TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

Bakwata ni Ukafiri
waislamu na uislam wao bhana...yaan ni manung'uniko na fujo kila mahal, dunia nzima. huwez kuta hawa jamaa wameridhika. mara hawa wameteka msikikiti, mara wale hawamtaki shekhe mkuu, yaan ni shaghalabalha
 
Haya mambo ya kuzika watu wakiwa wa moto (hai) yamepitwa na wakati. Dunia ya leo watu wanaishi mbali, wanafanya kazi mbali, wanasoma mbali huko Ulaya na kwingineko. Yaani hata watoto wasishuhudie mazishi ya mzazi wao; mambo gani haya. Labda FaizaFoxy na Ritz watatusaidia kwenye hili.

Hata akizikwa wa moto ndo atafufuka au marehemu atapata thawabu ? Huo ni utaratibu wa watu wa kushoto. Ambao wakifiwa wanashona sare, fulana, matarumbeta, wachukuwa video, wapiga picha na waandika risala na mashairi
Uislaam hauna hayo. dudus
 
Last edited by a moderator:

Kwanza natoa mkono wa pole kwa bakwata na waislam wote wa Tanzania kufuatia msiba mzito wa mpendwa wao,kiongozi wao.Lakini ningependa kuwaasa wanasiasa hasa watangaza nia wa ccm kutoutumia msiba huo kujinufaisha na kufanikisha ndoto na tamaa zao za kisiasa.Nayasema Haya kama tahadhari kutokana na ukweli kwamba katika miaka hii ya karibuni tumekua tukishuhudia wanasiasa hasa wa ccm wakizitumia nyumba za ibada pamoja na viongozi wa nyumba hizo kujipatia umaarufu wa kisiasa.Sasa kwa kuwa huu ni msiba wa kiongozi mkubwa kabisa wa dini ni wazi wapambe wa wagombea watakua katika harakati za kuuteka msiba na kuufanya ni jukwaa la kufanyia kampeni zao.Mara hii Tunaomba hili lisifanyike tuweke heshma kwa msiba kwa kuwa sisi sote hata wataka urais ni marehemu watarajiwa.

Nawasilisha.
 
Kama marehemu mwenyewe alijiingiza katika siasa enzi za uhai wake utazuia vipi hayo yasitokee.

Nilitegemea watampumzisha leo matokeo yake mpaka Alhamisi, hapa katikati tutashuhudia mengi, hii ina provide loop kwa wanasiasa kufanya yao.
 
Tukiwaambia Viongozi wa Bakwata ni kambi ya CCM hamtaki kuamini leo kifo cha Mufti kimetuonyesha mengi hata kuvunja misingi ya dini kwa sababu za kisiasa. Hata mfalme wa Saudia alizikwa siku hiyo hiyo pasipo kumsubiri Obama ama viongozi wa kimataifa na huyu alikuwa sii kiongozi wa dini bali kiongozi wa nchi.
 
Imetangazwa rasmi kupitia TBC Taarifa ya Habari kuwa maziko ni kesho saa Tisa Alaasir
Nawasilisha
 
Ninapenda kuungana na Waislam wote walioguswa na Msiba huu mzito.

Aidha, wakati tunaomboleza na kutafakari jinsi ya kumuenzi, ni vema mwenye CV yake atuletee hapa jukwaani.

Tunapoamua kumuenzi tujue tunamuenzi mtu wa hali ipi? Amesomaje? Ana level ipi ya ilim dunia.
 
Ili upate manufaa gani? Mwache marhum apumzike kwa amani. Tuwekee CV yako wewe uliye hai.
 
Back
Top Bottom