TANZIA: Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''
View attachment 830443
View attachment 830484
View attachment 830455
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Pia soma >
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.


Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.


rest in peace king majuto one of the best in east africa
 
Kifo hauna huruma,

Tutakukumbuka Daima Milele.

Wote kifo kinatungoja,kifo hakiepukiki.

Nasi Twafaata.
 
Ndio kwanza napata TAARIFA hivi punde baada ya kuingia JF.

JF inatusaidia sana.

Sikuwa na TAARIFA kabisa.

JEMBE Mzee MAJUTO hatunae tena.

Nakumbuka enzi zake na BI CHAU kwenye VIPINDI vya LUNINGA.

Jamani
 
Nimeaikitishwa sana na taarifa hizi. Sikutegemea iwe mapema hivi.

Inal llah waina illah rajuun
 
RIP King Mjuto. Tanzania will never ever have another comedian of your sort and your gap will never get filled. May the Almighty God rest your soul in eternal peace. Amen.
 
Kila nafsi itaonja umauti Mbele yetu mzee wetu nyuma yako sisi,kilicho kikubwa kwa sasa tulio baki ni kumuombea Dua tu.Eeee mwenyezi Mungu mfanyie wepesi mzee wetu uko aliko...
 
Back
Top Bottom