SoC01 Tanzanite kama Sarafu Mtandao Afrika

Stories of Change - 2021 Competition

Muharam12

New Member
Sep 1, 2021
2
3
WATU maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wanasumbuka kupata 'kiwakilishi' sahihi na bora kwenye kubadilishana bidhaa toka dunia kuumbwa.

Baada ya uwepo wa DOLA ya Kimarekani na EURO ya Ulaya watu wakadhani mapambano hayo yamefikia tamati. La hasha, bado yanaendelea !

Baada ya majaribio ya kadi mbalimbali, sasa dunia imeingia kwenye kutumia sarafu zisizoshikika kwenye kompyuta au simu zao za mkononi kwa jina la 'Crypto Currency'.

UMUHIMU WA MASOKO YA BIDHAA NA YALE YA FEDHA

FEDHA inahitajika ili jamii mbalimbali ibadiishane bidhaa.

Kama ndivyo, basi masokoo ya bidhaa na yale ya fdha na vitu kama hivyo yatandelea kuwa muhimu kwa wanadamu siku zote, ingawa kwa namna na sura au hali tofauti.

Pengine itakuwa busara kwa serikali na vyombo vyetu vinavyohusika na masuala ya masoko ya fedha kama vile benki kuu, benki nyingine na taasisi za elimu kujiongeza kwenye kuchangia kufunza na kuendeleza vijana wetu ili wawe ni kati ya watu bora duniani kwenye masuala ya masoo ya bidhaa, fedha au sarafu.

Kwa maneno mengine ili maendeleo ya nchi yetu na watu wake siku zote iwe ni kitu cha uhakika ni lazima nchi yetu na watu wake wawe juu kwenye masuala ya ujuzi na maarifa ya tehama, masoko ya fedha na ubadilishanaji fedha na bidhaa duniani.

Historia kama ufunuo vinaonesha kwamba vigezo vya kitu kutumika kama sarafu aminiwa, aghalabu, imekuwa ni uhakika thamani yake. Mchanga na mawe ya kawaida pengine kwa kuwa havina thamani, aghalabu, havitumiki kama sarafu ulimwenguni.

Ila vitu kama dhahabu; shaba; almasi; vitambaa vya hariri au vitu kama hivyo; ngozi au nywele za wanyama adimu vilikubalika. Kama vile magamba ya viumbe kama viumbe vya baharini au konokono na pembe za wanyama (kama ilivyokuwa kwa pembe za tembo au faru leo) au bidhaa adimu kama chumvi vivyo hivyo navyo vilikubalika.

Siri kubwa kwa vitu vinavyokubalika kama sarafu, aghalabu, ni kitu hicho kuwa adimu na hivyo kuwa na thamani kubwa kuliko vitu vingine inavyofanana navyo.

Dhahabu na Marekani

Baada ya Marekani kufanikiwa kudhibiti vyanzo vya dhahabu toka sehemu mbalimbali duniani na kuihusisha dhahabu na thamani ya sarafu yake iitwayo DALA, fedha ya Marekani ndipo ilipoanza kuwa na nguvu kuliko sarafu nyengine duniani na kukubalika, aghalabu, kote duniani.

Swali la kujiuliza hapa ni je, zoezi la kuendelea kuwa na sarafu zinazoshikika na zisizoshikika ulimwenguni lilikufa baada ya kuzaliwa na kustawi kwa DALA ya Marekani kuliko sarafu nyingine duniani ?

Ninaamini hili limeendelea kuwa vivyo hivyo, kwa sababu Marekani imeendelea kujiongeza kiintalijensia, kimaarifa na kuilinda ubora wa matofali yake ya dhahabu yaliyoko kwenye hazina yake ya wengine wafe wao wapone FORT KNOX.

BENKI KUU YA TANZANIA inahitaji kutoka nje ya boksi na kutokufikiri na kupanga sawasawa na nchi nyingi za Kiafrika. BOT sasa ianze kuiga Benki Kuu za Marekani, Uchina, Russia, Japani, Australia na nchi kama hizo. Ianze kwa kuwa na eneo maalum makao makuu Dodoma na jengo litakaoweza kuhifadhi Tanzanite yote ya Tanzania na madini mengine ya thamani na adimu tutakayogundua hapo baadaye. Ieleweke hata almasi na dhahabu vinaweza kuwa ndio tena viko kwenye mwanzo wa mwisho wake.

Eneo la Mererani liongezewa ulinzi maradufu wa kiteknolojia na kiintalijensia na mizigo kati ya Mererani itasafirishwa na ndege maalum ya Kijeshi katika vipindi visivyojulikana na mtu yeyote, isipokuwa Gavana wa Benki Kuu na viongozi wa juu wa nchi.

TANZANITE kama sarafu

Tanzanite inayopatikana Tanzania ina sifa kuzidi dhahabu na uadimu wa Tanzanite unaifanza uwe chaguo la kwanza duniani endapo dhahabu duniani itafikwa na janga lolote. Sintostajaabu kukuta kuna mataifa ambayo yameanza kulimbikiza Tanzanite ili wafanye haya ninayozungumza. Ila sidhani kama tumechelewa sana. Tujaribu kuishi maono ya Magufuli, zaidi ya yeye alivyoweza kubashiri.

Isitoshe, hatua za msingi zimekwishachukuliwa. Ikiwemo kuzungusha ukuta na ulinzi unaoendelea kuboreshwa kila kuchwao.

Ili, Tanzanite iwe na uwezo wa kuwa sarafu inayokubalika Afrika sio tu Tanzania iilinde kwa jino na ukucha. Bali Tanzania inastahili kutoa ulinzi wa Jeshii la Wananchi na Benki kuu ya Tanzania kuhakikisha hata punje ya Tanzanite inafichuliwa kokoote iliko na kuhifadhiwa kwenye: " FORT TANZANITE DODOMA. "

WAKATI hili linafanyika, viongozi wetu wasizungumze kwa maneno bali wazungumze kwa vitendo. Watanzania waliojipambanua kwenye TEHAMA na teknolojia ya mawasiiano hususan crypto currrency, masoko ya hisa, taaluma za fedha na mabaddilishano ya sarafu wahamasishwe na wawezeshwe kuja na 'crypto currency' ya TANZANITE ambayo itaanza kuuzwa mara moja kwenye intranet ya Tanznia na kisha mtandaoni kwa kutumia teknolojia zenye usalama wa hali ya juu kama ilivyo kwa sarafu nyengine kama hizo duniani. Hata kama itabidi kuwanunua Warussia au Waarabu au Wachina au Wamarekani.

Hali kadhalika, Tanzanite kama Crypto currency ianze kutumika mara moja kwa shughui za uchumi wa ndani badala ya kuhamisha shilingi toka hazina taifa kwenda mikoani, sasa, crypto currency itumike kwa biashara kati ya hazina, wizara, mikoa, wilaya na miji. Hii sintoshangaa likipunguza wizi na rushwa kwa kiasi kikubwa nchini.

Mafanikio ya ndani katika matumizi ya Tanzante kama Crypto currrency yachangie kuifanza sarafu hiyo kutumika kwanza Afrika Mashariki, kisha SADC, Afrika Mashariki na ya Kati; Afrika Magharibi na hatimaye Afrika nzima ili kufanikisha shughuli za soko huru la Afrika kuelekea 2050.

Kutokana na haya upo umuhimu Ikulu kuifanya ofisi yake maalum ya mawasilliano kwa TEHAMA iwe na vifaa vitakavyoundwa na kuendeshwa na watalaamu wetu wenyewe ili usalama kwenye mambo haya uwe wa hali ya juu kabisa.

Mawasiliano kati ya Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha budi yawe ni sehemu nyeti na muhimu katika uendeshaji mawasiiano kati ya Ikulu na Benki ya TANZANITE au benki ya fedha za Kitanzania mtandaoni.
 
Back
Top Bottom