Wale ambao wana data za watalii ambao wamekuja Tanzania toka 2000 mpaka 2005 hebu tuandikieni hapa.Halafu tuelezeni ni kiasi gani cha fedha za watalii katika miaka hiyo kimeingia katika mfuko wa serikali?
Ndio Defunkadelic, Tanzania ina utajiri mwingi sana lakini sisi wenyewe hatujui nama ya kuutumia! Kwa mfano hii gesi nyingine ambayo imegunduliwa sasa hivi tayari kuna wataalamu wamenza kusema Tanzania haiwezi ku-develop hii gesi yenyewe bila ya msaada kutoka Kenya na Uganda ili kuweka bomba la gesi. Hata hivyo wawezekaji hao hao wanasema gesi yetu sio nyingi. Sasa kwa nini hatuitumii nchini ili tupunguze gharama za mafuta?
Wawezekaji wa kigeni wamevamia madini yetu hasa dhahabu. Makaa ya mawe aaaa.Chuma aaaaa. Faida kubwa iko kwenye dhahabu kwa nini waweke fedha zao kwenye Chuma na Makaa ya mawe kuisaidia Tanzania?
Self criticism ndio kitu ambacho sisi watanzania tunatakiwa kufanya. Bila self criticism hatutaendelea popote. Rasi JK anajitahidi kwenda huku na huku kuwatafuta hao wawezekaji, mfano ni kiwanda cha Ethanol amapcho Sweden imeahidi kujenga:
Tujiulize hapa je Tanzania tunazo gari (mabasi na magari ya kawaida) ambayo yatatumia hiyo ethanol? Sweden tayari wanazo gari hizo na bei yake ni ghali mno.Balozi wetu ambaye yuko Sweden amefanya utafiti huu. Ni watanzania wangapi ambao watakuwa na uwezo wa kununua gari hizo. Kwa nini SAAB haileti gari zinazotumia gesi badala ya kujenga kiwanda kama hicho cha ethanol au tupate vyote(kiwanda na hizo gari za gesi).
Mmmh. That figure of Tourism, ningependa kuona pia. Pia ningependa kujua foreign policy ya kuvutia watalii. Kwanza naamini kabisa, wazungu ndio wanatengeneza pesa zaidi yetu kutokana na utajiri wa mbuga za wanyama etc. Watu wananunua packages huku huku ulaya, wanaofanya kazi za kuzungusha watu ni wabongo (kina Juma, Massawe etc), kwahiyo pesa inalipwa ulaya, wabongo wanapewa mabaki. Je serikali inaangalia vipi ku-encourage wawekezaji wa kiTanzania, wajichomeke nawenyewe ulaya, wafanye biashara kama wazungu, na pesa zionekane kufaidisha Tanzania zaidi? Au hata wafanya biashara wa kiTanzania wenyewe, what is their game plan? cos me am bit tired of looking for tourist for tourist companies back home....'mshikaji nitafutie wazungu basi'...yeah, i love doing that, lakini, hebu think bigger basi duuh!!
What is the foreign policy on education? Umeongelea gesi na kuleta wakenya/waganda. Let me tell you an interesting fact. Kenya has no oil/gas (maybe prospective, or discovered recently), lakini Shell has been based in Kenya for umpteen years. Hell, they even have Shell refineries. REFINERY IN KENYA??? WHY?? Kuna msichana nilikuwa naye chuo kimoja, mkenya, sasa hivi yuko anafanya Shell Kenya. Kuna mshikaji nimesoma naye (Mnigeria), sasa hivi yuko Shell UK. Na yeye ananiambia/anashangaa, hivi imekuwaje kuwaje waKenya wakawa na refinery? Halafu anakutana na waKenya wengi hapa Shell UK, lakini anajua hawana mafuta. Lakini hata siku moja hajakutana na mTanzania (ofcourse nina uhakika kuna waTanzania wapo wameshaingia Shell). This is putting things into perspective. So what is our policy on educating people to run our own things? Kwasababu with the years of giving/winning scholarships to/for people to study abroad (example kusoma mambo ya Agriculture pale Wageningen University Holland), how do we use these people? Kwasababu sioni maendeleo.
Kuna University hapa UK zenye course ya Petroleum Engineering, haziwezi kufunction bila kuwa na WaNigeria kiasi fulani. Kama mTanzania na mNigeria anapply, same qualifications, mNigeria atachukuliwa (trust me, this is inside information....). WaTanzania policy yetu niaje? Au tutaendelea kuleta wazungu wenye HND diploma tukifikiria ndio degree na uzoefu (wakati huku hawana market)?
Dr. Khamis, hicho kiwanda cha Ethanol ndio nasikia kwako. And that sounds like them White Elephant (is that the correct word? Nimesahau kidogo) projects. Wewe watu wata-afford magari ya Ethanol, wakati bado tuna-import 2nd hand kutoka Uarabuni na Japan? Wazungu wenyewe hapa hawawezi ku-afford sasa hivi (Oil =Petrol/Diesel is the cheapest form of energy at the moment for running cars/or for other usages, and it will remain that way, mpaka wazungu waishiwe mafuta).