Tanzania yadaiwa kujitoa kwenye Mahakama ya Afrika. Amnesty International na UN walaani hatua hiyo. Serikali yatoa ufafanuzi

kuna mzee alininong'oneza kwamba Kagame ndiye anaongoza Tanzania nikaleta ubishi .
 
Amnesty International: Uamuzi wa Tanzania katika Mahakama ya Afrika utazidisha ukandamizaji

  • Amnesty International: Uamuzi wa Tanzania katika Mahakama ya Afrika utazidisha ukandamizaji
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limesema uamuzi wa Tanzania kujitoa katika kifungu kinachowawezesha raia na mashirika yasiyo ya kiserikali kuishtaki serikali katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu yenye makao yake katika mji wa Arusha unahatarisha ongezeko la ukandamizaji nchini humo.
Amnesty imesema kujitoa huko kunawanyima watu na mashirika mbalimbali uwezo wa kupata haki zao za kisheria.
Msemaji wa Amnesty barani Afrika, Japhet Biegon amesema kitendo hicho kinayazuia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwenda moja kwa moja mahakamani kudai haki zao kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu, jambo ambalo ni jaribio la waziwazi la kukwepa wajibu na majukumu.
Taarifa ya shirika la Amnesty International imesema huu ni ushahidi wa ongezeko la uhasama wa serikali ya Tanzania dhidi ya haki za binadamu na watetezi wa haki hizo na uamuzi huo unadhoofisha mamlaka ya Mahakama ya Afrika, ni usaliti wa wazi kwa juhudi za bara la Afrika za kuanzisha mashirika madhubuti na ya kuaminika yanayoweza kudhamini haki na uadilifu.
Amnesty International imesisitiza kuwa Tanzania kama nchi mwenyeji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu inapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kutafakari tena uamuzi wake wa kujiondoa katika kifungu hicho. Vilevle imeitaka serikali ya Tanzania kuimarisha mfumo wake wa mahakama na kuhakikisha kwamba waathirika wa ukiukwaji wa haki za binadamu wanapata haki zao katika ngazi ya taifa.
4bskd810a4da5d1h25u_800C450.jpg

Rais John Magufuli wa Tanzania

Tanzania inakuwa nchi ya pili kujiondoa katika kifungu kinachowawezesha raia na mashirika yasiyo ya kiserikali kuishtaki serikali katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu baada ya Rwanda.
Katika barua yake kwa Umoja wa Afrika, ambao wanachama wake ndio waanzilishi wa mahakama hiyo, Tanzania ilielezea kuwa inajiondoa kwa kuwa mahakama hiyo imeshindwa kufanyia kazi maombi yake juu ya ruhusa ya watu na mashirika kushtaki serikali katika mahakama hiyo.
Takribani asilimia 40 ya kesi zilizofunguliwa katika mahakama hiyo ni dhidi ya Tanzania.
chanzo.https://parstoday.com/sw/news/africa-i57657-amnesty_international_uamuzi_wa_tanzania_katika_mahakama_ya_afrika_utazidisha_ukandamizaji
 
Natumai zipo hoja na sababu za msingi serikali yetu kuamua kujitoa mahakama Africa ya haki za binadamu.Walioshuhudia Bunge ama wizara husika watupe ufafanuzi. Tunajua vyombo vya sheria vipo kusaidia ku balance maisha dunia hii katika mazingira ya weak and strong.Vinginevyo sisi Watanzania tuhoji na kudai haki hiyo kama taifa huru lenye watu huru.
Screenshot_20191204-071015.jpeg
Screenshot_20191204-071008.jpeg
 
Haki ya kutaka kujua sidhani kama unayo,wewe endelea kuvumilia maumivu zaidi na zaidi.
 
Hili nalo limekua engineered na Paramaganda Jalalani?
Hakika huko mbele tutakuja kujua jinsi tulivyo bahatisha kupata waziri wa hovyo na mbaya kuliko walio pata kuwepo katika wizara alizopitia kwa karne nzima
 
Hili nalo limekua engineered na Paramaganda Jalalani?
Hakika huko mbele tutakuja kujua jinsi tulivyo bahatisha kupata waziri wa hovyo na mbaya kuliko walio pata kuwepo katika wizara alizopitia kwa karne nzima

Mama yangu alikuwa akichelewa kupika chakula cha jioni basi alikuwa na tabia ya kutupatia hadithi tamutamu ili tusilale na moja ya hadithi zake ilikuwa ni kwamba kinyonga akitaka kuzaa basi ni lazima apande mti hadi juu kabisa kileleni na kujiachia hadi chini anapasuka na kufa hapo hapo lakini kunakuwa na vijitoto viingi vya kinyonga mpya
 
Quinine,
zitto na Lissu wanaitesa sana serikali hii,zitto katafutiwa plan b hawampati wakimfuata wanageuka maji na wanawashwa wao,hvy njia ya kujihami ni kunguru muoga huepusha bawa lake,na bado watapatikana tu,jeuri ya mdomoni wakati mioyoni wanaumia na kuugulia
 
Tuanze kuisoma namba tuliwacheka Zaire, Libya na nchi nyingine sasa na sisi tunaingia huko. Hapa kazi tuuuuuuu!
 
Image gani? Fuatilia ujue uhalisia achana na wanamtandao uchwana wakina Erythrocyte katika Afrika ni nchi 9 tu ndiyo zilikuwa zimeridhia hiyo Mahakama. Halafu hao UN Human Rights waulize kwa nini Marekani siyo mwanachama kwenye hizo mahakama?
Tz siku zote imekua unique katika nchi zote za Africa lakini kama tumeanza kufuata nyao za Burundi hapo tumesha isha
 
Ukimtazama Kabudi utadhani ana akili vile, kumbe hawa waokotwa jalalani wanaweza kuusaidia udikteta kumea na kuangamiza mamilioni!!!
 
Erythocyte, haya matamko hayasaidii kwa madikiteita. matamko hayawatishi madikiteita, kinachowatisha ni mabomu na risasi kama Idd Amin, alikaa miaka 8 madarakani kwa vile matamko yalikuwa hayamtishi. Zilipoanza kumiminika risasi na mabomu masikio yakazibuka akaaza kupiga kelele za tupatanishwe, Nyerere akakataa (kama ulikuwa na akili za utu uzima enzi hizo... mimi nilikuwa nimemaliza form six nikiwa huko huko Kagera)
 
Wanakimbia kesi ya Muungano kule Arusha ,
Ali Adey na wazanzibari wenzake 40,000 wameishitaki Tanganyika kwa kuikalia Zanzibar kimabavu.
Hali si nzuri upande wao.

Ndio wametupa go ahead to UN Kufungua mashataka haya, naona Kama wanejinyonga, trust me
 
Back
Top Bottom