TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

Kisheria anatambulika kama mkuu wa waislam wote Tanzania, uwe unamkubali au humkubali yeye ndie kiongozi mkuu wa waislam wote Tanzania.

Hakuna mwingine anaetambulika kisheria kama kiongozi wa waislam.

Hujakosea huyo atakua hajitambui. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI. Poleni sana waislamu.
 
bakwata sijui wanaipeleka wapi dini ya kiislam, mtu amekufa juma tatu asubuhi wanamuweka hadi alhamisi ndio wamzike hii ni halali kweli? utamaduni na maamrisho ya kiislam hayako hivyo kabisa, wanachelewesha mazishi kwa sababu ambazo hazina mashiko kwa upande wa dini
 
RIP mufti ulikuwa kiungo muhimu kati ya Waislam na wasio Waislam
 
Kwa waislamu wameondokewa na Sheikh aliyekuwa muungwana sana....na msomi mkubwa mwenye ufahamu mkubwa mno.Mimi ni mkristu ki imani lakini nilipata kupita mikononi mwa Mzee huyu hakika Muungwana huyu kutoka kigoma mwenye Maisha yake kimakazi Shinyanga alikuwa na mengi mazuri sana yenye kupendwa na wanajamii wengi hasa Wazengo wenzie waliokuwa wamezunguka kabla ya kuwa Sheikh Mkuu na baada ya kuwa Sheikh Mkuu.

Sifa kubwa ya Sheikh huyu ni jinsi alivyokuwa anajali sana Elimu Dunia...yani Elimu ya darasani...alikuwa radhi yeye watoto wake waende darasani na kushiriki michezo kwa kushrikina na wanafunzi wengine bila kujali huyu ni imani ipi.Watoto wake wa kike kwa kiume wamesoma elimu ya darasani kiwango kikubwa sana hakika kusikia watoto wake wa ndani mwake kuwa ana PHD si jambo la ajbu manake bintii yake mmoja anaitwa Zainabu last time namuona alikuwa anasotea Masters.

Nilipendezwa na Mzee Simba kwa jinsi alivyokuwa anajali Ilim aliyokuwa akipenda kuitamka na kwa kubalikiwa sauti kubwa na nzito..apumzike kwa amani na maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu sana.Pole Zai kwa kuondokewa na Baba Kipenzi...
Sheikh Issa shaban Bin Simba.jpg
 
Hakika allah ana anayochukua na kutoa na sisi wote kwake tutarejea.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.

Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.

"Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja" amesema .

Amesema Waziri Mukangara: "Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu.

Aidha, kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina."

Imetolewa na;
Idara ya Habari(MAELEZO)

 
nipo kwake Shinyanga ni majonzi mtaa mzima. Mungu ampe pepo njema!
 
Mkulu yuko nje lazima awepo kwenye mazishi wampige picha.

Pia wanasubiri watia nia (mamvi) wafike kuuza fizi msibani.
So sad!!! wanavunja mafundisho ya dini kwa ajili ya siasa?Wanauvuruga Uislamu.Mufti angezikwa leo leo kuonyesha kuwa uislamu haubagui katika mafundisho yake.
 
Muda mfupi uliopita nimepata taarifa kuwa Kiongozi Mkuu wa Waislamu nchini Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia.

Hakika ni majonzi na pigo kubwa kwa Waislam na watanzania kwa ujumla. Amezaliwa Shaaban na ameondoka ndani ya mwezi wa Shaaban,Innalilah wainailah Rajiun.

Mwenyezi mungu ampe kauli thabiti na amjaalie pepo ya kheri na kumsamehe madhambi yake.

The Grand Muft of Tanzania has passed away.





poleni sana ndugu zangu / zetu wa kiislamu kwa kuondokewa na kiongozi wenu lakini pia poleni watanzania wote kwa kupatwa na msiba huu mzito wa kiongozi wa juu kabisa wa kidini hapa nchini tanzania. tupo pamoja ktk kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
 
Haya mambo ya kuzika watu wakiwa wa moto (hai) yamepitwa na wakati. Dunia ya leo watu wanaishi mbali, wanafanya kazi mbali, wanasoma mbali huko Ulaya na kwingineko. Yaani hata watoto wasishuhudie mazishi ya mzazi wao; mambo gani haya. Labda FaizaFoxy na Ritz watatusaidia kwenye hili.
Hiyo si itikadi ya Kiislamu!!!!!
Mtu akifa anatakiwa aoshwe,asaliwe na azikwe,that's all.Kuchelewesha kuzika kwa ajili ya watoto na ndugu walioko mbali si itikadi ya kiislamu hiyo!!!
Bakwata wametia aibu ya MWAKA na wamedhihirisha kuwa hawasimamii dini ila maslahi ya kidunia.
 
kuna tetes mufti simba kafariki yule wa bakwata,,mliopo eneo la tukio mtujuze

mmeshaanza sasa kutuchanganya! watanzania sijui tupoje. mleta uzi yupo very clear kwa taarifa yake na isitoshe hata ktk vyombo vyote vya habari taarifa hii ya msiba huu mzito imekuwa confirmed sasa nakushangaa wewe unavyotaka kulazimisha iwe kama vile ni tetesi. hebu tujaribu kuwa na utamaduni wa kuwaheshimu watu wanaotuletea habari za muhimu, nyeti na za uhakika kwani kwa kutowaamini kutawavunja moyo na siku nyingine wanaweza wakawa na taarifa nzuri zaidi na wasitushirikishe.
 
ungesema poleni waislamu wa BAKWATA ungeeleweka vizuri. sio waislamu wote wengine ni shura ya maimamu tanzania. hawamjui kabsaaa MAREHEM MUFT ALAZWE MAHALA ANAPOSTAHILI

"Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania litakuwa ndiyo chombo pekee cha kuongoza Waislamu na litakuwa na kauli ya mwisho katika kulinda, kutetea na kueneza Uislam na nadharia yake Nchini kwa mujibu wa Qur-aani na Sunna."

Mkuu hiyo ni nukuu ya katiba ya bakwata.
 
Mungu awape subira katika kipindi kigumu cha kuondokewa na Kiongozi wenu mkuu!!
 
Back
Top Bottom