Tanzia ya Dkt. Dau kwa rafiki yake hayati Benjamin William Mkapa

Sijui haya majibishano yanakujaje hapa. nssf ni taasisi ya umma na inahudumia umma mzima wa watzania.

Hao wafanyakaz wa hapo wanaonana uso kwa macho na hao wananchi kila siku. Watu wanaeleza walichokuwa wanakiona.

Mbona simpo tu.
Actually kilichowapa watu picha ya udini ni kukua kwa idadi ya wanaovaa visuruali vifupi na uchebe na wale wanawake wanaofunika kichwa. Hawa walikuwa wanaonekana kwa macho tu wala si kwa tochi.
 
Point yake naona imeegemea kwenye asilimia. Mfano shirika lina wafanyakazi A 300 na wafanyakazi B 100, baada ya utawala wa jamaa mwenye nasaba na B, wafanyakazi A wakawa 400 na wale B wakawa 350, hapa utaona wameajiri A 100 ,na wale B wameajiriwa 250.

Hapa utaona ingawa wale A bado wao ndio wengi lakini uwiano wa kuajiri umeegemea zaidi kwa wale B. Uwiano wa A:B ni 100:250 yaani katika kila watu A 10 waliojiriwa watu B ni 25.

Kwa hiyo je, ni kweli wakati wa Daktari Dau, uajiri hauku_favour upande wa dini yake zaidi!?

Kwa hiyo ulitaka kwa mfano watu wa dini gani wawe wengi katika kuajiriwa?

Maana yule aliyeajiri watu A 300 na watu B 100 wewe hiyo wala haikusumbui, ila unasumbuliwa na aliyefuata!
 
Actually kilichowapa watu picha ya udini ni kukua kwa idadi ya wanaovaa visuruali vifupi na uchebe na wale wanawake wanaofunika kichwa. Hawa walikuwa wanaonekana kwa macho tu wala si kwa tochi.

Kwa hiyo ulitaka wale wenye kuvaa misalaba na wenye kunena kwa lugha waendelee kuwa wao kwa wingi zaidi pale, hapo roho yako ingekuwa baridiii, imetulia tuli au vipi?
 
DR. RAMADHANI KITWANA DAU ANAVYOMKUMBUKA RAFIKI NA KIONGOZI WAKE RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILLIAM MKAPA

KWA NINI NAMLILIA MZEE BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Dkt. Ramadhani K Dau

Ilikuwa siku ya Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 kiasi cha saa 8 na nusu usiku kwa saa za Tanzania nilipopata simu kutoka Accra Ghana kutoka kwa Dkt. Ken Kwaku aliyekuwa Mshauri wa Rais Mkapa katika masuala ya uchumi kunifahamisha kuwa Mzee Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu amefariki dunia. Kwa hakika nilistushwa sana na taarifa hii kwa sababu mbili.

Kwanza, ni kawaida ya kibinaadamu kuwa kifo hakizoeleki na kila kinapotokea huwa kinastusha. Lakini sababu ya pili ni kuwa jana yake yaani siku ya Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 kiasi cha saa 11 jioni kwa saa za Tanzania nilikuwa nazungumza na mtoto wa mama yangu mdogo Bwana Kheri Abdul Mahimbali kuhusu Mzee Mkapa.

Sikujua kuwa kipindi hicho Mzee Mkapa alikuwa hospitali na alibakisha masaa machache kabla ya kuhitimisha safari yake ya hapa duniani aliyoianza tarehe 12 Novemba 1938.

Baada ya kupata taarifa hizo, haraka nikakimbilia kwenye simu yangu ya kiganjani na kukuta ujumbe kutoka kwa rafiki na ndugu yangu Mwanahistoria maarufu Bwana Mohamed Said.

Katika ujumbe wake, Mohamed alisema:

Balozi itakuwa vizuri uandike tazia (sic). Alikuwa rafiki yako na si wengi wanalijua hili.

Mara tu baada ya kupata ujumbe huo pale pale nikajikuta kuwa umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia kumuenzi Mzee Mkapa ambaye kwa hakika alikuwa mzee wangu wa karibu sana ambaye ameniongoza na kunisaidia mambo mengi; na kama alivyosema Mohamed si watu wengi walikuwa wanalijua hilo.

Mara ya kwanza kukutana na Mzee Mkapa ilikuwa mwezi Juni 2001 ikiwa ni takriban miezi mitano baada ya kuniteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF tarehe 21 Januari 2001.

Wakati huo tulikuwa Geneva, Uswisi kuhudhuria mkutano wa Shirika la Kazi Duniani yaani ILO.

Mzee Mkapa alikuwa miongoni mwa wageni watatu maalum walioalikwa kuwasilisha mada kuhusu ajira mbaya za utotoni (worse forms of child labour).

Baada ya hotuba yake, Mzee Mkapa aliombwa kukutana na wajumbe wa nchi zote za Afrika zilizohudhuria mkutano huo.

Wakati wajumbe wa Afrika walipokuwa wanatoka kwenye chumba kikuu cha mkutano (Plenary Hall) kuelekea kwenye chumba kilichoandaliwa kwa ajili na mkutano na Mzee Mkapa, kipindi hicho Mzee Mkapa aliwekwa kwenye chumba cha muda (holding room) akiwa na wajumbe wote kutoka Tanzania.

Nakumbuka Bwana Naftali Nsemwa, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF alikwenda kumsalimu mahala ambapo Mzee Mkapa alikuwa ameketi akiwa na viongozi waandamizi wa Serikali akiwemo Balozi Ali Mchumo. Katika mazungumzo na Bwana Nsemwa, Mzee Mkapa alimuuliza kuwa amesikia Mkurugenzi Mkuu wa NSSF nae amehudhuria mkutano huo.

Baada ya kusikia hivyo, Balozi Joshua Opanga ambaye alikuwa Mkuu wa Itifaki alitoka na kuja tulipokuwa tumesimama na kutuarifu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF anatakiwa na Mhe Rais.

Huo ndio ulikuwa mkutano wangu wa kwanza kabisa na Mhe Benjamin Mkapa.

Baada ya mkutano ule wa Geneva, nimekutana na Mzee Mkapa mara kadhaa aidha kwenye sherehe mbalimbali au kikazi kwenye ofisi yake Ikulu.

Idadi ya mikutano yetu iliongezeka sana baada ya Mzee Mkapa kustaafu mwezi Disemba 2005.

Mara nyingi tumekuwa tukikutana nyumbani kwake Sea View na baadae Sea Cliff.

Katika mikutano yetu yote, mkutano ambao ninaukumbuka zaidi kuliko yote ni ule tulioufanya nyumbani kwake Sea View mwezi Aprili 2006.

Mkutano huo ulikuwa ni wa kwanza baina yetu baada ya Mzee Mkapa kustaafu.

Siku hiyo nilikwenda kwa Mzee Mkapa kwa mambo mawili.

Kwanza ni kumjulia hali na kumpongeza kwa kumaliza uongozi wa nchi yetu kwa salama.

Pili ilikuwa kumshukuru kwa imani kubwa aliyoionesha kwangu kwa kuniteuwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi kubwa kama NSSF bila hata kunifahamu.

Nilimwambia Mzee Mkapa kuwa kwa bahati mbaya, katika jamii zetu mtazamo wa watu wengi ni kuwa nafasi nyeti kama hiyo huteuliwa mtu ambaye anafahamika sana au ana ukaribu na Rais kwa namna moja au nyingine.

Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF si ya kuteuliwa mtu ambaye hafahamiki kabisa kama nilivyokuwa mimi wakati huo.

Aidha nilimkumbusha Mzee Mkapa kuwa wakati ananiteuwa katika nafasi hiyo hakuwa ananifahamu kabisa na mara ya kwanza ya sisi kukutana ilikuwa miezi mitano baada ya uteuzi wangu.

Nilimalizia kwa kumwambia kuwa ni matarajio yangu kuwa nimekidhi mategemeo yake kwangu; nakumbuka kwa Kiingereza nilimwambia I hope I met your expectations.

Baada ya kusema hayo, Mzee Mkapa alizungumza kwa muda mrefu sana na kutoa yake ya moyoni. Kwanza aliniambia kwa maneno yake mwenyewe:

What do you mean you met my expectations. You exceeded my expectations by far!

Kwa tafsiri isiyo rasmi:

Una maana gani kusema umekidhi matarajio yangu. Wewe umevuka matarajio yangu kwa kiasi kikubwa sana.

Kauli yake hii aliithibitisha katika barua binafsi Kumb FP.III/12 aliyoniandikia tarehe 29 Machi 2007, kunishukuru na kunipongeza kwa kazi kubwa niliyoifanya kuibadili NSSF wakati wa uongozi wake.

Kwa maneno yake, Mzee Mkapa alisema:

. . . nimeshangazwa na kufurahishwa zaidi na maainisho ya maendeleo na viwango vya mabadiliko ambayo umeyabuni, umeyaanzisha, umeyatekeleza na kuyasimamia kwa ujasiri na ufanisi mkubwa. Hakika maendeleo hayo ni mapinduzi thabiti katika fani hii ya hifadhi ya jamii katika uchumi wa nchi. Hongera sana. (msisitizo kama ulivyo kwenye barua)

Umenishukuru kwa uteuzi na imani yangu kwako. Kwa upande wangu nakushukuru kwa kudhihirisha waziwazi hivi kwamba tuna hazina kubwa kitaifa ya wataalamu wazalendo, wenye ujuzi mkubwa, waadilifu na wachapa kazi. Matumaini yangu ni kwamba rekodi yako hii ya kazi ya kutukuka itatambuliwa kitaifa.

Katika mkutano wetu wa Aprili 2006, Mzee Mkapa aliniambia maneno ambayo sijapata kumsimulia mtu yoyote.

Katika mazungumzo yetu, Mzee Mkapa aliniambia kuwa katika teuzi zote alizozifanya akiwa Rais, uteuzi wangu ni miongoni mwa teuzi zilizompa taabu sana kutokana na fitna, uzushi na mizengwe dhidi yangu.

Mara ya kwanza alipotaka kuniteuwa, baadhi ya wazee ambao hakuwataja (nami sikuwa na sababu ya kutaka kuwajua) walimwendea na kumshawishi asiniteuwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kwa sababu mimi ni CUF.

Ushahidi wao ni kuwa nyumbani kwa baba yangu mzazi kuna bendera ya CUF.

Mzee Mkapa akawauliza iwapo natumia uCUF wangu kuhujumu Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kazi zangu za Mkurugenzi wa Masoko Mamlaka ya Bandari.

Wazee wakawa hawana majibu.

Akawauliza iwapo CUF ni Chama ambacho kipo kinyume cha Sheria au Chama ambacho kimepigwa marufuku kwa maana ya outlawed organization. Wazee wakawa hawana jibu.

Akawaambia wazee hao kuwa kuwepo kwa bendera ya CUF nyumbani kwa baba yangu si kosa; na hata kama ni kosa, si sahihi kuhukumiwa mimi kwa “kosa” ambalo amefanya baba yangu.

Wazee wakaishiwa hoja na kuondoka. Mzee Mkapa akanisimulia kuwa haikupita muda akaambiwa kuwa asiniteuwe kwenye nafasi hiyo kwa sababu mimi ni Mujahidina.

Ushahidi wao ni kuwa ninaswali ofisini na kwamba kila mwaka mwezi wa Ramadhani naenda Makka.

Mzee Mkapa akahoji iwapo natumia muda wa kazi kuhubiri dini kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari badala ya kufanyakazi niliyoajiriwa.

Jibu likawa hapana.

Mzee Mkapa akauliza iwapo Uislamu wangu unaathiri kazi zangu kama Mkurugenzi wa Masoko wa Mamlaka ya Bandari.

Jibu likawa hapana.

Baada ya kuridhika kuwa zile zote zilikuwa ni fitna, hatimaye tarehe 21 Januari 2001, Mzee Mkapa aliniteuwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kazi ambayo niliifanya kwa miaka 15 hadi tarehe 15 Februari 2016 wakati Mhe Rais Dkt. John Magufuli aliponipa heshima ya kipekee ya kuniteuwa kuwa Balozi wake katika nchi saba za Kusini Mashariki ya Asia.

Nchi hizo ni Malaysia, Indonesia, Thailand, Philippenes, Brunei, Cambodia na Laos.

Huo ni mfano mmoja tu kati ya mingi ya uadilifu wa Mzee Mkapa.

Leo najiuliza ni vijana wangapi wamekoseshwa fursa mbalimbali kutokana na fitna na uwongo dhidi yao.

Upo usemi maarufu wa Kiingereza unaosema:

“if you want to kill a dog, give it a bad name”.

Kwa tafsiri isiyo rasmi:

“ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina baya”.

Marehemu Mzee Mkapa atakumbukwa kwa mengi sana. Wakati wa utawala wake amefanya mengi ya kuendeleza nchi yetu.

Mengi sana yameandikwa kuhusu mema yake kama mwanadamu na mazuri aliyoyafanyia nchi kama kiongozi.

Lakini yapo mengi ambayo hayajaandikwa au hayapewi uzito ambao ni stahili yake.

Kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, leo nitayataja mambo mawili tu.

Kwanza, Mzee Mkapa alikuwa jasiri sana wa kufanya na kusimamia maamuzi yake.

Hapa nitatoa mifano miwili.

Mfano wa kwanza ni uamuzi wake wa kuwapa Waislamu kilichokuwa Chuo cha TANESCO ili waanzishe Chuo Kikuu chao.

Uamuzi kama huo unahitaji ujasiri mkubwa.

Alifanya hivyo baada ya kubaini kuwa sehemu kubwa ya raia wake wameachwa nyuma sana kielimu.

Kwa uwamuzi huo, Mzee Mkapa alikuwa anaitakia mema nchi yetu kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya juu kwa raia wake wengi ili kuharakisha na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi yetu.

Wapo ambao waliutazama uamuzi ule kuwa ni wa kidini.

Ukweli ni kuwa uamuzi wa Mzee Mkapa ulisukumwa na dhamira ya kudumisha ustawi na amani katika nchi.

Ni uamuzi ambao hoja yake kuu ni ya kiuchumi (economic argument) na pia kuweka mizania sawa katika jamii.

Hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuendelea iwapo idadi kubwa ya raia wake wapo nyuma kielimu.

Katika suala hili tunao mfano mzuri wa China.

Nchi hiyo imepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sababu ya kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya juu kwa raia wake.

Hadi kufikia miaka ya 1980s China ilikuwa na watu chini ya 50 milioni ambao walikuwa na shahada za Chuo Kikuu.

Hivi sasa watu wenye shahada za Chuo Kikuu nchini China wanakadiriwa kufika 500 milioni, idadi ambayo ni zaidi ya watu wote wa Marekani.

Mzee Mkapa aliliona hilo na ndio msingi wa uwamuzi wake wa kuwapa Waislamu Chuo cha TANESCO.

Mfano wa pili wa ujasiri wa Mzee Mkapa ni uwamuzi wake wa kutaka kutatua matatizo ya muda mrefu ya Waislamu baada ya kupokea malalamiko yao wakati wa Baraza la Eid tarehe 19 Januari 1999.

Baadhi tu ya malalamiko hayo ni idadi ndogo ya Waislamu kwenye vyuo vikuu na kwenye ajira katika Taasisi za Umma na Idara za Serikali, kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kutojiunga na Organization of Islamic Conference (OIC) licha ya ahadi aliyoitoa Bungeni aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe John Malecela mwaka 1993 kuwa Zanzibar inajitoa kwenye OIC ili kuipisha Serikali ya Muungano kujiunga na Umoja huo. Wakati wa uongozi wake, akiwa Mwenyekiti wa CCM, Mzee Mkapa aliliweka suala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005-2010.

Aidha Serikali ya Mzee Mkapa ilifanya utafiti wa kina kuhusu faida na hasara za kujiunga na OIC na kubaini kuwa kuna faida nyingi kwa Tanzania kujiunga na Umoja huo.

Kuhusu fursa za ajira, Serikali ya Mzee Mkapa iliagiza kufanywa kwa utafiti kwenye Mashirika yote ya Umma na Idara za Serikali kuhusu uwiano wa ajira nchini.

Nakumbuka wakati huo nikiwa Mamlaka ya Bandari, tulitakiwa na Wizara yetu tufanye utafiti huo na kuwasilisha mapendekezo yetu Wizarani kwa ajili ya kupelekwa kwenye Mamlaka za juu kwa hatua stahiki.

Sifa ya pili ya Mzee Mkapa ni kuwa alipenda sana watu wenye kujiamini na kuhimiza kuwa mabadiliko yoyote ya hali za watu ni lazima yaanzie au yatokane na wao wenyewe.

Kwenye suala hili, Mzee Mkapa alikuwa anapenda sana kutumia usemi wake wa sentensi moja ya maneno kumi yenye harufi mbili mbili.

Sentensi hiyo inasema:

if it is to be, it is up to me

Kwa tafsiri isiyo rasmi:

iwapo nataka jambo liwe, basi wajibu ni wangu mwenyewe.

Mfano wa usemi huu umetajwa kwenye Quran, Sura Ra’ad Aya 11 (13:11) ambapo Mwenyezi Mungu Amesema:

Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf-sini mwao.

Mzee Mkapa ameondoka wakati Taifa linamuhitaji sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika jitihada za kurekebisha uchumi.

Busara za Mzee Mkapa zilikuwa zinahitajika sana katika kipindi hiki kutokana na msimamo wake wa kutumia tofauti zetu kuwa ndio chanzo cha nguvu zetu bila kujali tofauti za mawazo, rangi, dini, kabila nk. kama alivyosisitiza katika hotuba yake aliyoitoa Kigali, Rwanda katika Mkutano wa baadhi ya viongozi wa Afrika uliofanyika kati ya tarehe 19-23 Mei 2014.

Mzee Mkapa alilionesha hili kwa vitendo kwani siku moja mwezi wa Ramadhani wakati wa magharibi Mzee Mkapa alikuwa anamtafuta mmoja kati ya walinzi wake wa karibu.

Baada ya kupewa jibu kuwa ameenda kufuturu, Mzee Mkapa alistuka kwani hakujua kabisa kuwa mlinzi wake wa karibu ambaye amemlinda kwa miaka mingi alikuwa Mwislamu!

Huyo ndio Mzee Mkapa. Kwenye masuala ya kazi na kutoa fursa, Mzee Mkapa alikuwa mwadilifu sana na hakubagua raia wake kwa misingi ya rangi, kabila au dini zao.

Kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla na kwa Waislamu, itakuwa vyema iwapo uongozi wa Chuo cha Waislamu Morogoro ukampa heshima ya kumtunuku Mzee Benjamin William Mkapa Shahada ya Heshima Uzamivu yaani Doctor of Letters (Honoris Causa) posthumously.

Aidha itakuwa vyema iwapo jengo la Utawala (Central Administration) likapewa jina la Benjamin William Mkapa Building.

Kwa upande wa michezo, Mzee Mkapa ametoa mchango mkubwa sana kwa kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa. Kwa kuuenzi mchango wake, nashauri Serikali ibadili jina la uwanja wa Taifa na kuitwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Benjamin Mkapa yaani Benjamin Mkapa Memorial Stadium.

Buriani Mzee Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hakika umeitendea haki nchi yako na raia wake. Daima utakumbukwa kwa mema, busara, ujasiri, umahiri, uadilifu na uungwana wako.

Innallillah Wainnaillahi Raajiuun

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea” (Quran 2:156).
Kumbe kusifia koote huku mimi nilidhani anasifia kwa kuwa marehemu Mkapa alifanya mema kwa wananchi wote kumbe sababu ya kutoa chuo kwa Waislamu,mlinzi wake kuwa muislamu, hakusikiliza majungu kuwa ni mjahidina,mara OIC. Dr Dau na rafiki yake mzee Mohamed ni wadini sana,kila kitu huanzia kwa mtazamo wa kidini.
 
Kwa hiyo ulitaka kwa mfano watu wa dini gani wawe wengi katika kuajiriwa?

Maana yule aliyeajiri watu A 300 na watu B 100 wewe hiyo wala haikusumbui, ila unasumbuliwa na aliyefuata!
Mimi nazungumzia Daktari Dau na uajiri wake. Hao waliopita kabla yake unaweza kuwaelezea wewe.
 
Kumbe kusifia koote huku mimi nilidhani anasifia kwa kuwa marehemu Mkapa alifanya mema kwa wananchi wote kumbe sababu ya kutoa chuo kwa Waislamu,mlinzi wake kuwa muislamu, hakusikiliza majungu kuwa ni mjahidina,mara OIC. Dr Dau na rafiki yake mzee Mohamed ni wadini sana,kila kitu huanzia kwa mtazamo wa kidini.

Angesifu jinsi Mkapa alivyosaidia vigango na Parokia ungeona siyo tatizo.

Waislamu nao ni wananchi tena ndo wa mwanzo kabisa kuunga mkono kwa wingi juhudi za kudai uhuru, wana haki ya kuwa treated fairly katika nchi yao, Kama kudai fairness ndo udini so be it!
 
Mimi nazungumzia Daktari Dau na uajiri wake. Hao waliopita kabla yake unaweza kuwaelezea wewe.

Kuzungumza speculations ni kupoteza muda. Maana tunazungumzia dhahania, ni claims tu zisizo na ushahidi.

Kama ushahidi ni kuwepo kwa waislamu NSSF, sasa ulitaka wawepo akina nani kwa mfano, Wakiristu watupu? hapo roho yako ingekuwa nyeupeee.

Ingekuwa hivyo sasa ungegeuka ungekuja na hoja kuwa "haajiriwi. mtu sababu ya dini yake bali vigezo", yaani all the time nyinyi akipata muislamu nafasi mnaweka question mark hata kama ana vigezo vyote. Ila akipata Mkristu mnaona kuwa hivyo ndivyo inavyopaswa iwe!

Acheni roho mbaya nyinyi!
 
Kwa hiyo ulitaka wale wenye kuvaa misalaba na wenye kunena kwa lugha waendelee kuwa wao kwa wingi zaidi pale, hapo roho yako ingekuwa baridiii, imetulia tuli au vipi?
Wale wanaovaa misalaba ,misalaba yao imenin'ginia nje!? Unawajuaje kama hawajavaa misalaba. Hata hao wenye visuruali vifupi na uchebe hiyo attention wamejiletea wao wenyewe. Nani angejua kama wasingekuwa wanavaa hivyo!?
 
Asante sana kaka

Mtu ukiwa Muislamu na unaipenda dini yako na unaiishi, kuna watu wanachukia sana

Lakini Makonda akienda kanisani akasema nchi hii iko chini ya kanisa, wala huoni wakishtuka na kumuita mdini. Hii ni kwa sababu kwao Maisha ni katika lenzi ya Ukiristo tu na kwamba life inapaswa iwe hivyo, na si vinginevyo. Ukifanya vinginevyo basi wewe ni mdini.

Kwa watu hawa, Ofisi za serikali zikipambwa miti ya Krismasi kipindi cha msimu wa Krismasi siyo tatizo, Ila Muislamu akisali ndani ya ofisi yake muda wa break ya lunch kwake hilo ni tatizo kubwa.

Kwa watu hawa mtu akiweka muziki wa kwaya kwenye computer yake huku akijifanyia kazi yake ndani ya ofisi ya serikali kwao siyo tatizo lakini muislamu akivuta tasbihi, tayari nongwa, maneno kila aina hadi kwa mabosi kuwa fulani ni Mujahidina.

Hapa Dau kamzungumzia mzee Mkapa kama mtu ambaye alikuwa fair, Mtu ambaye hakuwa mdini.

Dau Kazungumzia jinsi Mkapa alivyowapa Waislamu majengo ya TANESCO Morogoro wajenge chuo chao kikuu. Huu ni wema na legacy iliyoje!.

Mkapa alikuwa fair sana na ndiyo maana, akachukua na Majengo ya iliyokuwa benki ya NBC iringa akawapa wakatoliki wajenge chuo cha Ruaha Catholic University

Akatoa Majengo ya iliyokuwa Mazengo Secondary akawapa Waanglican nao wakajenga chuo chao kikuu huko Dodoma

Na akatoa majengo ya Magamba Secondary akawapa Walutheri nao wakajenga chuo kikuu

Huyo ndo Mkapa, Kiongozi bora na fair kabisa.
Dau angezungumzia jinsi gani Mkapa alipambana kutokomeza ukabila na ukanda katika awamu zake zote mbili za uongozi, basi nina hakika uzi huu ungepata wachangiaji wengi ambao wangempongeza Dr Dau kwa kulizungumzia hilo la ukabila, kwa vile ndugu zetu wengi humu wanachukulia ubaguzi ni ile aina ya kabila moja kuwa wengi serikalini dhidi ya makabila mengine na hasa katika kipindi hiki ambapo kila raisi anapofanya teuzi wao hukimbilia kuangalia jina la mteuliwa, kanda anayotoka na kabila lake. Wakigundua kwamba teuzi zimeegemea kanda au kabila la alie wateuwa, basi watakuja mbio mbio humu kulalamika kwamba kanda au kabila lao linabaguliwa (hata kama hawana au hawakuwa na vigezo vya kumshawishi mteuwaji awateuwe) Na wengi wataunga mkono hoja kwamba ubaguzi umetumika katika teuzi, ila ikionekana kwamba teuzi hizo zimeegemea kwenye dini fulan kisha wale wanaohisi kubaguliwa wakileta uzi kulalamikia teuzi hizo hapa jukwaan watashambuliwa na kuambiwa kwamba ni wadini, hawana vigezo, elimu nk, mfano mzuri ni hii mada hapa tayar Dr ashaanza kushambuliwa kwa alichoandika (alichoongea) Mimi ni mkristo lakini malalamiko haya ya ndugu zetu waislam huwa yananigusa na naona kama yana ukweli ndan yake japo inaonekana nobody cares about it. Nimalizie kwa kumtakia pumziko la milele kiongozi wetu mstaafu BWM. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe Daima Milele Ameen
 
Kuzungumza speculations ni kupoteza muda. Maana tunazungumzia dhahania, ni claims tu zisizo na ushahidi.

Kama ushahidi ni kuwepo kwa waislamu NSSF, sasa ulitaka wawepo akina nani kwa mfano, Wakiristu watupu? hapo roho yako ingekuwa nyeupeee.

Ingekuwa hivyo sasa ungegeuka ungekuja na hoja kuwa "haajiriwi. mtu sababu ya dini yake bali vigezo", yaani all the time nyinyi akipata muislamu nafasi mnaweka question mark hata kama ana vigezo vyote. Ila akipata Mkristu mnaona kuwa hivyo ndivyo inavyopaswa iwe!

Acheni roho mbaya nyinyi!
Nitolee roho mbaya yako hapa. Post yangu ya kwanza uliyo_quote mwisho kabisa nimeuliza " Je, wakati wa Daktari Dau, uajiri hauku_favor dini yake!? Hapo ni wapi nimetoa hukumu kuwa alipendelea dini yake!?
 
Dau angezungumzia jinsi gani Mkapa alipambana kutokomeza ukabila na ukanda katika awamu zake zote mbili za uongozi, basi nina hakika uzi huu ungepata wachangiaji wengi ambao wangempongeza Dr Dau kwa kulizungumzia hilo la ukabila, kwa vile ndugu zetu wengi humu wanachukulia ubaguzi ni ile aina ya kabila moja kuwa wengi serikalini dhidi ya makabila mengine na hasa katika kipindi hiki ambapo kila raisi anapofanya teuzi wao hukimbilia kuangalia jina la mteuliwa, kanda anayotoka na kabila lake. Wakigundua kwamba teuzi zimeegemea kanda au kabila la alie wateuwa, basi watakuja mbio mbio humu kulalamika kwamba kanda au kabila lao linabaguliwa (hata kama hawana au hawakuwa na vigezo vya kumshawishi mteuwaji awateuwe. Na wengi wataunga mkono kwamba ubaguzi umetumika katika teuzi, ila ikionekana kwamba teuzi hizo zimeegemea kwenye dini fulan kisha wale wanaohisi kubaguliwa wakileta uzi kulalamikia teuzi hizo hapa jukwaan watashambuliwa na kuambiwa kwamba ni wadini, hawana vigezo, elimu nk, mfano mzuri ni hii mada hapa tayar Dr ashaanza kushambuliwa kwa alichoandika (alichoandika) Mimi ni mkristo lakini malalamiko haya ya ndugu zetu waislam huwa yananigusa na naona kama yana ukweli ndan yake japo inaonekana nobody cares about it. Nimalizie kwa kumtakia pumziko la milele kiongozi wetu mstaafu BWM. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe Daima Milele Ameen

Good observation.

Wadini hasa wakiristo humu JF huwa hawataki kuzungumzia ubaguzi wa kidini katika teuzi na ajira kwa sababu hunufaika na jinsi mazoezi hayo yafanyikavyo ya kufavor watu wa dini zao!

Lakini wadini hao huwa faster sana kukemea teuzi zenye mrengo wa kikabila na kikanda.

Ni wanafiki
 
DR. RAMADHANI KITWANA DAU ANAVYOMKUMBUKA RAFIKI NA KIONGOZI WAKE RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILLIAM MKAPA

KWA NINI NAMLILIA MZEE BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Dkt. Ramadhani K Dau

Ilikuwa siku ya Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 kiasi cha saa 8 na nusu usiku kwa saa za Tanzania nilipopata simu kutoka Accra Ghana kutoka kwa Dkt. Ken Kwaku aliyekuwa Mshauri wa Rais Mkapa katika masuala ya uchumi kunifahamisha kuwa Mzee Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu amefariki dunia. Kwa hakika nilistushwa sana na taarifa hii kwa sababu mbili.

Kwanza, ni kawaida ya kibinaadamu kuwa kifo hakizoeleki na kila kinapotokea huwa kinastusha. Lakini sababu ya pili ni kuwa jana yake yaani siku ya Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 kiasi cha saa 11 jioni kwa saa za Tanzania nilikuwa nazungumza na mtoto wa mama yangu mdogo Bwana Kheri Abdul Mahimbali kuhusu Mzee Mkapa.

Sikujua kuwa kipindi hicho Mzee Mkapa alikuwa hospitali na alibakisha masaa machache kabla ya kuhitimisha safari yake ya hapa duniani aliyoianza tarehe 12 Novemba 1938.

Baada ya kupata taarifa hizo, haraka nikakimbilia kwenye simu yangu ya kiganjani na kukuta ujumbe kutoka kwa rafiki na ndugu yangu Mwanahistoria maarufu Bwana Mohamed Said.

Katika ujumbe wake, Mohamed alisema:

Balozi itakuwa vizuri uandike tazia (sic). Alikuwa rafiki yako na si wengi wanalijua hili.

Mara tu baada ya kupata ujumbe huo pale pale nikajikuta kuwa umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia kumuenzi Mzee Mkapa ambaye kwa hakika alikuwa mzee wangu wa karibu sana ambaye ameniongoza na kunisaidia mambo mengi; na kama alivyosema Mohamed si watu wengi walikuwa wanalijua hilo.

Mara ya kwanza kukutana na Mzee Mkapa ilikuwa mwezi Juni 2001 ikiwa ni takriban miezi mitano baada ya kuniteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF tarehe 21 Januari 2001.

Wakati huo tulikuwa Geneva, Uswisi kuhudhuria mkutano wa Shirika la Kazi Duniani yaani ILO.

Mzee Mkapa alikuwa miongoni mwa wageni watatu maalum walioalikwa kuwasilisha mada kuhusu ajira mbaya za utotoni (worse forms of child labour).

Baada ya hotuba yake, Mzee Mkapa aliombwa kukutana na wajumbe wa nchi zote za Afrika zilizohudhuria mkutano huo.

Wakati wajumbe wa Afrika walipokuwa wanatoka kwenye chumba kikuu cha mkutano (Plenary Hall) kuelekea kwenye chumba kilichoandaliwa kwa ajili na mkutano na Mzee Mkapa, kipindi hicho Mzee Mkapa aliwekwa kwenye chumba cha muda (holding room) akiwa na wajumbe wote kutoka Tanzania.

Nakumbuka Bwana Naftali Nsemwa, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF alikwenda kumsalimu mahala ambapo Mzee Mkapa alikuwa ameketi akiwa na viongozi waandamizi wa Serikali akiwemo Balozi Ali Mchumo. Katika mazungumzo na Bwana Nsemwa, Mzee Mkapa alimuuliza kuwa amesikia Mkurugenzi Mkuu wa NSSF nae amehudhuria mkutano huo.

Baada ya kusikia hivyo, Balozi Joshua Opanga ambaye alikuwa Mkuu wa Itifaki alitoka na kuja tulipokuwa tumesimama na kutuarifu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF anatakiwa na Mhe Rais.

Huo ndio ulikuwa mkutano wangu wa kwanza kabisa na Mhe Benjamin Mkapa.

Baada ya mkutano ule wa Geneva, nimekutana na Mzee Mkapa mara kadhaa aidha kwenye sherehe mbalimbali au kikazi kwenye ofisi yake Ikulu.

Idadi ya mikutano yetu iliongezeka sana baada ya Mzee Mkapa kustaafu mwezi Disemba 2005.

Mara nyingi tumekuwa tukikutana nyumbani kwake Sea View na baadae Sea Cliff.

Katika mikutano yetu yote, mkutano ambao ninaukumbuka zaidi kuliko yote ni ule tulioufanya nyumbani kwake Sea View mwezi Aprili 2006.

Mkutano huo ulikuwa ni wa kwanza baina yetu baada ya Mzee Mkapa kustaafu.

Siku hiyo nilikwenda kwa Mzee Mkapa kwa mambo mawili.

Kwanza ni kumjulia hali na kumpongeza kwa kumaliza uongozi wa nchi yetu kwa salama.

Pili ilikuwa kumshukuru kwa imani kubwa aliyoionesha kwangu kwa kuniteuwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi kubwa kama NSSF bila hata kunifahamu.

Nilimwambia Mzee Mkapa kuwa kwa bahati mbaya, katika jamii zetu mtazamo wa watu wengi ni kuwa nafasi nyeti kama hiyo huteuliwa mtu ambaye anafahamika sana au ana ukaribu na Rais kwa namna moja au nyingine.

Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF si ya kuteuliwa mtu ambaye hafahamiki kabisa kama nilivyokuwa mimi wakati huo.

Aidha nilimkumbusha Mzee Mkapa kuwa wakati ananiteuwa katika nafasi hiyo hakuwa ananifahamu kabisa na mara ya kwanza ya sisi kukutana ilikuwa miezi mitano baada ya uteuzi wangu.

Nilimalizia kwa kumwambia kuwa ni matarajio yangu kuwa nimekidhi mategemeo yake kwangu; nakumbuka kwa Kiingereza nilimwambia I hope I met your expectations.

Baada ya kusema hayo, Mzee Mkapa alizungumza kwa muda mrefu sana na kutoa yake ya moyoni. Kwanza aliniambia kwa maneno yake mwenyewe:

What do you mean you met my expectations. You exceeded my expectations by far!

Kwa tafsiri isiyo rasmi:

Una maana gani kusema umekidhi matarajio yangu. Wewe umevuka matarajio yangu kwa kiasi kikubwa sana.

Kauli yake hii aliithibitisha katika barua binafsi Kumb FP.III/12 aliyoniandikia tarehe 29 Machi 2007, kunishukuru na kunipongeza kwa kazi kubwa niliyoifanya kuibadili NSSF wakati wa uongozi wake.

Kwa maneno yake, Mzee Mkapa alisema:

. . . nimeshangazwa na kufurahishwa zaidi na maainisho ya maendeleo na viwango vya mabadiliko ambayo umeyabuni, umeyaanzisha, umeyatekeleza na kuyasimamia kwa ujasiri na ufanisi mkubwa. Hakika maendeleo hayo ni mapinduzi thabiti katika fani hii ya hifadhi ya jamii katika uchumi wa nchi. Hongera sana. (msisitizo kama ulivyo kwenye barua)

Umenishukuru kwa uteuzi na imani yangu kwako. Kwa upande wangu nakushukuru kwa kudhihirisha waziwazi hivi kwamba tuna hazina kubwa kitaifa ya wataalamu wazalendo, wenye ujuzi mkubwa, waadilifu na wachapa kazi. Matumaini yangu ni kwamba rekodi yako hii ya kazi ya kutukuka itatambuliwa kitaifa.

Katika mkutano wetu wa Aprili 2006, Mzee Mkapa aliniambia maneno ambayo sijapata kumsimulia mtu yoyote.

Katika mazungumzo yetu, Mzee Mkapa aliniambia kuwa katika teuzi zote alizozifanya akiwa Rais, uteuzi wangu ni miongoni mwa teuzi zilizompa taabu sana kutokana na fitna, uzushi na mizengwe dhidi yangu.

Mara ya kwanza alipotaka kuniteuwa, baadhi ya wazee ambao hakuwataja (nami sikuwa na sababu ya kutaka kuwajua) walimwendea na kumshawishi asiniteuwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kwa sababu mimi ni CUF.

Ushahidi wao ni kuwa nyumbani kwa baba yangu mzazi kuna bendera ya CUF.

Mzee Mkapa akawauliza iwapo natumia uCUF wangu kuhujumu Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kazi zangu za Mkurugenzi wa Masoko Mamlaka ya Bandari.

Wazee wakawa hawana majibu.

Akawauliza iwapo CUF ni Chama ambacho kipo kinyume cha Sheria au Chama ambacho kimepigwa marufuku kwa maana ya outlawed organization. Wazee wakawa hawana jibu.

Akawaambia wazee hao kuwa kuwepo kwa bendera ya CUF nyumbani kwa baba yangu si kosa; na hata kama ni kosa, si sahihi kuhukumiwa mimi kwa “kosa” ambalo amefanya baba yangu.

Wazee wakaishiwa hoja na kuondoka. Mzee Mkapa akanisimulia kuwa haikupita muda akaambiwa kuwa asiniteuwe kwenye nafasi hiyo kwa sababu mimi ni Mujahidina.

Ushahidi wao ni kuwa ninaswali ofisini na kwamba kila mwaka mwezi wa Ramadhani naenda Makka.

Mzee Mkapa akahoji iwapo natumia muda wa kazi kuhubiri dini kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari badala ya kufanyakazi niliyoajiriwa.

Jibu likawa hapana.

Mzee Mkapa akauliza iwapo Uislamu wangu unaathiri kazi zangu kama Mkurugenzi wa Masoko wa Mamlaka ya Bandari.

Jibu likawa hapana.

Baada ya kuridhika kuwa zile zote zilikuwa ni fitna, hatimaye tarehe 21 Januari 2001, Mzee Mkapa aliniteuwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kazi ambayo niliifanya kwa miaka 15 hadi tarehe 15 Februari 2016 wakati Mhe Rais Dkt. John Magufuli aliponipa heshima ya kipekee ya kuniteuwa kuwa Balozi wake katika nchi saba za Kusini Mashariki ya Asia.

Nchi hizo ni Malaysia, Indonesia, Thailand, Philippenes, Brunei, Cambodia na Laos.

Huo ni mfano mmoja tu kati ya mingi ya uadilifu wa Mzee Mkapa.

Leo najiuliza ni vijana wangapi wamekoseshwa fursa mbalimbali kutokana na fitna na uwongo dhidi yao.

Upo usemi maarufu wa Kiingereza unaosema:

“if you want to kill a dog, give it a bad name”.

Kwa tafsiri isiyo rasmi:

“ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina baya”.

Marehemu Mzee Mkapa atakumbukwa kwa mengi sana. Wakati wa utawala wake amefanya mengi ya kuendeleza nchi yetu.

Mengi sana yameandikwa kuhusu mema yake kama mwanadamu na mazuri aliyoyafanyia nchi kama kiongozi.

Lakini yapo mengi ambayo hayajaandikwa au hayapewi uzito ambao ni stahili yake.

Kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, leo nitayataja mambo mawili tu.

Kwanza, Mzee Mkapa alikuwa jasiri sana wa kufanya na kusimamia maamuzi yake.

Hapa nitatoa mifano miwili.

Mfano wa kwanza ni uamuzi wake wa kuwapa Waislamu kilichokuwa Chuo cha TANESCO ili waanzishe Chuo Kikuu chao.

Uamuzi kama huo unahitaji ujasiri mkubwa.

Alifanya hivyo baada ya kubaini kuwa sehemu kubwa ya raia wake wameachwa nyuma sana kielimu.

Kwa uwamuzi huo, Mzee Mkapa alikuwa anaitakia mema nchi yetu kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya juu kwa raia wake wengi ili kuharakisha na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi yetu.

Wapo ambao waliutazama uamuzi ule kuwa ni wa kidini.

Ukweli ni kuwa uamuzi wa Mzee Mkapa ulisukumwa na dhamira ya kudumisha ustawi na amani katika nchi.

Ni uamuzi ambao hoja yake kuu ni ya kiuchumi (economic argument) na pia kuweka mizania sawa katika jamii.

Hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuendelea iwapo idadi kubwa ya raia wake wapo nyuma kielimu.

Katika suala hili tunao mfano mzuri wa China.

Nchi hiyo imepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sababu ya kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya juu kwa raia wake.

Hadi kufikia miaka ya 1980s China ilikuwa na watu chini ya 50 milioni ambao walikuwa na shahada za Chuo Kikuu.

Hivi sasa watu wenye shahada za Chuo Kikuu nchini China wanakadiriwa kufika 500 milioni, idadi ambayo ni zaidi ya watu wote wa Marekani.

Mzee Mkapa aliliona hilo na ndio msingi wa uwamuzi wake wa kuwapa Waislamu Chuo cha TANESCO.

Mfano wa pili wa ujasiri wa Mzee Mkapa ni uwamuzi wake wa kutaka kutatua matatizo ya muda mrefu ya Waislamu baada ya kupokea malalamiko yao wakati wa Baraza la Eid tarehe 19 Januari 1999.

Baadhi tu ya malalamiko hayo ni idadi ndogo ya Waislamu kwenye vyuo vikuu na kwenye ajira katika Taasisi za Umma na Idara za Serikali, kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kutojiunga na Organization of Islamic Conference (OIC) licha ya ahadi aliyoitoa Bungeni aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe John Malecela mwaka 1993 kuwa Zanzibar inajitoa kwenye OIC ili kuipisha Serikali ya Muungano kujiunga na Umoja huo. Wakati wa uongozi wake, akiwa Mwenyekiti wa CCM, Mzee Mkapa aliliweka suala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005-2010.

Aidha Serikali ya Mzee Mkapa ilifanya utafiti wa kina kuhusu faida na hasara za kujiunga na OIC na kubaini kuwa kuna faida nyingi kwa Tanzania kujiunga na Umoja huo.

Kuhusu fursa za ajira, Serikali ya Mzee Mkapa iliagiza kufanywa kwa utafiti kwenye Mashirika yote ya Umma na Idara za Serikali kuhusu uwiano wa ajira nchini.

Nakumbuka wakati huo nikiwa Mamlaka ya Bandari, tulitakiwa na Wizara yetu tufanye utafiti huo na kuwasilisha mapendekezo yetu Wizarani kwa ajili ya kupelekwa kwenye Mamlaka za juu kwa hatua stahiki.

Sifa ya pili ya Mzee Mkapa ni kuwa alipenda sana watu wenye kujiamini na kuhimiza kuwa mabadiliko yoyote ya hali za watu ni lazima yaanzie au yatokane na wao wenyewe.

Kwenye suala hili, Mzee Mkapa alikuwa anapenda sana kutumia usemi wake wa sentensi moja ya maneno kumi yenye harufi mbili mbili.

Sentensi hiyo inasema:

if it is to be, it is up to me

Kwa tafsiri isiyo rasmi:

iwapo nataka jambo liwe, basi wajibu ni wangu mwenyewe.

Mfano wa usemi huu umetajwa kwenye Quran, Sura Ra’ad Aya 11 (13:11) ambapo Mwenyezi Mungu Amesema:

Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf-sini mwao.

Mzee Mkapa ameondoka wakati Taifa linamuhitaji sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika jitihada za kurekebisha uchumi.

Busara za Mzee Mkapa zilikuwa zinahitajika sana katika kipindi hiki kutokana na msimamo wake wa kutumia tofauti zetu kuwa ndio chanzo cha nguvu zetu bila kujali tofauti za mawazo, rangi, dini, kabila nk. kama alivyosisitiza katika hotuba yake aliyoitoa Kigali, Rwanda katika Mkutano wa baadhi ya viongozi wa Afrika uliofanyika kati ya tarehe 19-23 Mei 2014.

Mzee Mkapa alilionesha hili kwa vitendo kwani siku moja mwezi wa Ramadhani wakati wa magharibi Mzee Mkapa alikuwa anamtafuta mmoja kati ya walinzi wake wa karibu.

Baada ya kupewa jibu kuwa ameenda kufuturu, Mzee Mkapa alistuka kwani hakujua kabisa kuwa mlinzi wake wa karibu ambaye amemlinda kwa miaka mingi alikuwa Mwislamu!

Huyo ndio Mzee Mkapa. Kwenye masuala ya kazi na kutoa fursa, Mzee Mkapa alikuwa mwadilifu sana na hakubagua raia wake kwa misingi ya rangi, kabila au dini zao.

Kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla na kwa Waislamu, itakuwa vyema iwapo uongozi wa Chuo cha Waislamu Morogoro ukampa heshima ya kumtunuku Mzee Benjamin William Mkapa Shahada ya Heshima Uzamivu yaani Doctor of Letters (Honoris Causa) posthumously.

Aidha itakuwa vyema iwapo jengo la Utawala (Central Administration) likapewa jina la Benjamin William Mkapa Building.

Kwa upande wa michezo, Mzee Mkapa ametoa mchango mkubwa sana kwa kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa. Kwa kuuenzi mchango wake, nashauri Serikali ibadili jina la uwanja wa Taifa na kuitwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Benjamin Mkapa yaani Benjamin Mkapa Memorial Stadium.

Buriani Mzee Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hakika umeitendea haki nchi yako na raia wake. Daima utakumbukwa kwa mema, busara, ujasiri, umahiri, uadilifu na uungwana wako.

Innallillah Wainnaillahi Raajiuun

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea” (Quran 2:156).
Apumzike kwa amani mzee Mkapa
 
Kwani inakuathili nini kuwa na sehemu ya kusali kwenye ofisi ya umma.
Kwa nini kwenye wimbo wa Taifa tunasema Mungu ibariki??? Kama tunakili uwepo wa Mungu kuna shida gani iwe wakristo au hata waislamu wakiweka sehemu yao ofisini kumuomba Mungu.

Mnajifanya mmestaarabika kumbe ni wabaguzi zaidi yaMakaburu
Kwa nini unataka serikali au taasisi ya umma igharamie dini yako? Suala la wewe kwenda peponi ni lako binafsi haliwahusu wengine.
 
Mzee baba lichukuliwe ghorofa ujue wewe media zote zisiandike? Unajua Dr Dau ni balozi wa nchi 7? Kama mmemshindwa kangi lugola sidhani kama mtamuweza Dau, hivi unahisi Dr Dau na kangi nani anawafuasi wengi nyuma yake?
Mbona iliandikwa kwebye media. Mna ubishi usio na kichwa
 
Back
Top Bottom