Tanzania yapokea mkopo wa trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia. Kuboresha tabia nchi, usalama na barabara

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,488
7,938
Benki ya Dunia imeipa Serikali ya Tanzania trilioni 1.2 kwaajili ya tabia nchi, barabara na viwanja vya ndege.

Nadhani sasa ni muda wa kuondoa tozo au kuambiwa siku ya ukomo.

Kiuchumi mkopo unakwenda kusisimua mzunguko wa fedha hasa kama sehemu kubwa ya hizi tenda yatapewa makampuni ya hapa nchini, pesa zitatembelea mifuko ya wananchi na shughuli za uzalishaji zitaongezeka kupokea pesa za wananchi hawa. Hasara yake, tunaandika deni jipya katika madeni ya Serikali.
======

mkopo benki dunia.jpg

Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wa Sh1.2 trilioni utakaofungua milango ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya Mikoa.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Benki ya Dunia (IDA) leo Mei 27, imesema mkopo huo utaiwezesha Tanzania kufanikisha maeneo hayo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) utakaowezesha pia taasisi husika katika kupanga na kusimamia sekta hiyo.

Imesema ufadhili huo utasaidia uboreshaji na ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 500, zikiwemo za Mtwara-Mingoyo-Masasi (kilomita 201), Lusahunga-Rusumo (kilomita 92), Songea-Rutukila (kilomita 111) na Iringa-Msembe (kilomita 104), huku ikishughulikia hali ya hewa ili kuongeza ustahimilivu wa barabara.
 
Ahha na hizo tozo na ushuru walio ongeza kupita sawa n robi tatu sisi tume zivumilia. Maana ila wao wameona hazitoshi
 
Mabeberu bwana! watakuambia ni mkopo wa masharti nafuu lakini hayo "masharti nafuu" hayawekwi wazi!!

Tuambieni hayo masharti nafuu ni yapi? Tuambieni riba ni asilimia ngapi?

Tukimaliza kulipa tutakuwa tumelipa trilioni ngapi jumla? Je kuna mgao wa Zanzibar?

Kama upo ni shilingi ngapi? Je watalipa deni hao zenj au litabaki kuwa ni deni la T'nyika?
 
kwa jinsi tulivyoongeza WAGES BILL na Makusanyo yetu yalivyo kiduchu kulikua hakuna namna zaidi ya kukopa kugharamia miradi...

Huko mbeleni ktk mapato yetu ya ndani ukitoa
1. Wages bill
2. Matumizi ya kawaida
3. Marejesho ya mikopo sidhani km tutaweza kufanya mradi wowote kwa pesa zetu za ndani.
 
Benki ya Dunia imeipa Serikali ya Tanzania trilioni 1.2 kwaajili ya tabia nchi, barabara na viwanja vya ndege.

Nadhani sasa ni muda wa kuondoa tozo au kuambiwa siku ya ukomo.

======

Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wa Sh1.2 trilioni utakaofungua milango ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya Mikoa.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Benki ya Dunia (IDA) leo Mei 27, imesema mkopo huo utaiwezesha Tanzania kufanikisha maeneo hayo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) utakaowezesha pia taasisi husika katika kupanga na kusimamia sekta hiyo.

Imesema ufadhili huo utasaidia uboreshaji na ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 500, zikiwemo za Mtwara-Mingoyo-Masasi (kilomita 201), Lusahunga-Rusumo (kilomita 92), Songea-Rutukila (kilomita 111) na Iringa-Msembe (kilomita 104), huku ikishughulikia hali ya hewa ili kuongeza ustahimilivu wa barabara.

Utashangaa kiasi kitakachopelekwa Zanzibar.
 
Safi sana Mama Samia. Muangalie na mkoa wa Pwani.

Barabara ya Kisarawe inahitaji lami lakini pia barabara ya kuunganisha makao makuu ya mkoa - Kibaha na wilaya zake hakuna.

Ajabu Jakaya hakuliona hili licha ya kutoka mkoa husika.
 
Back
Top Bottom