Tanzia: Zakaria Ndemfoo wa Machame Kisiki

R.I P nguli wa salama enzi hizo akiwa sambamba na Jofrey Njeleka wa mkwajuni Chunya Mbeya(sasa Songwe). Bila kujisahau mimi mwenyewe nikirindima kutuma salamu Idhaa ya kiswahili ya Channel Afrika miaka ya 80's 90's. Wakati huo watangazaji ,,,William Njelanje, Kaleja kaunda wakifanya vyema kabisa as radio presenters kwa habari na vipindi vya salaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah..! Mbuyu wa salam umeanguka. Lala kwa amani mzee wetu. Mwenye picha yake tafadhali.
DSC01245.JPG
DSC01245.JPG
 
Me nlipewa tu story na mwenyeji wangu nlikuwa hata simjui Ila miaka imeenda mnoo maana mwenyeji wangu hata kabla hajahamia hapo kwake huyo chesco alishakufa.
Miaka zaidi ya 8 imepita.
Si alikuwa dereva??
Siyo kwamba alikuwa ana kibanda cha kuuza matunda pale Sinza Afrika Sana?
 
Mimi namjua Zakaria Ndemfoo wa Lake Babati club enzi hizo.
ZAKARIA NDEMFOO wa MACHAME KISIKI haya majina mawili likiwa la mtuma salami maarufu duniani kupitia idhaa za kiswahili za Marekani, Uingereza, Afrika Kusini, India, Sauti ya Ujerumani, Radio China na Sauti ya Injili (Ethiopia) na redio za Afrika Mashariki miaka ya sitini na kuendelea alifariki tarehe 17 / 01 / 2020. Mzee Zakaria ndiye mtanzania pekee aliyekuwa maarufu masikioni mwa watu duniani, enzi hizo Zakaria Ndemfoo na Machame Kisiki vilizagaa kwenye anga duniani na lugha ya kiswahili japo wengi hawakujua alikieneza kiswahili kwa njia ya salamu kupitia redio.
PUMZIKA PEMA MZEE ZAKARIA NDEMFOO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifo cha Zakaria Ndemfoo ni ujumbe kwa wale wanaodhani kiswahili kilikuwa hakitangazwi nchi za nje na wao ndiyo wanaanza kukitangaza wajue sivyo. Kiswahili kilianzia pwani ya Afrika Mashariki toka Lamu nchini Kenya, Kilwa, Unguja na Msumbiji pia nchini Kongo ya DR. Kenya na Kongo ndiyo waliokitangaza sana kiswahili kupitia wanamuziki wao ambao walikuwa maarufu sana kabla ya miaka ya sitini, na Kenya ndiyo walikuwa watunzi wakubwa wa vitabu vya kiswahili kuliko sisi.
 
ZAKARIA NDEMFOO wa MACHAME KISIKI haya majina mawili likiwa la mtuma salami maarufu duniani kupitia idhaa za kiswahili za Marekani, Uingereza, Afrika Kusini, India, Sauti ya Ujerumani, Radio China na Sauti ya Injili (Ethiopia) na redio za Afrika Mashariki miaka ya sitini na kuendelea alifariki tarehe 17 / 01 / 2020. Mzee Zakaria ndiye mtanzania pekee aliyekuwa maarufu masikioni mwa watu duniani, enzi hizo Zakaria Ndemfoo na Machame Kisiki vilizagaa kwenye anga duniani na lugha ya kiswahili japo wengi hawakujua alikieneza kiswahili kwa njia ya salamu kupitia redio.
PUMZIKA PEMA MZEE ZAKARIA NDEMFOO.
RIP,yes kipindi hicho nchi ina HESHIMA na ADABU,ila kama nimekosea ninaomba nisahihishwe huyu si alikuwa BABATI?
 
Back
Top Bottom