CCM kwa kutoa matokeo mazuri katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

4. Upinzani kupoteza mwelekeo

Vyama vya upinzani vimepoteza mwelekeo na kutokua na sera mbadala za kimaendelo zitakazowavutia watanzania.

Viongozi wake wamekua wakipinga mema ambayo serikali inafanya kwa wananchi pamoja na kusukumwa na matukio.

Matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo inakadiriwa kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura yamekua njia rasmi kwa wapinzani kuwafikia wananchi huku CCM ikijiimarisha miji na vijijini kupitia vikao na mikutano na wanchi kusikiliza na kutatua changamoto zao.

Idadi ya watumiaji wa Intenet inakadiriwa kufikia milioni 10 kati ya watumiaji hao ni watanzania milioni 6 tu wanafuatilia masuala ya siasa katika mitandao ya kijamii.

Hivyo basi kama mgawanyo wa watu utafuata upenzi wa vyama ni wazi katika watu milioni 6 ni watu milioni moja wanapinga juhudi za serikali katika kuletea wananchi maendeleo.

5. Ushahidi katika tafiti zingine

Tafiti zilizowahi kufanyika nchini na nje ya nchi zinaotoa majibu yafuatayo katika chaguzi mbalimbali:-

No Jina la Mtafiti na Eneo la Utafiti Jina la Utafiti Matokeo ya Utafiti

1 Twaweza 2014 Kuelekea Uchaguzi Mkuu Jumla ya Watanzaia 51% wataichagua CCM, 24% Chadema, 25 % hawajui.

2 Twaweza 2017 Sauti ya Wananchi Asilimia 84% ya wananchi wamesema watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 67% ambao walijitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2015

Ushindi kwa CCM ni 63% hadema ni 17%

Hitimisho:
Uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 utaipa ushindi CCM kwa asilimia zaidi ya 87% huku muungano wa vyama vya upinzani ukiwa na asilimia 13%.

View attachment 1316179
Mleta mada achaujinga nakukariri unawatukana wanavijiji bilahata hatawewe kujuwa andikolako linaonesha vijijini hawajitambui siokweli kabisa marakadhaa wabunge wengi kwakiasi chao waupinzani hutokea kwenye wilaya ambazo zipopamoja navijiji kwasasa watu wavijijini wanaufahamu sawa nawamjini tu mfano kampeni zilizoanza lisu amepita maeneo yamorogoro kwenye vijiji watu walikuwa namori kubwa sana kumshabikia tuache uongo nasayansi zakishamba watu wanajuwa hakizao uelewe
 
Mleta mada achaujinga nakukariri unawatukana wanavijiji bilahata hatawewe kujuwa andikolako linaonesha vijijini hawajitambui siokweli kabisa marakadhaa wabunge wengi kwakiasi chao waupinzani hutokea kwenye wilaya ambazo zipopamoja navijiji kwasasa watu wavijijini wanaufahamu sawa nawamjini tu mfano kampeni zilizoanza lisu amepita maeneo yamorogoro kwenye vijiji watu walikuwa namori kubwa sana kumshabikia tuache uongo nasayansi zakishamba watu wanajuwa hakizao uelewe
Usitukemee,
Andiko halijaongea watu wa vijijini hawajielewi usilete propaganda za Chadema hapa,lete hoja.
 
Usitukemee,
Andiko halijaongea watu wa vijijini hawajielewi usilete propaganda za Chadema hapa,lete hoja.
Umesema kura zaccm zipo vijijini ndiomimi nikajibu sikweli waliopo vijijini ambalo upinzani haupo kama andikolilivyo sema siokweli uelewa kwasasa v na m nisawasawa hatawabunge wengi waupinzani hutokea kwemajimbo yawilayani siomikoani nahapa ukibisha madayako ondoa itakuwa imekwama
 
Back
Top Bottom