TANZIA: Sir. George Kahama afariki dunia

Chuo kikuu cha Ushirika ana jengo limepewa Jina Lake .Lecture Hall ipo Karibu kabisa na Hostel aliyeyokua akiishi aliyekua mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda au Daudi Albert Bashite.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM! Is it confirmed au is just an assumption?...
 
Nasikia kwa pamoja waliukutaa msaada wa Misri kujenga chuo kikuu cha kwanza cha kiislam E.Africa na kuyaondoa makao makuu ya umoja wa kiislam E.Africa kutoka Tz to Kenya.
 
Wakuu,

Taarifa nilizopata punde ni kuwa Mzee Kahama amefariki Dunia kama muda mchache uliopita katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili (muda wa saa 10 kamili jioni hii).

254d423a971d2b2c303a79e51ee2afbf.jpg

Clement George Kahama, al-maarufu Sir. George, ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa aliye mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika kudai uhuru mnamo miaka ya 1950, hadi kujitawala mwaka 1961, na baada ya uhuru mpaka alipostaafu utumishi wake kwa umma si miaka mingi iliyopita.

Kahama alipelekwa Uingereza na Chama cha Ushirika wa zao la Kahawa cha jimbo lililoitwa Ziwa Magharibi wakati ule, likiwa na wilaya za Bukoba, Karagwe, Biharamulo na Ngara, na sasa ni mkoa wa Kagera, ili kusomea taaluma ya ushirika na masoko kwa ajili ya maendeleo ya chama kile.

Katika kutimiza dhana yao ya kuzima harakati za Nyerere za kudai uhuru, na kwa vile hakuwa peke yake katika harakati zile, wakoloni walimpatia masurufu yasiyokidhi mahitaji yake akiwa masomoni, kusudi akose uwezo wa kuwasiliana na waasisi wenzake kwa kuwatumia nyaraka kwa njia ya posta.

Alipokwisha taabika kwa muda mrefu akisaidiwa na baadhi ya wanachuo wenzake kutoka Tanganyika waliokuwa katika vyuo mbalimbali vya Uingereza, ndipo alipodokezwa ya kuwa yupo mwenzao aitwaye Clement George Kahama katika chuo kingine kuwa, alikuwa na uwezo kifedha kutokana na kusomeshwa na chama cha ushirika wa zao la kahawa.

Mwalimu Nyerere alifurahi akawa na matumaini ya kusaidiwa, kwanza kwa sababu alikwishaona ushirikiano wa Watanganyika wengine, akajua hata Kahama atamsaidia.

Lakini kwa mujibu wa Sir George, tumaini la Nyerere lilizidishwa na ukweli kwamba, wote wawili ni watani wa jadi.

Tangu walipokutana mpaka waliporejea nyumbani baada ya kuhitimu masomo, gharama zote za kutuma nyaraka za kisiasa kuja kwa waasisi wa harakati za kudai uhuru, zilitolewa na Sir George, kiasi kwamba, hata wenye kujadili ni jinsi gani alipachikwa cheo cha Sir, wanadhani Nyerere kiutani huenda ndiye alimwita vile kutokana na mazingira ya msaada huo.
Ustaadh Mohamed Saidi, njoo utupe darasa juu ya huyu bwana...
 
Back
Top Bottom