TARURA waingia mkataba na wakandarasi kuanza ujenzi

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
Kazi imeiva katika mkoa wa DSM baada ya TARURA kuingia mkataba na wakandarasi wazawa kujenga barabara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa DSM. Billioni 14 tayari zimemwagwa.

Sasa tunataka kazi zionekane, wakandarasi wazawa pigeni kazi muache visingizio, kazi mmepewa hela mmepewa sasa ole wenu mule hela za walipa kodi halafu kazi zisikamilike.

Pongezi kwa Rais Samia kwa kudhamiria, naamini maeneo ya pembezoni yamepewa kipau mbele zaidi kwa mfano maeneo ya Kiluvya gogoni. n.k
 
Kazi imeiva ktk mkoa wa DSM baada ya TATURA kuingia mkataba na wakandarasi wazawa kujenga barabara ktk maeneo mbalimbali ya Mkoa wa DSM.
Billioni 14 tayari zimemwagwa.
sasa tunataka kazi zionekane, wakandarasi wazawa pigeni kazi muache visingizio, kazi mmepewa hela mmepewa sasa ole wenu mule hela za walipa kodi halafu kazi zisikamilike.
Pongezi kwa Rais Samia kwa kudhamiria.
Bilioni 14 ni kujenga Barabara zipi na ziko wapi dar ? Je ni kilometers ngapi? Vinginevyo fedha hizo ni za kununua magari ya starehe. Nani anakagua miradi ya Tarura?
 
Bilioni 14 ni kujenga Barabara zipi na ziko wapi dar ? Je ni kilometers ngapi? Vinginevyo fedha hizo ni za kununua magari ya starehe. Nani anakagua miradi ya Tarura?
kila halmashauri itakuwa imeaanisha barabara zake zitakazo jengwa.
bilashaka wabunge na madiwani wa maeneo husika wameshirikishwa kikamilifu.
 
sasa ni mwendo wa lami mitaani.

Jiji la DSM litang'aaa sana.

Pongezi za dhati kwa Rais wetu kipenzi Samia kwa kuamua kutekeleza, haya ndio maendeleo tunayo yataka.
 
Sijajua ni kiwango kipi cha lami!! Ila bilioni 14 kwa barabara ya kiwango cha lami ni ndogo sana japo itapunguza kero kiasi kikubwa!

Kwani zile pesa za tozo za miamala bado hazijatosha tu! Ziko wapi zimefika kiasi gani na mpaka zifike ngapi ndo zianze kutumika!! Mbona hatupeani taarifa wakati ni jasho letu?
 
Bilioni 14 kwa lami sahihi ni inatosha kilometa 14 tu sasa jiji zima la dar kivipi?
Nadhani sehemu kubwa itakuwa kuzijenga kwa vumbi,hizo fedha ni chache Sana hususani Dar.

Ila kwa mujibu wa Tarura hiyo ni awamu ya kwanza kutakuwa na awamu 3 na awamu zijazo ndio hasa pesa ya tozo.

Nchi nzima Tarura wanatangaza Kazi zingine mwezi huu wa 8 kwa pesa za mafuta .
 
Bilioni 14 Kujenga Barabara za vumbi " mvua zikinyesha utaambia wapiga kura Barabara ziliekekea wapi" anyway miradi haikaguliwi
 
Bilioni 14 Kujenga Barabara za vumbi " mvua zikinyesha utaambia wapiga kura Barabara ziliekekea wapi" anyway miradi haikaguliwi
Uwaambie kwani hizo mvua zinakuwa zilinyesha chumbn hazikuonekana au? Bil.14 ni km 15 tuu za lami sasa kila mkoa una utaratibu wao wa vipaombele walivyokubaliana na madiwani wewe kama shida yako ni kukagua kakague
 
Kwa mfano sisi sehemu tuliko mahitaji na barabara za kuunganisha mtaa na mtaa zipitike na kuwe na madaraja lami sio kipaombele japo huwa wanajenga km 1 kila mwaka .Hii ni kulingana na bajeti finyu iliyopo .

Halmashauri zingine hata mita 500 ya lami hazijengw maana sio muhimu.Cha muhimu ni madaraja na kufanya barabara zipitike tuu
 
Back
Top Bottom