Tanzania's CAG Report; March 2012

Mkuu Pasco,
Hiyo lunch yenu ni ya kozi ngapi manake masaa karibia matatu umekaa kimya. Hapo kwenye ofisi za Bunge hakuna chips dume na juice ili ukamate haraka haraka na kurudi kwenye kikao?
 
nchi hii ina viongozi wapumbavu sana...ni sawa na wewe pasco uvue shati lako kisha ulitundike dirishani halafu uzunguke nyuma ya nyumba na kuanza kunyata taratibu kuelekea pale ulipolitundika shati..kisha ukalikwapua na kukimbia nalo....

umeua kila kitu mkuu
 
Pasco Pasco...

Una deni huku, wengine tuko mbali mkuu, tunategemea sana ma-feed back ya watu kama wewe... Hatupendi pia kuyasomea kwenye on-line news!!
 
Yani kila saa napita hapa kucheki updates lakini nashangaa Pasco ametuacha kwenye mataa vibaya mno!
Kama umekumbana na "changamoto" mkuu tueleze tu tuache kusubiria
 
wakuu badala ya kuanza kusoma 7mb worth of paperwork kuna ambae ameshasoma amwage summary hapa.., na hii ni kwa faida ya wanaotumia simu na modem za kuazima (hatutaki kumaliza salio la wenye modem, utakuwa sio ustaarabu)
 
Wakuu ripoti hii hapa, watu waanze kuogelea.
Mkuu Halisi, sio siri, kusoma nondo hizo na kuzielewa kunahitaji uwezo fulani, nyinyi wenye uwezo tunaomba, usaidizi wenu kwenye hili, mtutafunie tuweze kumeza!.
 
Huu wote ni upuuzi tu! Hakuna lolote ambalo CAG amelisema ambalo halijawahi kusemwa; hakuna lolote analosema serikali imefanya au kushindwa kufanya ambalo halijawahi kusemwa kabla. Wanaoambiwa ni watu wale wale, wa chama kile kile na Bunge linaongozwa na watu wale wale! Ni upuuzi tu wangetaka kudhibiti matumizi ya fedha wangeshadhibiti mwaka wa kwanza wa JK madarakani!
 
source mwananchi


Hivi hizi hela zinaenda wapi na wanazikopa za nini?

mbona wakati wanaenda kukopa hawatwambii ila tunaambiwa tunapodaiwa kula wale wao kulipa tulipe sisi
 
Huu wote ni upuuzi tu! Hakuna lolote ambalo CAG amelisema ambalo halijawahi kusemwa; hakuna lolote analosema serikali imefanya au kushindwa kufanya ambalo halijawahi kusemwa kabla. Wanaoambiwa ni watu wale wale, wa chama kile kile na Bunge linaongozwa na watu wale wale! Ni upuuzi tu wangetaka kudhibiti matumizi ya fedha wangeshadhibiti mwaka wa kwanza wa JK madarakani!

lakini angalau wanatufungua macho.
 
Kwa hali ilivyo ndugu zangu kila mtu kwa imani yake na kwa kadri anavyoweza ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani si zaidi ya 2015 vinginevyo tutakwisha. Kwenye ripoti hiyo bado kuna suala la deni la taifa kuongezeka kwa zaidi ya 30% kwa mwaka mmoja wa fedha, jamani hizo hela zote zinaenda wapui? hakuna nchi inayoendeshwa bila kukopa sawa, lakini ukikopa unapeleka wapi? hatuoni viweanda vikifufuliwa, hakluna uwekezaji wa amaana kwenye nishati, kila siku ngeleja na megawati, kama deni linjaongezeka kwa kununulia mashangingi, jamani kuendelea na CCM tunachimbia kaburi tukiwa hai. Suala la ukwapuaji na matumizi ya hovyo hakuna namna ambayo CCM watakwepa hii ni swerikali ya chama chao na rais ndiyo mwenyekiti wa chama, hivi CCM mnatupeleka wapi?
Ee mola tusaidie mbinu za namna ya kuiondoa CCM ibaki chama cha upinzani tu isife.
 
Alafu inauma pale unapoambiwa unadaiwa while wakati wa kuchukua mkopo hukuwa notified kama mwananchi!
 
Back
Top Bottom