Taratibu za kupima kiwanja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taratibu za kupima kiwanja

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by amkawewe, Aug 20, 2012.

 1. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wakuu wa JF,

  Msaada wenu unahitajika:
  1. Naomba kujua taratibu za kupima kiwanja dar es salaam ikoje? Process inakuwaje na cost?
  2. Kupata leseni ya makazi process yake ikoje?

  Asanteni
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Tutasaidiwa wengi, tafadhali
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Ungeweka udaku hapa au habari zinazohusu kufunguana zipu, weeee, ungeona thread inajaa by the second.

  Mie nilichoka nilipoambiwa bei ya kupimiwa chapchap (rushwa) ni 2.5 million.

  Otherwise kuna kama miezi sita ya kusubiri kikao cha madiwani na ujinga mwingine kama huo ambao hata sikuwa na moyo wa kuusikiliza vizuri samahani.Nikakataa kutoa rushwa. Nikaelewa matatizo ya serious investors.

  Kama kabwela mie naombwa (more like napewa "bei" ya rushwa inayotakiwa) 2.5 milioni, investor anayetaka kuanzisha a genuine multi million dollar business?

  I suspect walikuwa wananitisha tu kutaka kunitoa hela, wakanikuta mtu mwenyewe sina shida hivyo sikufuatilia sana, to the chagrin of input seekers on this thread.

  I am watching this space. I am also wondering if the NHC apartments are worth it, especially considering the commutes.
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Ungeweka udaku hapa au habari zinazohusu kufunguana zipu, weeee, ungeona thread inajaa by the second.

  JF ndivyo walivyo, angalia thread za ngono, zitachangiwa mpaka.........pages 40 and above. Weka thread ya sheria, afya, lo watu wawili/watatu, kama hii hakuna mtu. MMU utachoka utitili wa michango! The oldest trade made by human being was related to sex! ANYWAY KUPANGA NI KUCHAGUA
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,033
  Likes Received: 23,967
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona unatoka nje ya mada? Toa darasa bana acha longolongo mingi kama Pinda.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  na anayejua gharama za mkoa wa pwani atutajie jamani, za huku kisarawe
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Like father like son, na wewe umetoka nje ya mada. Ungeacha comment yako ukachangia mada.
   
 8. by default

  by default JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi kuna heneo lipo heka mbili nilimchukua jamaa mpimaji kwenda kucheck tu kwa madarubini na kuweka pin kupata ukubwa wa eneo,ili akanitafutie kwenye raman ya mipango miji alikula 350000,kwenye ramani ya jiji limeonekana sasa ni mchakato wa kuweka mawe nataka anitolee viwanja vinne ktk heka mbili kwa iyo shuguli anaitaji 2.5 baada ya hapo ndio kupata title sijajua itagharimu sh ngapi.kuhusu utaratibu wa serakal ya kijij inatakiwa uende na hati ya mauziano kama ni kurith uwe na barua ya kikao cha wanafamilia kukubal wew ndo mrith wa eneo mwenykt wa kijij atapga sahii,kama umenunu kwenye mktaba kuna garama ya manunuz serikal ya kijij watataka uwalipe 10% ya ile pesa bila kupunguza sh1 na ukumbuke kuna gharama ya ofce muhuri kama sh 20elf au 30.kwa mtendaj wa kata utalipa elf10.ths thng zinaboa sana rushwa nje nje japo sijatoa hadi sasa na bdo cjapata hadi nataka nikipata hati niuze 30m kwa kiwanja vipo madale
   
 9. by default

  by default JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kumbuka raman ya mipand mij muhm sana unaweza kuta eneo ni open spabe,religi0‹2n,health centre,marketn nk so nimuhm kujua eneo lako kama ni maalm kwa makaz ili usijijenga kweny eneo la shule au vingnevyo utakuja juta.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  ushuari wangu bei sijui ila nenda wizarani pale ongea na mshkaji unayemfahamu kwani process inaweza kukugharimu ama isikugharimu lkn taratibu za awali ni hizi hapa

  nenda serikali ya mtaa wakuandikie kitu inaitwa muhutasari wa kuomba kupimiwa eneo. hii huwaga wana chaji 10%ya bei ulonunulia eneo na wanakupa risiti but kwa uzoef wangu naona hata vitabu vyenyewe vya risiti havikaguliwi so ni kama za kwao tu. ukiongea nao vzr wanaweza kupunguza bei.

  baada ya hapo kagua eneo lako kama kuna jirani ambaye amepima eneo lake so ana beacon kama yupo soma namba za jiwe zinaandikwaga juu kabisa mf ZN 49 etc.

  kama hakuna basi hapo tafuta mtu wa jikon kabisa kule ardhi mweleze nia yako achukue GPS aje apime coordinates kwenye engo zote za eneo wao watakwenda kuingiza kwenye master pln waone kama lina mchoro kama halina jua unatakiwa kugharamia mchoro ila kama upo basi kazi kwako ni rahisi sana.

  wakishajua kama halijapimwa ndipo watakapo kuambia nini cha kufanya so b4 kwenda savei kwanza eneo lako ama kuna beakon ili ujue itakugharim nini hasa.

  usitishwe na bei bana kila ktiu kinazungumzka ila usiende ka hawa private consultants watakulima miele kibao nenda huko front usogope. pia kama eneo haliihitaj ramani basi muda ni mchache sana unakuwa umepata hati na mawe. manake watakupa ofa kisha ndipo kama baada ya miez 2 unapata title deed. ni vitu ambavyo vinafanyika bana ila wanaotaka kupitia kwa hawa wa private wanapigwa na unakuta hata baada ya miaka 2 bado title deed hajapata.
   
 11. p

  puto Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  1 KITENGO CHA MIPANGO MIJI AFISA MIPANGO MIJI(TOWN PLANNER) • Kuandaa michoro ya ubunifu ya mipango miji ya maeneo ambayo itaratibu uendelezaji wa mji husika.(inaitwa town planning drawings inshort TP) • Kubadilisha matumizi ya ardhi ya viwanja ambavyo vimeshapewa hati • Kutoa vibali vya ujenzi wa majengo • Kutoa vibali vya upimaji wa ardhi • Kufanya marekebisho ya michoro ya mipango miji Mchoro wa mipango miji ambao unaonyesha matumizi mbali mbali ya eneo husika e.g shule, open spaces etc ukishatayarishwa na manispaa ni lazima upelekwe wizarani kwa mkurugenzi wa mipango miji wa wizara ya ardhi ili audhinishe. 2 KITENGO CHA UPIMAJI AFISA UPIMAJI (LAND SURVEYOY) Kazi kubwa ya mpimaji ni kupima eneo ambalo tayari lina mchoro wa mipango miji na anatakiwa kupima kulingana na mchoro wa mipango miji kama unavyo eleza. Upimaji uatendana na mambo yafuatayo • Atapanda mawe(beacons) • Atakupa kiwanja namba(plot number) • Ataonyesha ukubwa wa eneo plot area) • Ataonyesha na mipaka ya kiwanja(plot boundaries) Ramani ya upimaji inayo onyesha mawe ya kiwanja, kiwanja namba, ukubwa wa kiwanja na mipaka ya kiwanja ambayo lazima iwe imesajiliwa na kuidhinishwna mkurugenzi wa upimaji na ramani wa wizara ya ardhi 3 KITENGO CHA ARDHI AFISA ARDHI(LAND OFFICER) Majukumu ya huyu bwana ni • Kuandaa hati miliki ya viwanja ambavyo vimeshapimwa na ili aanze kukuandalia hati utatakiwa umpelekee mchoro wa mipango miji unaonyesha kiwanja chako ili ajue matumizi yake, ramani ya upimaji ya kiwanja chako ili ajue anaanda hati ya kiwanja gani, kipo wapi na kina ukubwa gani coz wanapokadiria kodi ya kiwanja lazima wajue ukubwa wa kiwanja. • Kazi nyingine ya afisa ardhi ni kuhuisha miliki yani kuongeza mda wa umilikiwa ardhi mana kuna hati za miaka 33, 66 na 99. • Kazi nyingine ni kuhamisha miliki kutoka kwa mmiliki mmoja na kwenda kwa mwingine inaitwa transfer. Hati nayo ikisha kamilika kuandaliwa na manispaa ni lazima ikahakikiwe na kamishna wa ardhi wa wizara na hatimaye msajili wa hati naye ataisajili. NB: mara nyingi gharama za kupima kiwanja kimoja ni kati ya laki 800000 hadi 1000000/- lakini bei huwa inapungua mkiwa zaidi ya mtu mmoja mana mtakuwa mnashare gharama. Kwenye suala la upimaji wa viwanja hakunaga vikao vya mipango miji ila kazi zote za mipango miji ni lazima ziinishwe na kamati ya mipango miji ya manispaa kabla ya kuwasilishwa wizarani. Kwa mawasiliano zaidi na uelewtuwasiliane through 0779000250. Nawasilisha
   
 12. M

  MANAKE MKARI Senior Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu mchango wako ni mzuri sana ila nina swali ambalo litanufaisha na wengine. Hizo gharama ulizoonyesha ni gharama zote hadi kupata hati?Kwa maneno mengine nikikupa hiyo hela unaniletea hati baada ya kufanya ninayotakiwa kama kwenye serikali ya mtaa, etc
  ?
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  Kama ni shamba la ekari 40 gharama pia huwa ni hizo? Kati ya laki 8 hadi 1m? Au itaongezeka?


   
 14. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante wadau kwa michango yenu naendelea kukusanya, ili nijue hatua na kuchukua kupimiwa eneo langu.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swali lako ni taratibu za kupima kiwanja. Mimi naomba nikujibu kwa upana zaidi. Kuna kupima kiwanja na kurasimisha umiliki wa kiwanja. Kupima kiwanja ni simple sana na haicost zaidi ya sh. laki mbili. Kama kiwanja kiko mjini ni kazi isiyozidi saa moja, kwa sababu anachofanya surveyor ni kutafuta jiwe la kiwanja kilichopimwa then anacorrigate na kiwanja chako, then anachukua city master plan na kuonyesha kiwanja chako kilipo. Hapo kazi ya kupima imeisha.

  Ugumu ni kwenye process ya kurasimisha umiliki. Kuna aina mbili ya kurasimisha zote zinatambulika 1. Kupitia serikali za mitaa 2. kupitia serikali kuu.
  From 1. Unahitaji kuwa na karatasi ya manunuzi ya kiwanja au makubaliano yaliyokuwezesha kumili kiwanja kama uristhi etc. Hii unaenda nayo ofisi ya seriali ya mtaa. Hawa watataka asilimia 10 ya mauzo ya kiwanja na uthibitisho wa mjumbe wa shina kuwa kiwanja hicho anakijua na anakutambua, watahitaji pia majina ya majirani wa kiwanja hicho kwa pande zote. Ukitimiza haya watakutengenezea barua ya utambulisho na hati ya serikali ya mtaa. barua ya utambulisho utakayopewa unaenda nayo ofisi ya halmashauri ya wilaza kitengo cha kodi ya ardhi na majengo. Pale watakupa namba ya kiwanja chako na kukadiria kodi. makadirio ya kodi unayachukua na kwenda kulipa kodi TRA. From that momen wewe ni mmiliki halali wa eneo husika unayetambulika kisheria.

  From 2. baada au kabla ya kupimiwa kiwanja na cadastro surveyor unaandika barua kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kupiti ofisi ya serikali ya kata na ofisi ya serikali ya mtaa ya kuomba kupimiwa kiwanja chako. Barua hiyo unaiambatanisha na barua ya utambulisho toka kwa mjumbe wa shina na nyaraka zinayoonyesha jinsi ulivyomiliki eneo. Again ofisi ya serikali ya mtaa iwapo eneo hilo hujalipata kwa kurithi watataka asilimia 10 ya bei. kama ni eneo la kurithi watataka nyaraka za mahakama yiliyokumilikisha. Barua hiyo ikishapitishwa ngazi ya mtaa na kata, unaipeleka kwa mkurugenzi. Hapa kuna options mbili, unaweza kumtumia surveyor wako au ukaomba surveyor wa serikali. Kuharakisha ni vizuri kutumia wako. Halmashauri watasubiri baraza la madiwani likae na liwe na muda wa kuijadili hoja ya eneo hilo kupimwa. madiwani wakikubali basi mchoro ulioletwa na surveyor unaingizwa kwenye ramani ya mji. Ukishaingizwa kwenye ramani, file linatkiwa lipelekwe wizara ya ardhi kwa ajili ya kuingizwa kwenye kumbukumbu za kitaifa na kutengeneza hati.
   
 16. p

  puto Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  hyo laki nane hadi milion moja ni gharama ya kupima kiwanja kimoja but vikiwa vingi hata cost yake inapungua, kwa mfano vikiwa kumi unaeza ukapimiwa kwa laki1 kwa kila kiwanja coz cost za labour, transport na machines zinakuwa ni zile zile tu. naomba kurudia tena kwemye kupima viwanja hakuna haja ya vikao vya madiwani. vikao vya madiwani huwa vianafanyika kama mtu anahitaji kubadili matumizi ya kiwanja chake labda kutoka makazi kwenda shule n.k, kugawanya kiwanja na vibali vya ujenzi.
   
 17. p

  puto Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  gharama ya kuandaa hati kwa malipo halali ya serikali haiwezi kuzidi laki 300000/= kwasababu utahitajika kulipia fomu ya kuomba kumilikishwa ardhi kutoka ofisi ya ardhi ya wilaya au manispaa ambayo ni elfu 5000/=, utahitaji kulipia kodi ya ardhi(land rent) kwa mwaka ambayo itategemea thamani ya ardhi ya eneo husika na ukubwa wa kiwanja ambayo mara nyingi haizidi laki mbili na mwisho gharama ya kuandaliwa deed plan(raman ya hati) ambayo nayo haizidi elfu50.
   
 18. NDAMANDOO

  NDAMANDOO JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Tunashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri ngoja nijipange ili niwaone hao TP.
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,506
  Likes Received: 5,622
  Trophy Points: 280
  Hii thread kwanini sio sticky?????????????????????
   
 20. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Dah,
  Very productive.
  Sasa kama master plan inasema ni Barabara, nawe ushanunua, kuna uwezekano mipango miji wakapindisha au ku-ammend??
  Manake master plan wanazifungia watu wa Ardhi, huku mitaani watu wanathibitishiwa Na serikali ya kijiji ambao hawajui chochote!!
   
Loading...