Sina hakika kama Tanzania ni nchi ya kijamaa vile lakini ninafikiri udhibiti wa unyonyaji wa makundi yenye nguvu kiuchumi dhidi ya makndi ya wafanya kazi na wachuuzi wadogo ndio tatizo letu. hatujamudu kuweka udhibiti maridhawa, ndio sababu kuna migogoro ya wawekezaji na wananchi. Ndio sababu wakulima na wafugaji hawaishi kugombana: Kumekosekana udhibiti madhubuti katika sekta za uzalishaji mali. Wawekezaji wanaoanekana ni wa maana kliko wananchi.
Wawekezaji wanaonekana wa maana lakini siyo wa maana Sana vile vile haswa ukichukulia Tanzania haina any competitive advantage kiuchumi kwenye sekta yeyote ile (labda madini kwa mbali sana), bila hii competitive advantage mwekezaji anakua hana uhakika wa mtaji wake achilia faida atakayopata-kama hujajua competitive advantage angalia gharama za uzalishaji, kodi,miundombinu mibovu, upatikanaji wa wafanyakazi wenye uzoefu na sekta husika, n.K, kwa haya Mimi Naona serikali ingebidi iweke mazingira mazuri zaidi kwa wawekezaji haswa wale wa ndani kwa zaidi hata ya inavyofanya sasa ambapo mazingira bado hayakidhi haja ya mwekezaji kuwekeza zaidi ya kwenye sekta ya madini peke yake.