Ndugu nakushangaa sana unapoorodhesha nchi zinazoruhusu Uraia pacha bila ya kutambua ya kwamba kila nchi ina Vipaumbele vyake yaani kila nchi kuna mambo ambayo inaona ni muhimu hizo nchi za Kiafrika ulizozitaja wao wameona umuhimu wa Uraia pacha sisi kwetu bado hatujaona na hakuna tatizo lolote hapo!
Nitakupa mfano mdogo sana umetaja Marekani kwamba ina ruhusu uraia pacha lakini unajua Sheria ya Marekani inasema nini kuhusu Uraia pacha?
Kama haufahamu ni hivi kama wewe ukiwa raia wa Marekani halafu ukaamua kuchukua Uraia wa nchi nyingine tusema TZ na unaishi TZ basi ni lazima pia ulipe kodi Marekani yaani kwa maana nyingine ulipe kodi mara mbili (nchi unayoishi na Marekani) na kwa Marekani ni lazima ulipe 30% ya Mshahara wako kodi, sasa ni kwa nini wameamua hivi?
Na jibu lake ni rahisi wao kama Marekani wameona raia wao kuwa uraia pacha hawafaidiki kama nchi na ili wafaidike basi ni lazima wanaochukua uraia wa Marekani na wanaishi nje ya Marekani pia walipe kodi Marekani na ndio hata sisi (mimi binafsi) tunasema maadamu Diaspora aliamua mwenyewe kwa hiari yake kwa manufaa yake binafsi kuchukua Uraia wa nchi nyingine basi pia hatuwezi kumwacha tu anvyoamua yeye kwa matakwa yake mwenyewe na siku anayotaka yeye kuwa Mtz au la, HAPANA na ndio maana Serikali imesema aliyeukana UTZ basi siku akirudi TZ atakuwa utambulisho wa Makazi maalumu, kumbuka huyo Muomani unayemuongelea ametimiza masharti ya Uraia wa TZ, ni rahisi kihivyo tu!