Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 1,729
- 3,368
Kuna video inamuonesha mwandishi wa habari akihaha kumkimbilia Kocha wa zamani wa Arsenal ya Jijini London, Mzee Arsene Wenger kwa ajili ya kupata mahojiano mara baada ya nguli huyo kutua Airport ya JK Nyerere kwa ajili ya michezo ya African football league (afL).
Kichekesho ni pale Mzee Wenger amekaa anamsikiliza ndugu Mwandishi. Yule mwandishi ameishia kujikanyagakanyaga mwenyewe na kuchekacheka huku akimwamkia Wenger kwa lugha ya Kifaransa cha kuchapia! Sasa nikajiuliza kulikuwa na ulazima gani wa yule mwandishi kutumia kifaransa wakati hata yeye mwenyewe hakijui swsw zaidi ya salamu. Au sijui alifikiri Wenger hajui kiingereza? Mzee wa watu akaona isiwe taabu akafunga mlango wa gari na kujiondokea!
Hivi hizi aibu za waandishi kwenye mahojiano zitaisha lini jamani? wanatutia aibu hawa watu.