Tanzia: Maalim Rashid Ayoub Mshana afariki akiwa mahabusu

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,229
8,780
"INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN"

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zaTanzania zinatangaza kifo cha Maalim Rashid Ayoub Mshana aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa Vyombo vya Dola Jumamosi January Tarehe 25, 2020.

Maalim Rashid ni Mmoja wa Mahabusu akitokea Mtwara Tanzania, walioshikiliwa na Vyombo vya Dola na ni miongoni mwa mamia ya Waislamu walioko Gerezani kwa kesi za kidini wakituhumiwa kwa kosa la Ugaidi lakini kesi zao hazijapatikana ushahidi na wala hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.

Kama walivyokuwa Mahabusu wengine wakikabiliwa na hali mbaya za kiafya amefariki wakati ambao wenzake wanaendelea kuugua.

Mwili wa Maalim Rashid mpaka mchana wa leo ulikuwa bado upo mikononi mwa vyombo vya Dola na hatimae mida ya Alasiri ya leo imekabidhiwa kwa Waislamu kwa ajili ya mazishi.

RATIBA YA MAZISHI
Marehemu ataandaliwa na kuswaliwa katika Msikiti wa Kichangani Magomeni mida ya saa 6:55 Adhuhuri Kichangani. Aidha, mnamo majira ya saa 7:15 mwili wa marehemu utaelekezwa katika Makaburi ya Mwinyi Mkuu kwa ajili ya Mazishi.

WITO
Tunaomba wale wote walioguswa na msiba huu kuhudhuria. Pia, tunaomba upatapo taarifa hii mfikishie mwingine ili walau apate nafasi ya kutabaruku japo kwa kugusa Jeneza hili linaloingia katika historia kubwa.

Wabilahi Tawfiq.

"HAKIKA SOTE NI WA ALLAH NA MAREJEO YETU NI KWAKE"

Sheikh Ponda Issa Ponda.
 
Hivi kwanini mara nyingi na mara zote ni upande wa dini ya kiislamu zaidi ndio hukumbwa na visanga vya kujihusisha na ugaidi?

MArehemu kaenda wacha akakutane na maswaaba wake na wanawake wenye macho makubwa mazuri ambao kama watanyoosha kidole kimoja tu hapa duniani nasikia wanaume wote tungeweza acha wake zetu.

sikejeli ila ni maneno ambayo ni ahadi kutoka kitabu chao kitukufu

anyway poleni wote mlioguswa na msiba
 
Kila MTU atakufa uwe kafir uwe muumini lakini ubinadamu ni kitu kizuri kwa kila mmoja wetu chuki zisikufungie ndani ushindwe kuiona haki na kuifuata!!!
 
Hivi kwanini mara nyingi na mara zote ni upande wa dini ya kiislamu zaidi ndio hukumbwa na visanga vya kujihusisha na ugaidi?
MArehemu kaenda wacha akakutane na maswaaba wake na wanawake wenye macho makubwa mazuri ambao kama watanyoosha kidole kimoja tu hapa duniani nasikia wanaume wote tungeweza acha wake zetu.

sikejeli ila ni maneno ambayo ni ahadi kutoka kitabu chao kitukufu

anyway poleni wote mlioguswa na msiba
Huyu Amefanya UGAIDI gani??au ugaidi wake kuwa muislamu ??
 
Nazidi kuelewa kwanini hatuendelei huku watu Weusi.

Apumzike kwa Amani.

Nimewahi kuona jinsi mtu wa Karibu alivyotoka Mahabusu akaumwa saana kupita maelezo.

Akaonesha baadhi ya maherahi aliyopatiwa...uzuri au ubaya.Waliohusika walifanya conclusive judgment juu ya tukio flani.

Kwa weledi wao na mtazamo wao...kuna mengi ya kujifunza.Na wamejisikia vibaya sana baada ya tendo lao baya maana ni majirani wakirudi toka kazini.
 
Hivi kwanini mara nyingi na mara zote ni upande wa dini ya kiislamu zaidi ndio hukumbwa na visanga vya kujihusisha na ugaidi?
MArehemu kaenda wacha akakutane na maswaaba wake na wanawake wenye macho makubwa mazuri ambao kama watanyoosha kidole kimoja tu hapa duniani nasikia wanaume wote tungeweza acha wake zetu.

sikejeli ila ni maneno ambayo ni ahadi kutoka kitabu chao kitukufu

anyway poleni wote mlioguswa na msiba
Mzee ni lini unaona mshabiki wa liver akiisifia man u? Ishu za hao watu ni ngumu kwa sababu serikali haitaki hata kesi zitangazwe, pili ni muda mrefu umepita ila watu hawatiwi hatiani, ndio maana kuna watu wanaamini kuna uonevu unafanyika
 
Mkuu kwani marehemu bado alikua MTUHUMIWA? Maana kesi ya kitambo ile. Kama bado alikuwa mtuhumiwa waja hatuna haki kumhukumu kama gaidi!!! Na ingebidi tupaze sauti hizi kesi ziishe. Maana kama kweli walihusika na ushahidi upo ni kwa nini kesi ichukue muda mrefu kuisha?
 
TZ hii chini ya uongozi wa madhalimu CCM . Mtu kaenda kuposa mtoto wa mtuhumiwa wa Huo uitwao ugaidi , kaambiwa naye ni Gaidi na yuko ndani zaidi ya miaka 5 sasa
 
Back
Top Bottom