Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,514
- 19,266
Arsene Wenger ameanza taratibu za kununua baadhi ya wachezaji ili kuziba pengo lililiachwa na Mathieu Flamini na uwezekano wa kuondoka kwa Alex Hleb kwenda Inter Milan.
Ifuatayo ni orodha ya majina na wachezaji wanaozungumzwa pale Emitares.
Ivan Gennaro Gatusso.
Mshindi wa kombe la Dunia na timu ya Italia na mchezaji wa AC-Milan pia ya Italia.
Gattuso amewahi kucheza Uingereza katika ligi ya Scotland akiwa na timu ya Rangers. Ni mchezaji wa kiungo na kununuliwa kwa kijana mdogo Flamini kunaashiria kufunguliwa milango kwa Gattuso kutafuta timu maana atakuwa ansugua benchi. tatizo ni umri ambao ni mkubwa kidogo wa miaka 31 na Wenger hilo linamzuia.
Jean II Makoun
Huyu ni kutoka Cameroon. Arsenal wanafuatilia mwenendo mzima wa kijana huyu na iwapo Alex Hleb ataondoka basi huyu ndio ataziba pengo. Moja ya matazamio ya Jean ni kuingia Uingereza baada ya mkataba wake kwisha pale Lille Ufaransa.
Obafemi (Oba) Martins
Oba ana kasi, nguvu na ni mwepesi.
Pia Wenger ana uwezo wa kulipa mpaka paundi 15milioni kwa mshambiliaji huyu matata. Pamoja na kwamba tayari pana washambiliaji kama Emmanuel Adebayor, Robin Van Persie, Eduardo and Nicklas Bendtner, tatizo la majeruhi ndilo limewadhuru Arsenal msimu huu. Newcastle wana matatizo ya fwedha na kocha wao Kevin Keegan amekiri kwamba itabidi auze baadhi ya wachezaji ili kupata fwedha kidogo za kuijenga upya timu hiyo ambayo msimu huu haijaweza kuwa hata katika kumi bora.
Niko Cranjcar
Kranjcar, alijitengenezea jina na timu ya Dinamo Zagreb na Hajduk Split kabla ya kujiunga kwa paundi £3.5m na timu ya Portsmouth miezi 20 iliopita, amecheza vizuri katika ligi kuu msimu huu na pia ameisaidia sana Croasia kuitoa Uingereza katika mechi ya kutafuta timu za kucheza fainali za mataifa ya Ulaya miezi michache ijayo mwaka huu.
Wenger anaweza kuweka mezani paundi milioni 10 kwa kijana huyu mwenye umri wa miaka 23.
Ni hayo tu wapenzi wenzangu wa Arsenal ingawa pia kuna majina mengine ambayo yanazungumzwa kama Charles N'zobia wa Newcastle anaegharimu paundi 10 milioni na Ben Arfa wa Lyon ya Ufaransa ambae atagharimu paundi 12milioni.