Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,225
- 8,780
"INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN"
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zaTanzania zinatangaza kifo cha Maalim Rashid Ayoub Mshana aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa Vyombo vya Dola Jumamosi January Tarehe 25, 2020.
Maalim Rashid ni Mmoja wa Mahabusu akitokea Mtwara Tanzania, walioshikiliwa na Vyombo vya Dola na ni miongoni mwa mamia ya Waislamu walioko Gerezani kwa kesi za kidini wakituhumiwa kwa kosa la Ugaidi lakini kesi zao hazijapatikana ushahidi na wala hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.
Kama walivyokuwa Mahabusu wengine wakikabiliwa na hali mbaya za kiafya amefariki wakati ambao wenzake wanaendelea kuugua.
Mwili wa Maalim Rashid mpaka mchana wa leo ulikuwa bado upo mikononi mwa vyombo vya Dola na hatimae mida ya Alasiri ya leo imekabidhiwa kwa Waislamu kwa ajili ya mazishi.
RATIBA YA MAZISHI
Marehemu ataandaliwa na kuswaliwa katika Msikiti wa Kichangani Magomeni mida ya saa 6:55 Adhuhuri Kichangani. Aidha, mnamo majira ya saa 7:15 mwili wa marehemu utaelekezwa katika Makaburi ya Mwinyi Mkuu kwa ajili ya Mazishi.
WITO
Tunaomba wale wote walioguswa na msiba huu kuhudhuria. Pia, tunaomba upatapo taarifa hii mfikishie mwingine ili walau apate nafasi ya kutabaruku japo kwa kugusa Jeneza hili linaloingia katika historia kubwa.
Wabilahi Tawfiq.
"HAKIKA SOTE NI WA ALLAH NA MAREJEO YETU NI KWAKE"
Sheikh Ponda Issa Ponda.