Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,507
- 8,136
Benki ya Dunia imeipa Serikali ya Tanzania trilioni 1.2 kwaajili ya tabia nchi, barabara na viwanja vya ndege.
Nadhani sasa ni muda wa kuondoa tozo au kuambiwa siku ya ukomo.
Kiuchumi mkopo unakwenda kusisimua mzunguko wa fedha hasa kama sehemu kubwa ya hizi tenda yatapewa makampuni ya hapa nchini, pesa zitatembelea mifuko ya wananchi na shughuli za uzalishaji zitaongezeka kupokea pesa za wananchi hawa. Hasara yake, tunaandika deni jipya katika madeni ya Serikali.
======
Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wa Sh1.2 trilioni utakaofungua milango ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya Mikoa.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Benki ya Dunia (IDA) leo Mei 27, imesema mkopo huo utaiwezesha Tanzania kufanikisha maeneo hayo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) utakaowezesha pia taasisi husika katika kupanga na kusimamia sekta hiyo.
Imesema ufadhili huo utasaidia uboreshaji na ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 500, zikiwemo za Mtwara-Mingoyo-Masasi (kilomita 201), Lusahunga-Rusumo (kilomita 92), Songea-Rutukila (kilomita 111) na Iringa-Msembe (kilomita 104), huku ikishughulikia hali ya hewa ili kuongeza ustahimilivu wa barabara.