TANZIA Anna Maulidah Komu Afariki Dunia

TANZIA Anna Maulidah Komu Afariki Dunia

Kinyungu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
22,344
Reaction score
44,941
Kuna taarifa kuwa Anna Maulidah Valerian Komu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya walalamikaji katika shauri la mgawanyo wa rasilimali za CHADEMA, amefariki dunia. Mazishi yatakuwa kesho.

Mama huyu alikuwa mgombea mwenza wa Mzee Freeman Mbowe katika uchaguzi mkuu wa 2005, amekuwa mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA na Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini CHADEMA.
20260429_023238.jpg


1000724757.jpg
 
Kuna taarifa kuwa Anna Maulidah Valerian Komu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya walalamikaji katika shauri la mgawanyo wa rasilimali za CHADEMA, amefariki dunia. Mazishi yatakuwa kesho. Mama huyu alikuwa mgombea mwenza wa Mzee Freeman Mbowe katika uchaguzi mkuu wa 2005, amekuwa mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA na Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini CHADEMA.
View attachment 3581148


View: https://x.com/i/status/2049245166108590493

Akazikwe na msajiri sasa, shenzi kabisa.
 
Mama Maulidah Anna Komu amefariki dunia. Alijiunga na Chadema mwaka 1993 akitokea CCM. Chadema ilimpa fursa mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge wa viti maalumu, Waziri kivuli wa maendeleo ya Jamii, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini, na baada ya kufariki kwa aliyekua Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Sylvester Masinde mama Komu alikaimu nafasi hiyo kwa muda. Hata hivyo, mwaka jana Bi.Maulidah Komu kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa Bodi ya Wadhamini ambao ni Ahmed Rashid Khamis na Said Issa Mohamed, walifungua kesi ya mgawanyo wa mali za Chadema katika shauri la madai namba 8960 la mwaka 2025. Katika kesi hiyo waliomba Mahakama izuie Chadema kufanya shughuli zozote za kisiasa na viongozi wake wazuiwe kutumia mali za chama. Mahakama kuu iliweka zuio kwa viongozi wa Chadema kufanya shughuli zozote za kisiasa na wale waliojaribu kufanya japo vikao vya ndani walikamatwa na Polisi. Pia mahakama ilizuia mali za Chadema zisiguswe, hali iliyosababisha ofisi na magari kuharibika kwa kutotumika kwa muda mrefu. Amri hiyo ilidumu kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kufutwa na Mahakama ya rufani mwezi April mwaka huu. Kama hiyo haitoshi tarehe 04 Oktoba 2025, Maulidah Komu na wenzake walifungua shauri dogo la kuomba mahakama itoe amri ya kuwakamata na kuwashikilia Viongozi wa CHADEMA, akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche, Katibu Mkuu John Mnyika, na viongozi wengine wakiwemo Godbless Lema, Rose Mayemba, Brenda Rupiah, Hilda Newton, Twaha Mwaipaya na Gervas Lyenda kwa madai ya kukiuka amri ya Mahakama. Maombi hayo yaliwasilishwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga. Baada ya yote hayo, hatimaye Mama Maulidah Anna Valerian Komu amehitimisha safari yake duniani usiku huu, na anatarajiwa kuzikwa kesho. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un" (إِنَّا لِلَّٰهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ) 🙏🏽
 
Kuna taarifa kuwa Anna Maulidah Valerian Komu, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya walalamikaji katika shauri la mgawanyo wa rasilimali za CHADEMA, amefariki dunia. Mazishi yatakuwa kesho.

Mama huyu alikuwa mgombea mwenza wa Mzee Freeman Mbowe katika uchaguzi mkuu wa 2005, amekuwa mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA na Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini CHADEMA.
View attachment 3581148

View attachment 3581181
Asante Mungu kumuondoa huyu ibilisi kwenye uso wa dunia.
 
Back
Top Bottom