Mbona hamsemi saa ngapi? Kwa huku East Africa?
Nilivyouona uzi huu nikagoogle kujua mambo hayo. Kwa ufupi ni saa nane hivi hapa EAT, kwa Dar na Tanzania kwa ujumla imeandikwa ni Partial Solar Eclipse, kwa maana ni kiasi kidogo na yawezekana mtu usihisi chochote. Ila Uganda kuna baadhi ya maeneo watapata Total Solar Eclipse, wakati ambapo Ghana na Ivory Coast watapata Maximum Total Solar Eclipse giza kabisa, hali hiyo ya maximum itashuhudiwa kwa muda wa dakika1 na Sekunde39.