TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

Mnazareth

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
3,447
2,000
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo. Mtoto wa amarehemu amethibitisha kifo.

Rwakatare.jpg

Mtoto wa Marehemu Mama Rwakatare, Mutta Rwakatare amethibitisha kwa kusema

"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.

Marehemu alikuwa kiongozi wa kiroho, mmiliki wa Shule za St. Mary's na pia mwanasiasa.

Mwaka 2007, Mama Rwakatare aliingia kwenye siasa rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Marehemu Salome Mbatia aliyekufa kwa ajali. Soma Mchungaji Getrude Rwakatare amrithi marehemu Salome Mbatia - JamiiForums

Aidha, Mwaka 2017 aliteuliwa tena kuwa Mbunge wa Viti Maalum akichukua nafasi ya Sophia Simba. Soma Dr. Getrude Rwakatare ateuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum nafasi ya Sofia Simba - JamiiForums

Matukio mengine:

Mwaka 2012, Mama Rwakatare aliichongea JF Bungeni. Soma Mama Lwakatare aichongea JamiiForums

Mwaka 2013, Mama Rwakatare alifiwa na Mumewe, Mzee Kennedy Rwakatare. Soma TANZIA: Mch. Getrude Rwakatare amefiwa na mumewe

=============

Tutakukumbuka kwa mchango wako kwenye nyanja za elimu na jamii kwa ujumla.

Umepigana vita na mwendo umeumaliza

Upumzike kwa amani!!


RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Ikulu.jpg


TAARIFA YA BUNGE
Bunge.jpg


WASIFU WA MAMA RWAKATARE

0.33440300 1494232974.png


Hon. Rev. Dr. Getrude Pangalile Rwakatare

Phone : +255679997051

P.O Box : P. O. Box 8844, Dar es Salaam

Email Address : g.rwakatare@bunge.go.tz

Date of Birth : 1950-12-31

Education History :

School Name/LocationCourse/Degree/AwardFromToLevel
Mood Bible Institute , Chicago, USABachelor of Arts in Theology (Mass Com.)19841988Bachelor Degree
North London PolytechnicDiploma in P/M19741975Diploma
Railways' CollegeCertificate19711972Certificate
Korogwe Girls Secondary SchoolCSEE19651968Secondary School
Ifakara Girls Primary SchoolCPEE19611964Primary School
Mbingu Primary School-19571960Primary School


Employment History :
Company/InstitutionPositionFromTo
Tanzania Harbours AuthorityPersonnel Manager19701983
Pan African Christian Women AssemblyChairperson19891993
Mountain of Fire Assemblies of GodPastor19952017
St. Mary's International SchoolsDirector19962017
St. Mary's Teachers CollegeDirector20032017
Mountain of Fire Assemblies of GodPresenter20042017

Political Experience :

Political PartyPositionFromTo
Parliament of TanzaniaMember of Parliament20172020
Parliament of TanzaniaMember of Parliament20072010
Parliament of TanzaniaMember of Parliament20102015
Chama cha MapinduziGuardian to the District Women Wing20052005
Community Development Committee of the ParliamentMember20072010
Social Services Committee of the ParliamentMember20102015

PIA SOMA
Mchungaji na Mbunge Getrude Rwakatare azikwa na Serikali kanisani kwake (Mlima wa Moto) na watu wasiozidi 10 - JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom