Tanzania ya 'Rais Lowassa' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ya 'Rais Lowassa'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Oct 10, 2011.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu naomba tutafakari kidogo na hii hadithi ya EL kuendelea kuwepo katika midomo na mawazo ya watu katika kuwania urais 2015, hii ikiwa pamoja na kashfa zote na hii sera ya kujivua gamba kuonekana inamuogopa. Sasa basi kama hamna lolote litakalotokea na akiweka watu wake NEC 2012 basi njia ni yake na ukichukulia kwamba Mwinyi na Mkapa wote walishindwa kumuachia kiti mtu wao, basi na JK hatoweza, EL anakua rais 2015, japokua wanasema a week in a political life is a long time, lakini Tanzania yetu hatujafika hapo siasa za kinafiki zisizokomaa bado zinatawala kwa hiyo 2015 ni kesho tu. Sasa serikali, ccm, tanzania ya EL itakuaje? tusafiri kidogo hadi mida hiyo tujionee as time travel is always a human fascination.

  Kwanza huyu jamaa ameutaka urais toka 1995 na 2015 itakua ni miaka 20 kamili lazima ataunda serikali ya Ki-Lowassa Lowassa yaani itakua na marafiki, wapambe, na loyalists bila kujali ari, uwezo, upeo wa uongozi na uzalendo wao kwa taifa hili. Kumbuka hii itakua ni kama sherehe lazima walioumia nae miaka yote hii wazawadiwe. Tumeliona hili kwenye serikali hii ya Kikwete na jinsi linavyotuumiza kwa sasa kwa kua a mawaziri na viongozi wanaolindana na wasiokua na uzalendo, uwezo na wala tija ya kazi. Hapa majina kama Mahanga,Karamagi, Chenge, Nchimbi, Malima, Sofia Simba, Masha, Kapuya etc yatarudi tena katika uongozi, wote wana matatizo katika uongozi

  EL anaamini ana maadui wengi waliomletea matatizo katika njia yake takatifu ya kupata urais na jinsi alivyo hawa lazima wawajibishwe, hizi ni siasa za visasi. Tofauti na Mkapa aliyeunda serikali ya umoja katika CCM na Kikwete alielipiza kisasi kwa kiwango kidogo kutokana na character yake na imani yake, EL anaona ameonewa na kunyanyaswa siyo kisiasa tu bali hata utu wake na hii ni very personal kwake kwa kua anaamini yeye ndiye aliyekua anafaa muda wote kua rais ila aliwekewa fitna. Hii kwanza ni tabia ya kujiona wewe uko sawa kila wakati na unaonewa tu hata ukifanya makosa ni tabia isiyo faa katika uongozi wowote hata wa familia. Hii ndugu zangu itaathiri utendaji wa serikali yake kwa kua nguvu za ziada zitaelekezwa kwenye hili na siyo kusaidiana kujenga Taifa kwa kushirikiana na kusikiliza mawazo ya wote.

  Kwa kiongozi aliyejiuzulu na skendo iliyomuhusu yeye mwenyewe ni vigumu baadae kuchukulia hatua au kuziba mianya ya wizi na ubadhirifu serikalini na ukichukulia yeye na watu wake wa karibu ni wafanya biashara kwenye nchi isiyo na uongozi madhubuti wa kisheria basi hatutakua na budi kuangalia maozo ya serikali zote zilizopita siyo tu yakiendelea bali yakiongozeka pia katika muda wake wa utawala.

  Nyerere hakumtaka Lowassa na Malecela kwa sababu mbili tofauti, Lowassa kwa ugeni wake katika ngazi za juu za maamuzi ya nchi na chama na fedha zake za haraka haraka alizozipata kwa kipindi kifupi. Na kwa upande wa Malecela kwa sababu ya Kutaka kuhodhi madaraka yote ya Kichama na serikali. Network ya Malecela ilikua tishio kwenye CCM ambapo Nyerere hakutaka mtu mmoja kuwa na nguvu kuliko chama so akawaengua wote.Fast forward 2011 EL siyo tu kwamba ameongeza hela pia ana nguvu kwenye chama ambayo hakuwa nayo 1995 na hii ni shida kwa demokrasia yetu changa kichama na kitaifa.

  Hii ina ubaya na uzuri wake. Ubaya ni kwamba hamna mtu atamkosoa kwenye chama, serikali, na atatumia nguvu hizi za umoja huu kudidimiza uhuru wa habari, upinzani na demokrasia nchini. uzuri unaweza kua ataweza kuharakisha mambo yafanyike haraka zaidi kwenye ngazi zote kichama na serikali, lakini je kama ataunda timu dhaifu haya mazuri hatutayaona kwa sababu serikali siyo mtu mmoja/rais serikali ni timu. Kama Nyerere's one man show ilishindwa EL hatoweza.

  Tofauti na wenzake Rais EL atataka kiti cha urais kiwe karibu nae hata wakati akiwa amestaafu. Hapa tutaona atakavyojipa nguvu aogopewe kichama na kiserikali ili apate nafasi ya kumchagua mrithi wake 2025. Kama tulivyosema hapo juu atajipa nguvu kwa kuengua maadui, kujaza nafasi zote kwa watiifu wake, kubana vyombo vya habari au kutumia marafiki kuvinunua kama wanavyofanya sasa hivi, na kumaliza nguvu za wapinzani kwa kupachika watu wake ndani ya upinzani na kutumia nguvu za dola ambazo inaaminika ana uhusiano nao vizuri. siasa za urithishaji viti zitakua zimeanza rasmi Tanzania.

  EL ana kiburi kisichofaa katika siasa za nyakati hizi za uwazi, ushirikiano na demokrasia zaidi. Kwani Katika skendo yake alijishirikisha mwenyewe sana bila kujali matatizo yanayoweza kumkuta na baada ya hapo hakupanga kuongelea hili kiundani na Rais, Spika wala kamati ya Bunge kumnusuru alikaa kimya kijeuri akiamini ataogopwa hatoguswa kinyume chake kamati ikafanya kazi ikabidi awajibike kwa shingo upande na kuanza kutafuta wachawi kila kona kusababisha nyufa wenye chama na serikali ambazo zimeathiri wananchi kwa kiasi kikubwa.

  Je ujeuri huu, ubinafsi huu, umungu mtu huu unatusaidia vipi katika matatizo yetu Watanzania? Nafikiri haitusaidii kua na kiongozi wa aina hii haswa katika muda huu ambao tunataka uongozi unaoweka maslahi ya taifa kwanza.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  EL for ccm 2015
   
 3. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Maelezo Mengi Point hakuna kabisa. Kila Mtanzania Ana Haki ya kugombea urahisi kikatiba na unapogombea sio lazima ushinde ina maana kura ndizo zitaamua. Mambo ya 2015 kuyazungumzia sasa hivi ni kama mtu anaota ndoto maana hata hatujui ni nani atafanikiwa kuuona mwaka 2015.
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Arusha huyu Lowasa ana majumba kila kona, London kila kona Dar sijui Tanzania kaifilisi kwa miradi yake ya DOWANS, ebu fikiri kidogo akipewa Urais si nchi itabaki jangwa?
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  aisee Lowassa ni king'ang'anizi yaani bado anautaka urais tu, pamoja na shuruba zote zile za dowansi na richimondi? aisee.....
   
 6. J

  JajiMkuu Member

  #6
  Oct 10, 2011
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani let us be fair, hii miaka minne ambayo EL amekaa nje ya "madaraka", imemwondolea EL kwa kiasi kikubwa uwezo wa kutusaidia wanamtandao wenzake. Hivyo ni halali kabisa kwa EL kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015 ili kuwezesha, baada ya ukame mkubwa, kutwaa angalau mgodi moja au miwili ya uranium, mradi mmoja au miwili ya Kilimo Kwanza na hata hisa za kutoshakwenye kampuni hilo linalokuja la kuagiza mafuta toka nje kwa pamoja kwa faida yetu wanamtandao. Hoja ya kwamba nchi ataiacha jangwa inatoka wapi kama si fitina tu za akina Sitta, Nape, Sendeka, Mwakyembe, Lembeli na Kilango?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa uranium ameshachelewa. Kikwete kishawapa maswahiba wake Marekani. Labda tugundue madini mengine hapo baadaye.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  aiseeee[SUP].........[/SUP]
   
 9. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No need to read your writing. Lowasa hawezi kuwa rais wa Tanzania. Hata akaombe Nigeria mara mia.
   
 10. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Lowasa ni fisadi kweli anataka kuwa rais, sawa, je ndiye atakayepiga kuraa????
   
 11. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa nini CCM mnamuota EL kwa urais 2015? Hamna wengine?
  Nyerere alimwambia hivi - una utajiri kuliko umri wako; hiyo ni 1995
  Kashfa ya Richmond na Dowans -Tutapoteza over 100bn/- kwa ufisadi wake
  Mtu wa visasi nk.
  Lakini naona bora ccm wampandishe chati ili waweze kumeguka. Makongoro Nyerere wa Mara ameshasema kuwa wale wote waliotajwa kwenye NEC kuwa ni mafisadi lazima waondoke; na tayari anaandaa hoja hiyo na ile ya kutaka mwenyekiti asiwe rais. CCM ikimg'ang'ania EL, Makongoro atameguka na kundi lake.
  Halafu kuna hili sakata la ugonjwa wa Mwandosya na sasa Mwakyembe. Ikidhirika kuna suala la sumu, kanda ya juu kusini lazima kuna pande litameguka. Kitakachokuwa kimebaki ni vipande vipande tu vya CCM.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,625
  Likes Received: 2,003
  Trophy Points: 280
  Ni mmasai,haendi mahali labda wamwue.Ndo ukweli huo.EL is definetly going to come back come 2015.Watakanyagana sana kwenye proccess hatahivyo.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Lowassa will never be president. He shouldn't expect a political come back. Kinacho muangusha Lowassa ni kwamba majority ya wananchi hawamtaki huyu mtu. Hawakumtaka kama waziri mkuu na hawata mtaka kama raisi. 2015 CCM itatumia kigezo cha kuto kukubalika kwake kumuangusha.
  Anyway siasa mchezo wa ajabu sana huwezi jua kitakacho tokea.
   
 14. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  afadhali apewe EL nchi ibaki jangwa , atauza hadi Nyegere wa Singida
   
 15. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Wastage of time kama tukijadili hii thread kwa vile Lowasa hawezi kuwa rais na CCM kwa ujumla.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi tatizo letu Watanzania ni Lwassa kuwa rais au kutokuwa?
   
 17. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Think biggest,open your mindset.Eti Lowasa rais 2015 mada yako jaribu kuiweka sawa mazee
   
 18. K

  Kiminyio Member

  #18
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyeianzisha mada ana ajenda ya siri. atupe hiyo siri ni kwa nini anamuhofia EL atakuwa raisi. kuna mambo mengi ya muhimu ya kujadili ndani ya kipindi hiki ambayo yanaweza kuwaamsha viongozi wetu waliolala na kuwa tija kwa maendeleo ya nchi yetu tofauti na kuzungumzia utopian ideas. Tusubiri hadi kipindi kitakapokaribia, na watakaochukua fomu tuanze kuwajadili na kuwapigia kura za kutokuwa na imani ama kuwa na imani nao muda huo. Ila kwa ufupi sana kama akichukua fomu ya uraisi, na akapitishwa na chama chake, na wananchi wakampa kura, basi huyo ndiyo raisi wa Tanzania ajae.
   
 19. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kama CCM itampitisha Lowasa awe mgombea wa urais 2015 basi usindi wa CDM ni mlaini sana
   
 20. Ng'wanambula

  Ng'wanambula Senior Member

  #20
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na muanzisha mada hapo juu.Lakini cha ajabu humu jf baadhi ya watu inaonekana hawana uchungu na nchi hii,kazi yao kufikiria maslahi yao na familia zao.Huyo jamaa sijui lakini inavyoelekea ana probability kubwa ya kushinda kwenye chama.inasemekana kwenye NEC ya CCM 65% ya wajumbe ni loyal kwake na ma-DC na RCs zaidi ya 75% ni waaminifu sana kwake.Hivyo amejipanga na tusipokuwa makini atachukua nchi hii na ndipo kilio na kusaga meno kwa watanzania kutakapokuja
   
Loading...