Tanzia: Mtangazaji wa DW, Mohammed Dahman afariki dunia

Tanzia: Mtangazaji wa DW, Mohammed Dahman afariki dunia

Kwani yule mohamed ambae kwa sasa ameshastaafu alikuwa na sauti nzito nzito fulani nae ni mwingine tofauti na huyu au ni wawili tofauti
nadhanai dw walikuwepo kadhaa wenye majina ya Mohamed mfano: Mohammed Ahmed, Mohammed Abdulrahman, Mohammed Khelef na huyu Mohammed Dahman mie nawakumbuka hao
 
Kwani uko DW kuna nini maana uyu ni wa pili kutoka tanzania ndani ya mwaka huu.
R.I.P Dahman.

Kwani wanaofariki wote Dunia hii unapata taarifa?

Kuna watu wanapata taarifa ya msiba wa ndugu mwingine wakiwa kwenye msiba wa ndugu.

Alimradi kifo kipo nasi daima...mambo kama hayo hutokea.
 
Mimi ni msikilizaji mzuri wa DW ingawa karibia Watangazaji wote nawafahamu kwa sauti zao tu.

Watangazaji kama Sudi Mnete, Urmur Kheri, Nkamiti Kibayasi, Sizia Mwehozi...kwa kuwataja wachache.
 
nadhanai dw walikuwepo kadhaa wenye majina ya Mohamed mfano: Mohammed Ahmed, Mohammed Abdulrahman, Mohammed Khelef na huyu Mohammed Dahman mie nawakumbuka hao
namuelewa sana Mohammed abdurahman
 
Sikuwahi kuiona post hii.
Mahali ninapoishi frequency zina shida na hivyo siwezi tena kukamata Radio DW Swahili na hivyo nin miaka zaidi ya 15 bila kuisikiliza.

Kwa watangaziaji wanaotumia lugha ya Kiswahili, kwangu huyu alikuwa ni mtangazaji namba moja duniani; alikuwa ana sauti ambayo sijawahi kuisikia kwa mtangazaji mwingine yoyote yule hapa duaniani; mbali na namna ya usomaji wake ulivyokuwa ni wa kufurahisha sana. Nimesikitika sana kwa kumkosa.

Nimejaribu pia ku-search clips za zamani za sauti yake alipokuwa yupo kwenye matanagazo, lakini sijafanikiwa kuzipata.

Naomaba kama kuna mtu anazo aniwekee hapa ili niweze kubaki na kumbukumbu ya sauti yake

Kwa watangazaji wa zamani; hapa nchini, mtangazaji mwingine wa kike ambaye naweza kumfananisha na huyu ni binti aliwahi kuwepo Radio One miaka ya 94---; alikuwa anaitwa Blandina Mugezi. Huyu mtu sijui alipotelea wapi; possibly alienda kufanya kazi nje ya nchi. Huyu na Dahman waliatkiwa wafanye kazi kwenye kituo kimoja.

Miaka ya kuanzia 94 ilikuwa ikitokea Radio One studio kukawa na Charles Hilary na Blandina Mugezi, unaweza ukaahirisha kwenda kwenye Lecture
 
Taarifa za kifo cha mtangazaji mwenzetu Mohammed Dahman, aliyeaga dunia siku ya Ijumaa (02.08.2019) mjini Cologne, magharibi mwa Ujerumani, zimeishtua timu nzima ya Idhaa ya Kiswahili ya DW mjini Bonn.
View attachment 1171318
Mohammed alikuwa mwandishi habari mahiri katika nyanja zote, lakini alipendelea sana taarifa ya habari za ulimwengu na makala ya mbiu ya mnyonge.

Asilimia kubwa ya wasikilizaji walizipenda sana makala zake kuhusu masuala ya haki za binadamu na sauti yake ya huruma. Aliwapa sauti wasiokuwa na saut, hakukata tamaa kuwatafuta watu muafaka wa kuwahoji na alikuwa makini sana katika kuhakikisha taarifa zake pamoja na makala haziegemei upande mmoja.

Kama mwandishi, Mohammed alikuwa mfano wa kuigwa kwa wengi wetu. Amekuwa akiugua kwa kipindi cha takriban miaka miwili na muda wote huu hakuweza kufanya kazi. Hata hivyo hatukukata tamaa kwamba angepata afueni na kurejea kazini kujumuika nasi kuendelea na majukumu yake.

Katika wakati huu mgumu wa majaribu, fikra na dua zetu tunazielekeza kwa mke wake, binti yake na familia yake visiwani Zanzibar na ughaibuni. Tunawapa pole na kutoa rambirambi zetu kwa majonzi makubwa, machozi yakitiririka machoni mwetu. Tunawaombea. Tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt, na wafanyakazi wote wa idhaa hii mjini Bonn tunawapa pole jamaa, marafiki na mashabiki kwa kuondokewa na mpendwa wetu.

(Andrea Schmit; Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW)
Huyu watangazaji wenzake wa DW-Swahili walikuwa wamempa nickname ya SAUTI YA DHAHABU


View: https://www.youtube.com/watch?v=-l7DOCLrG4k&pp=ygUabW9oYW1tZWQgZGFobWFuIGR3IHN3YWhpbGk%3D

Isikilize sauti hiyo kwenye clips hizi hapa kwenye makala zake alizokuwa anatangaza za MBIU YA MNYONGE



 
wanapiganaaaa misumari semaa watz unakuta weupeeee wanawahiwaaa ...
RIP Mwamba
Kifoooikifooo kifoo hakinaaa hurumaaaa kifoo hakina dhambiii...
 
Huyu ndiye mtangazaji ambaye kwa upande wangu mimi, hakuna mtangazaji mwingine ambaye ameshavunja rekodi ya sauti yake hapa duninani, labda kwenye sayari zingine, kama wapo watangazaji wengine huko
 
wanapiganaaaa misumari semaa watz unakuta weupeeee wanawahiwaaa ...
RIP Mwamba
Kifoooikifooo kifoo hakinaaa hurumaaaa kifoo hakina dhambiii...
Nashauri muwe mnaangalia pia tarehe za nyuzi mnazochangia, kabla ya kuchangia
 
Nashauri muwe mnaangalia pia tarehe za nyuzi mnazochangia, kabla ya kuchangia
Hatakama n mwakajuzi wengine hatukuisoma kama ulisoma wewe huzuii wengine kutoa maoni
Ov
 
Back
Top Bottom