TANZIA: Baba mzazi wa Balozi Dk Wilbroad Slaa, Mzee Peter Qamara Tluway (98) afariki dunia

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,564
2,000
Baba mzazi wa balozi wa Tanzania nchini Sweden Dk Wilbroad Slaa, mzee Peter Slaa amefariki dunia, Mkuu wa Wilaya ya Arusha (DC), Gabriel Daqarro amethibitisha.

R.I.P

slaa+pic.jpg

Peter Qamara Tluway (98), baba mzazi wa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbroad Slaa amefariki dunia jana Jumatatu Novemba 18, 2019 kwa ugonjwa wa moyo.

Yasinta Aloyce ambaye shemeji yake Dk Slaa amesema Tluway alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa zaidi ya miezi nane.

"Amekua akipata matibabu ya ugonjwa wa moyo katika hospitali tofauti na hatua ya mwisho madaktari walikuwa wanakuja nyumbani kuangalia hali yake ila mara ya mwisho walikuja na kukuta ameshafariki dunia,” amesema Yasinta akibainisha kuwa Dk Slaa ameshapatiwa taarifa za msiba huyo na ameanza safari kurejea nchini.

Yasinta amesema mazishi yatafanyika Novemba 23, 2019 katika kijiji cha Ayalabe wilayani Karatu.

Chanzo: Mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom