Tanzia: Mwanamuziki nguli na mpiga Ala, Mzee Bakari Selemani Majengo afariki Dunia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Mwanamuziki nguli tanzania na mpiga ala ya kupuliza saxaphone, Mzee Bakari Selemani Majengo amefariki alipolazwa Muhimbili hospitali kwa maradhi ya moyo na pumu Jumamosi 16/09/2017.

Msiba uko kwake Magomeni Mapipa mtaa wa Korongo jirani na Bondeni hotel.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un

Bakari.jpg

=========

SHIKAMOO Jazz Band ‘Wana Chelachela Beat’, ni kundi la muiziki wa dansi lilianzishwa mwaka 1993 kwa kujumuisha baadhi ya nguli wa miondoko hiyo kutoka katika bendi nyingine kadhaa.
Nguli hao ni Salum Zahor, John Simon, Ally Adinani, Athuman Manicho, Ally Rashid, Kassim Mapili na wengine ambao ni marehemu, akina Mohammed Tungwa, Kassim Mponda na Mariam Nylon.

Mbali ya hao, kuna mwanamuziki mwingine nguli katika upulizaji wa Domo la Bata ‘Saxophone’, aliyepitia bendi kadha wa kadha za muziki wa dansi, Bakari Majengo.

Akiwa mmoja wa waasisi wa Shikamoo Jazz, Majengo amechangia mafanikio makubwa ndani ya bendi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuiongezea mashabiki na kuvuta mapromota nje ya nchi.
Majengo anamtaja mzungu aitwaye Ronnie Graham aliyekuwa anafanyakazi katika shirika la Help Age Tanzania, kuwa ndiye chanzo cha Shikamoo Jazz.

Ronnie akiwa HelpAge alikuwa na kamati iliyokuwa na wajumbe kama John Kitime, Mariam Hamdani, marehemu Godigodi ambayo ndiyo iliyowezesha ujaji wa vyombo vya muziki kutoka Uingereza na baada ya hapo Godigodi na Kitime ndio walienda nyumbani kwa Mzee Salum Zahoro na kumtaka akusanye wakongwe wenzie watengeneze kundi lililokuwa chini ya Helpage na kuwa ni njia moja wapo ya shirika hilo kuwezesha wazee kujitegemea.

Anasema kuwa, tangu ajiunge na bendi hiyo ambayo awali maskani yake yalikuwa Tanzania Region, ameshasafiri nayo nchi kadhaa, zikiwamo Kenya na Uingereza.

Ronnie aliamua kuiacha bendi hiyo kutokana na vituko vilivyofanywa na mmoja wa wazee hao bendi ilipoenda Uingereza.

Kutokana na waanzilishi wengine kuwa wameshafariki, ni wanamuziki wanne tu wanaoiendesha Shikamoo Jazz Band sasa, ambao ni Salum Zahor, John Simon, Ally Adinani na yeye mwenyewe.
Akizungumzia historia yake kimuziki, Majengo anasema kuwa, mwaka 1954 ndipo alipoanza kujiingiza kwenye fani hiyo kwa kujiunga na bendi ya Dar es Salaam Jazz, akiwa mkung’utaji Tumba.

Kabla ya hapo, Majengo anasema kuwa, alikuwa akipiga ngoma kwenye vibendi vya watoto na kutumbuiza katika sherehe mbalimbali za kichama, kwenye ofisi za TANU.

Baadhi ya wanamuziki waliompokea Dar es Salaam Jazz, ni pamoja na Edward Salvu na Grey Sindo waliokuwa mahiri kwa upulizaji Sax, ambao kwa nyakati tofauti walichangia kumnoa kwenye chombo hicho.

Ilipofika mwaka 1963, marehemu King Michael Enock aliingia Dar Jazz na kumuongezea ujuzi wa kupuliza Sax kwa kiwango kikubwa.

Mwaka 1968 aliondoka Dar Jazz akiwa keshashiriki kupiga Sax kwenye vibao vingi, kikiwamo kile maarufu, ‘Mtoto Acha Kupiga Mayowe’, akajiunga na bendi ya Wakongoman watupu iliyoitwa King Afrika.

Mwaka 1969 alijiunga na bendi nyingine ambayo nayo ilikuwa ya Wakongoman, iliyoitwa 60 Zaire, kabla ya mwaka 1970 kuingia Nova Success ya Papaa Micky, saksafoni katika nyimbo kama Chlorida na kadhalika ni kazi ya Majengo.

Aliachana na Nova Success mwaka 1974, bendi ilipopata safari ya Swaziland ambapo yeye alishindwa kwenda kutokana na ajira aliyokuwa nayo katika kiwanda cha BATA Shoes, jijini Dar es Salaam. Alifanyakazi kazi kwenye kiwanda cha BATA tangu mwaka 1963.

Mwaka 1975 aliingia Maquis Original ‘Wana Kamanyola’ iliyokuwa chini ya mpulizaji Sax hodari, Chinyama Chiaza, akashiriki kurekodi vibao vingi zaidi vya bendi hiyo, huku mwenyewe akisifu kazi aliyoifanya katika wimbo ‘Nimepigwa Ngwala’.

Akiwa Maquis, mwaka 1986 alisimama kufanyakazi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifua na alipopata nafuu, alikwenda kumsaidia mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ aliyekuwa kaanzisha bendi yake ya Orchestra Double O.

Chinyama alipobaini hilo, alimfuata na kumuomba arudi Maquis, ambapo siku aliyorejea kazini alikuta bendi iko chini ya Tshimanga Kalala Assosa ambaye wakati huo walikuwa hawajuani.

“Nilisalimiana naye kikawaida lakini nilipotaka kupanda jukwaani alinizuia akitaka nimsujudie kumuomba kwa vile yeye ndie Kiongozi, baada ya majibizano nilisusa na kusimama bendi,” anasema Majengo.
Majengo anasema kuwa, alipokuwa kasimama kuitumikia Maquis, siku moja alitembelea onesho la pamoja na OSS ‘Wana Power Iranda’ na mmiliki wa OSS, Huggo Kisima alipomuona akamvuta kwake, na Septemba 1986 alianza kazi rasmi na wanamuziki Muhidin Gurumo, Skassy Kasambulla na Abdallah Kimeza ndani ya OSS na kushiriki kurekodi nao vibao vingi vikiwamo ‘POP’ na ‘Mbu’.

Mwaka 1990 alirudi tena Maquis na kushiriki nao hadi mwaka 1993 alipoachia ngazi rasmi na kuwa mmoja wa waanzilishi wa Shikamoo Jazz.

Tofauti na wanamuziki wengi wanaotupa lawama kwa vyombo vya habari kuhusiana na kudidimia kwa dansi, Majengo anaweka wazi kuwa, ubinafsi wa wanamuziki wenyewe ndio chanzo.

Majengo anasema kuwa, kila mmoja kwenye muziki wa dansi anajijali yeye mwenyewe na wanamuziki wake tu na kwamba ushirikiano uliopo ni wa mdomoni si wa vitendo.

Faida aliyoyapata Majengo katika kazi ya muziki anayoielezea kuwa ni ngumu kufanikiwa kwa sasa, ni kufanikiwa kujenga nyumba maeneo ya Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa familia, Majengo anayefurahia watoto wake kutorithi kazi yake ya muziki, ana mke na watoto watano, ambao ni Selemani, Kassim, Juma, Zubeda na Tunu.

Alizaliwa mwaka 1943, Kariakoo, jijini Dar es Salaam na kupata elimu ya msingi katika shule ya Mchikichini kwa miaka miwili ya 1949 na 50.

Mwaka 1955 ilipoanzishwa shule ya Magomeni Mzimuni, alilazimika kuanza tena darasa la kwanza hadi la nane mwaka 1962.

TANZIA: Mwanamuziki Nguli wa hapa nchini aliyewika katika kupiga ala ya kupuliza Saxaphone, Bakari Selemani Majengo amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Pumu. Msiba uko Nyumbani kwake maeneo ya Magomeni Mapita mtaa wa Korongo jirani kabisa na Bondeni Hoteli.

Mazishi ya Mzee Bakari Selemani Majengo yatakuwa leo huko Visiga Mkoani Pwani.

======

Back
Top Bottom