TANZIA: Leticia Nyerere afariki dunia

TANZIA: Leticia Nyerere afariki dunia

fmlyimo

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
331
Reaction score
210
leticia.jpg

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere amefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki..

Msiba upo DMV 9004 Brightlea Court, Lanham, MD 20706.

Leticia aliolewa kisha kutengana na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu.

Leticia alikuwa mtoto wa Mzee Musobi Mageni.

Julai 27 2015, Leticia alitangaza kuihama CHADEMA na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi,
Amina.
 
Hizi habari zinaukweli wowote?maana nakumbuka wiki mbili zilizopita zililetwa tena hivi hivi mwisho ikawa jii.
 
Alikuwa amelazwa USA
 
Attachments

  • 1452494765088.jpg
    1452494765088.jpg
    46.1 KB · Views: 137
  • 1452494780262.jpg
    1452494780262.jpg
    47.2 KB · Views: 122
R.I.p Mbunge viti Maalum Chadema pole kamanda Mbowe na wanachama wote wa Chadema.
 
aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia chadema mama leticia nyerere is no mere
Kwa kuwa aliisha jiondoa CHADEMA tangu july 2015, hivyo kutumia neno aliyekuwa Mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA sio mahala pake ni vema mkaandika aliyekuwa mwanachama wa CCM na msiihusishe CHADEMA kwani hadi mauti yanamkuta huyu alikuwa CCM.
 
View attachment 316118
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere amefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki..

Msiba upo DMV 9004 Brightlea Court, Lanham, MD 20706.

Leticia aliolewa kisha kutengana na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu.

Leticia alikuwa mtoto wa Mzee Musobi Mageni.

Julai 27 2015, Leticia alitangaza kuihama CHADEMA na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mungu ailaze roho ua Marehemu mahali pema peponi,
Amina.
R.I.P Leticia Nyerere
 
Dah huyu mama kila siku anatangazwa kafa vipi ukiitwa nyerere lazima kifo chako kiwe cha utata tu ??
 
Back
Top Bottom