Tanzania yatajwa kuwa sehemu bora ya uwekezaji

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Jarida maarufu la biashara na linalofuatiliwa duniani kote la Business Insider lenye Makao Makuu yake Jijini New York, Marekani limeitaja Tanzania kuwa moja ya mataifa machache ulimwenguni yanayokua kwa kasi kwa sasa kwenye uwekezaji ambayo ni sehemu bora na salama zaidi kwa uwekezaji.

Jarida lenye uzoefu wa miaka 16 lililojikita kwenye utafiti wa habari za kibiashara na kifedha. Februari 14, 2023 ilichapisha kwenye mtandao wake ikisema mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji yaliyowekwa na Rais Samia Hassan yametuma ujumbe mzuri kwa wawekezaji duniani kote wanaoendelea kuichagua Tanzania kama sehemu sahihi ya kuwekeza na kufanya biashara huku idadi ya miradi ya uwekezaji inayoingia na kusajiliwa nchini ikizidi kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 128.

Kwenye taarifa yake inasema, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) inaonyesha kwamba kwa mwezi Februari 2023 pekee, jumla ya miradi 41 kutoka nje ya Nchi imesajiliwa kote nchini ikiwa ni ongezeko la asilimia 128 ikilinganishwa na miradi 18 tu iliyosajiliwa kipindi kama hicho hicho mwaka uliopita 2022.

Kwa miradi pekee ya uwekezaji iliyosajiliwa mwezi Februari mwaka huu 2023 ina thamani ya Dola Milioni 339.2 (Bilioni 780) na inakwenda kutoa ajira 7,370 kwa Watanzania na inaonyesha ukuaji mkubwa wa mitaji kutoka Nje inayoingia kwenye uchumi wa Taifa kwa ongezeko la zaidi ya Dola Milioni 75.9 ikilinganishwa na kipindi hicho hicho mwaka jana 2022.
Screenshot 2023-03-27 at 16.28.18.png




Kwenye taarifa ya Jarida hilo, imenukuu taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini Gilead Teri ikisema mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Rais Samia na uamuzi wake wa kurahisisha sana upatikanaji na usajili wa leseni za biashara na matamanio yake makubwa ya kukuza uwekezaji nchini ndiyo yamewezesha kwa kiasi kikubwa sana uwekezaji huu mkubwa ambao haukuwahi kutokea kuja nchini.

Rais Samia imeirudisha Wizara ya Uwekezaji chini ya Ofisi yake ya Rais katika harakati za kuondoa changamoto za uwekezaji na kuharakisha masuala ya uwekezaji zaidi. Sasa thamani ya mitaji ya uwekezaji iliyoingia nchini imepanda kwa zaidi ya asilimia 413 kutoka Dola Milioni 66 Januari mpaka Dola za Milioni 339 kufikia Februari 2023
 
Back
Top Bottom