Tanzia: Mzee Peter Kisumo afariki Dunia

Tanzia: Mzee Peter Kisumo afariki Dunia

RIP Mzee Kisumo. Kamwambie Mwalimu kuwa ule upinzani wa kweli hatimae mwaka huu umedhihiri. Punde tu atasikia RIP CCM
Akamwambie pia Mwalimu kuwa ule utabiri wake alioutoa miaka 20 iliyopita kuwa upinzani wa nguvu wa kisiasa hapa nchini utatoka ndani ya CCM baada ya chama hicho kumeguka vipande vipande waenda kutimia mwaka huu.

Akamwambie pia Mwalimu kuwa utabiri wake no 2 kuwa watanzania wasipoyapata mabadiliko ndani ya CCM wataenda yatafuta nje ya CCM, utabiri huo pia waenda tekelezwa tarehe 25 mwezi wa 10 mwaka huu, na hivyo kuifanya CCM ivifuate vyama vyenzake vikongwe vilivyoleta uhuru nchini kwao kama vile KANU ya Kenya, UNIP ya Zambia na MCP ya Malawi.
 
Alifanya juhudi kuihujumu KNCU ili ife, yeye pamoja na masisiemu yenzake. Acha afe tu na yeye.. Akalazwe patakapomfaa
Duh....... Mkuu waleta visasi hadi kwa Marehemu?

Kwani hujasoma maandiko kwenye Bible yanayosema tusamehe hata mara 7 mara 70?
 
RIP Mzee Kisumo.

Mzee Kisumo amefariki akiwa ni mwenyekiti wa barza la wadhamni wa CCM.

Moja ya wosia ambao ameacha lakini ukiwa haukupokwlewa kwa shwari ni kuwaambia wazee wengi walio kwenye chama kwamba hawana budi kuwaachia vijana nafasi.

Mzee Kisumo alipokuwa waziri kwenye serikali ya hayati Mwalimu Nyerere mwaka 1965, Cleopa Msuya alikuwa kamishna katika wizara ya fedha wakti huo, waziri mkuu maehemuRashid Mfaume Kawawa, Michael Kamaliza.

Mzee Kisumo ni miongoni kwa viongozi wane waliojiuzulu mwezi January nwaka 1977 baada ya kashfa ya mauaji huko katika mikoa ya shinyanga na Mwanza. Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani, Mzee Siyovelwa nae akiwa waziri wa usalama wa taifa Ikulu nae akajiuzulu, hali kadhalika mzee Peter Kisumo akiwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Marco Mabawa akiwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Baada ya hapo Mwalimu akafanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri kama ifuatavyo:

Waziri Mkuu: Edward Sokoine

Mambo ya Nje : Ben Mkapa

Ulinzi: Rashidi Kawawa

Waziri wa Fedha : Edwin Mtei

Waziri wa Ujenzi: Alfred Tandau

Maliasili: Solomon Ole Saibul

Waziri wa Kazi : Crispin Tungaraza

Kilimo: John Malecela

Ardhi: Tabitha Siwale

Elimu: Nicholas Kuhanga

Sheria : Julie Manning

Habari na Utangazaji : Isaac Sepetu

Utamaduni na Michezo: Mirisho Sarakikya

Mawasiliano : Amir Jamal

Biashara : Alphonse Rulegura

Mambo ya ndani : Nassor Moyo

Waziriwa mitaji : Hasnu Makame

Afya : Leader Stirling

Maji : Al-Noor Kassum

Viwanda : Cleopa Msuya

Utumishi : Abel Mwenga

Ilikuwa kazi kazi tu.
 
Hadi anafariki ndio board chairman wa Vodacom
 
Watanzania

Ni mstuko ndani ya Taifa hili baada ya Mungu kumchukua na kwenda kumhifadhi Mzee wetu Peter Kisumo. Mzee wetu amefariki dakika chache zilizopita.

Tutazidi kuwajuza taratibu zote na baadhi ya Taarifa kadri tutavyobarikiwa kuzipata.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwa. Amen

R.I.P MZEE KISUMO baba mlezi wa Jk na Lowassa kisiasa.

Jk lowassa uso kwa macho msibani,can't wait to c the reaction za marafiki hawa wa zamani.
 
Tupe historia yake kwa ufupi yeye ni nani

siangaliagi TBC...ila jumapili fulani jicho lilikwama kwenye makala moja ikimuonesha bw kisumo(RIP) na harakati zake za kisiasa akiwa mkuu wa mkoa wa Daresalam hapo zamani....moja wapo kuugawa mkoa wa Daresalaam na kuuanzisha mkoa wa Pwani.
 
[h=1]Peter Kisumo, pumzika tu![/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 05 August 2008

Tume yajadili "kirafiki" na mafisadi


kisumo_1.jpg



PETER Kisumo amechoka. Anahitaji msaada. Lakini wale ambao wangempa msaada ni wanafiki. Wanasemea kiganjani. Ni aina ya "kakitandugaho"? wale wasiojiamini na waoga wa kuwa chanzo cha mjadala.
Mshiriki wa siasa za Tanganyika African National Union (TANU) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kisumo amenukuliwa akitetea usiri ndani ya chama chake na bungeni.
Mara hii Kisumo anamkosoa Anne Kilango (Malecela), mbunge wa Same Mashariki kwa kile alichoita kudhalilisha CCM kwa kuishutumu serikali yake kuhusiana na wizi kwenye akaunti ya EPA ya Benki Kuu (BoT).
Kilango alitamka bungeni, kwa nguvu na sauti isiyotiliwa mashaka ya kusikika, kwamba iwapo fedha za EPA hazitarudishwa, pale bungeni "hapatatosha."
Kisumo anasema Anne amekaidi maagizo ya Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba katika kikao cha wabunge wote wa chama hicho, ya kutaka mjadala juu ya EPA kusitishwa. Anasema Makamba aliagiza mjadala juu ya ukwapuaji wa Sh. 133 bilioni kutoka akaunti ya EPA usitishwe lakini Kilango akakaidi.
Tuanzie hapa. Kisumo anataka wabunge wote wawe katika sare ya fikra. Kwamba Makamba akikohoa, basi wote wafyate. Mwenyekiti wao akitabasamu, basi wote wagegeme kwa mtindo wa waigizaji. Siku viongozi wao watakapokuja wanalia, basi na wao walie.
Huu ni uzee mchafu. Uzee usiogundua kuwa unaelekea ukomo; usiotambua na kuthamini kumea na kukua kwa fikra mpya; usiotambua mgongano wa fikra; usiojali thamani uhuru wa kufikiri na haki ya kuwa na mawazo tofauti.
Hata ndani ya chama kimoja, ni muhimu kuwa na mawazo tofauti ambayo yanaweza kukiimarisha badala ya kuendeleza mgando wa fikra ambao ni rahisi kubomoa hata kwa hoja dhaifu.
Kutokemea ufisadi ndani ya chama kinachopanga ikulu, ni kukubali kwamba kuanzia rais, baraza la mawaziri, hadi mwakilishi wa serikali kwa ngazi ya chini kabisa, ama wote ni mafisadi au wananufaika na ufisadi au wanapenda ufisadi.
Hii haiwezi kuwa sahihi. Uongozi wote kitaifa hauwezi kukosa hata mtu au watu wachache wenye fikra tofauti za kujenga chama chao na jamii. Hata hivyo, vyama vya siasa havina utakatifu wowote.
Vyama hivi vinaongozwa na watu wanaofahamika kwa kuwa na roho nzuri au mbaya, kwa ubabe, kwa ulafi, kwa ushirikina, kwa ulokole, kwa wizi, kwa ufisadi, kwa ukahaba, kwa ukondoo na kwa tabia ainaaina.
Katika mazingira haya kuna umuhimu wa kuwa na watu wachache ndani ya chama ambao wana macho yanayoona zaidi ya wenzao; masikio yanayosikia zaidi ya wengine na midomo inayotoa kauli sahihi zenye kuwakilisha nyoyo nyoofu za kukosoa na kuimarisha chama.
Kwa hiyo kushikilia bango kuwa chembechembe za ukosoaji serikali kupitia bungeni sharti zitoke kwenye kambi ya upinzani peke yake, ni kukiri upofu. Ni kukimbia wajibu wa mwanachama wa chama kilichoko ikulu wa kukosoa serikali yake; ni kutafuta ukondoo.
Lakini ni muhimu kukubali hapa kwamba inawezekana upinzani, ndani au nje ya bunge, usione kasoro au uchafu ndani ya serikali. Inawezekana pia kwamba hata ukiyaona hayo, baadhi ya viongozi wanaweza kushindwa kujenga hoja thabiti kutokana na kuminywa na hata kuhongwa peremende.
Uzoefu unaonyesha kuwa wabunge wengi wa CCM wamekuwa wakidharau hoja kutoka upande wa upinzani na wakati mwingine kuzomea na hata kuua hoja maridhawa zenye mantiki na maslahi kwa taifa.
Katika mazingira haya, sauti kutoka ndani ya chama kinachopanga ikulu inakuja kama kiungo kwa "sauti iliayo nyikani." Huu basi siyo upinzani ndani ya CCM, bali hapa ni mahali ambako wanaotawala na wapinzani wao wanakutanishwa kwa hoja kwa kuwa nchi ni yao wote.
Kwa kuzingatia kauli ya Kilango, hakuna lolote alilokosea ambalo linafanya Kisumo aseme kuwa mwanamke huyo "hastahili kuwa hata naibu waziri." Baada ya kusoma kauli ya Kisumo mtu anajiuliza kwa nini achague nafasi ya naibu waziri na siyo Katibu Tarafa au Katibu Kata au waziri kamili.
Inawezekana Kisumo amepata tetesi kwamba Kilango atakwaa nafasi ya naibu waziri? Amesikia Kilango akisema hiyo ndiyo nafasi anayotafuta? Ameambiwa kuwa nafasi hiyo inahitaji ndumila kuwili asiye na mawazo ya kujitegemea?
Kwa fikra za aina hii, Kisumo ataendelea kuchoka. Ataendelea kuzeeka kwa kasi. Atamomonyoka. Ukale alioubeba utamwelemea. Katika mazingira ya sasa, ataisha kama sabuni, ndani ya chama chake ambacho leo hii kinahitaji fikra mpya ili kiweze kuendelea kuwepo.
Peter Kisumo, kwa sasa na baadaye, siyo wa msaada kwa chama chake au upinzani. Aandaliwe zawadi yake kwa utumishi uliopita huku akichagizwa kuelewa matakwa ya akili mpya katika chama chake na minyumbuliko ya kisiasa katika mazingira mapya.


 
Alikuwa mzee poa sana. Nilikutana naye kwenye hospitali fulani nje ya nchi na kukaa naye kama wiki mbili. Jamaa alikuwa anapenda sana kuongea kiingereza. Lakini alijawa hekima. Siku zote niliponana naye alikuwa akinishika mkono kwa muda bila kuuachia akiomba assurance kama atakuwa salama. Kama nakumbuka vizuri alikuwa ana matatizo kwenye moyo na figo. Bila shaka ni hayohayo yaliyomuua.
Yeye ni kati ya watanzania wachache waliokuwa na uwezo wa kwenda nje ya nchi (kwa gharama za serikali na yeye binafsi) na kupata huduma bora na za kisasa, la sivyo angekuwa ni ordinary citizen angekuwa kafariki zamani sana. RIP Mzee Peter Kisumo.
 
Umemaliza safari yako, pumzika kwa Amani mzee wetu!
 
Back
Top Bottom