Arsene Wenger kuja kuwatizama SIMBA kwa Mkapa

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ni moja ya wageni watakaokuja Tanzania katika ufunguzi wa Mashindano ya African Football League Oktoba 20.

Wenger ambaye ni moja ya watu wa ufundi wa FIFA atakuwa sehemu ya watu watakaolitazama pambano la mechi ya Simba SC na Al Ahly ya Misri katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mmoja ya waratibu wa mchezo huo wa ufunguzi (jina limefichwa) alithibitisha ujio wa kocha huyo raia wa Ufaransa.
 
Dah! Kama ana akili bora tu asije.

Maana hataamini kama kuna timu mpaka kwenye karne hii ya 21 bado zinacheza mpira wa kubutua butua tu uwanjani (yaani mpira wa papatu papatu), badala ya ule mpira uliozoeleka wa kwenye kitabu.
 
Kwa kusikia kua kuna watu mashuhuri wanakuja watajifanya wanacheza mpira wa kutandaza.
Hapo Ahly ndipo watakapojipatia maokoto.
Bora wacheze tu papatu papatu lao waitunzie heshima nchi yetu.
Kweri ya lawama kuliko fedheha.
 
Back
Top Bottom