Tanzia: Mzee Peter Kisumo afariki Dunia

Peter Kisumo ni Veteran CCM wa siku nyingi. Ni group ya kina Msuya, Songambele, Barongo etc. Alishakuwa waziri katika Serikali ya Nyerere kama sikosei Serikali za mitaa. Lakini ame chair boards nyingi baada ya hapo kama SUDECO, TPC, VODACOM, TFA etc. baada ya ku retire ali settle Moshi akafungua kampuni ya kuuza vifaa vya kilimo - Farm Equipments and General Trading.

Huwezi kuitaja CCM katika mkoa Kilimanjaro bila kumtaja Peter Kisumo, alishiriki sana mwaka 1995 katika kutaka kumuingiza JK madarakani.

Kujuwa historia na waasisi wa TAIFA haihitaji uwe na umri mkubwa ni tabia tu ya watu kutafuta taarifa.
 
Mungu ailaze roho ya Mzee Peter Kisumo mahali peme peponi.
 
Alifanya juhudi kuihujumu KNCU ili ife, yeye pamoja na masisiemu yenzake. Acha afe tu na yeye.. Akalazwe patakapomfaa
 
Alikuwa nguzo muhimu ktk mwanzo wa michakato ya kisiasa ya Mh Prof JK
 
RIP Mzee Peter Kisumo, mdhamini wa CCM taifa.
 
namfahamu vizuri nilisomaga na watoto wake shule ya msingi korongoni ana mtoto wake mmoja naye marehemu aliyekua anaitwaga Andwer
ulale mahali pema peponi mzee
 
...jina lake lihimidiwe.Mwenyezi mungu nakuomba umpokee mja wako..apumzike kwa amani.
 
si umwambie mwenzio kuwa ni miongoni mwa wadhamini wa chama kilichotufilisi kimkakati kwa kupinduapindua kila kilicho kizuri.

Nimejikuta nacheka badala ya kusikitika..JF bana..
 
RIP mzee Kisumo. Bora umejipumzikia kwa amani kabla ya Octoba ambapo ungeshuhudia anguko la chama chako ambacho umekitumikia muda mrefu. Ingekuwa ni hudhuni kubwa kulishuhudia hilo lililosababishwa na huyu mliyempa chama akiongoze naye akaweka wahuni kama Nape na wengine ambao wamekiua kabisa.
Ni heri umeshusha mvi zako kwenye mapumziko ya milele bila kuliona hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…