Tanzania ya 'Rais Lowassa'

baada ya huyu jamaa kuondoka kuna nini kipya kimefanyika zaidi ya zile shule za kata nini tena kipya
kimefanyika jamaa ni kichwa hata kama ni mwizi lakini ni mchapa kazi acheki na kima wala wazembe
 
Kama vipi gombea wewe urais ni haki ya kila raia na kuchagua mtu unayemtaka ni haki ya kila raia je akitaka kugombea kuna mtu atakayemkataza? Jamani tusubiri muda ufike ukweli itajulikana tu na wananchi ndo waamuzi wa mwisho kusuka au kunyoa
 
Hivi hizo hela alizonazo Lowassa zimewekwa kwenye akaunti ya Benki Gani ili tuibane serikali yetu ikazichukue.

Naona umeibeba hoja yako tasa na kuibukia huku. Msalaba uliotwishwa mzito na ni vizuri ukawaambia wenyewe kwamba hauuziki.
 
Pengine nakosea mie ntaomba mnirekebishe; Huya jamaa tuhuma kubwa aliyonayo ni ya RICHMOND,DOWANS...SYMBION(Hii yote kitu kimoja) ukiangalia hili sakata linavyokwenda inaonekana automatically linamsafisha.

Kuna story za ,mali nyingi ambazo hazitajwi...ila kinachoonekana wazi huyu jamaa kwa mipango na ushawishi hatari manake kupitia yeye na RA ndio JK aliweza kuingia madarakani.Na alifanya hivyo akijua anajitengenezea yeye njia laini ya kuja kuingia ikulu ndio maana utaona wakata JK anawapa vyeo wajomba na mashemeji na nyumba ndogo zake yeye akapanga safu UWT,MA DC,NA MA RC...tena hapa nampongeza kwani yeye aliweka watu makini.

Swala la uchapa kazi kwa huyu jamaa anayelipinga apinge liko wazi kabisaaaaaaaa...hana mchezo anayo mapungufu ya kawaida kama binadamu wengine walivyo km vile kutumia nguvu nyingi ambalo halimnyimi kuwa kiongozi mzuri.

Kitakachofuata baada ya DOWANS sijui kashfa gani tena mtaleta ambayo ni mpya haikutajwa kipindi hiki.Swala la mtandao ambao ndio ulimwingiza JK madarakani yeye ndio mastermind,sa sijui mnategemea nini hapo. Sasa uchafu wake na wizi wa kuwazidi wenzie uko wapi si muutaje? Au kosa kuwa tajiri?Pia na huo utajiri utajwe ulinganishwe na kipindi cha utumishi wake na biashara anazomiliki tangu aanze biashara.......nina wasi wasi kama kuna mtu anazo data za kuoongelea vibaya utajiri wako zaidi ya maneno matupu. Si wakati wote tukubaliane na Nyerere kwani pamoja na kwamba jamaa alikuwa kichwa lakini kwa fitina na kugawa watu pia alikuwemo sana...kama vile alivyosema wachaga hawafai kupewa nchi??? Sababu hakuzitoa.

Ni dhahiri ndani ya CCM EL atachukua tiketi ..... swala ni kwamba yeye kuwa Rais itategemea na upinzani utakavyokuwa au watatumia mchezo ule ule uliomwingiza JK awamu ya pili(kwa wafuatiliaji wa mambo mnaujua)

Hivyo kwa maoni yangu na jinsi mambo yalivyo huyu jamaa atatimiza hizo ndoto zake....... kwani wakati wengine wanapiga kelele yeye yuko kwenye mipango.... pia ni rahisi kama sio wazi atapata back up kubwa sana kutoka kwa JK ili amfichie maswala yake.
 
Mimi ningependa kuwaonya watanzania wenzangu hata hao wana ccm wakimpitisha sisi watanzania tumkatae hatufai kutuongoza.

Kura ni tendo lakidemokrasia na ni matakwa ya mtu binafsi,usitufundishe kumchagua au kutomchagua El,hili lipo mikoni mwa mwananchi,
Ben aliandamwa na kashfa kibao ikiwemo kiwira na isue ya Rada lakini nani kama Ben katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini?Licha ya kashfa zote lakini jamaa ndie pekee ambae aliweza kuinua uchumi wa tanzania licha ya mapungufu fulanifulani ambayo yalijitokeza.Ni nani anaweza kubisha juu ya ukweli kwamba EL licha ya kashfa alizonazo jamaa ni mchapa kazi na mzuri ktk swala zima la uwajibikaji na ungozi?
 
Huyu jamaa mnamuonea bure.uPM wenyewe kafanya mda mfupi tu.hata kama aliiba kipindi akiwa waziri wa maji mbona hakuna skendo.
Hii ya richmond si ilifail.KAMA HUYU JAMAA NI TAJIRI KIIVO WHERE DID HE GET MONEY?
Binafsi naamini si tajiri kiivo ni UZUSHI TU.
 
Nafikiri tunajua kwamba pamoja na kwamba umaarufu wa CCM unaendelea kupungua kwa kasi kubwa, bado chama hiki kikongwe tawala kinaweza kufanya vizuri kushinda katika uchaguzi ujao, hii inatokana na ushawishi wa CCM vijijini ambako wapinzani wamekua wanapata shida kufikisha ujumbe wao vizuri na nguvu ya dola ilihodhiwa na CCM kama chama tawala.

Sasa inabidi kuwaangalia kwa karibu wagombea wote wa CCM kwa umakini tukianza na kinara wa mbio hizi Mheshimiwa waziri mkuu wa zamani Edward N. Lowassa.
Wanaomsapoti Lowassa wanakubali ana mapungufu ya kimaadili lakini wanasema ni mchapa kazi na ana maamuzi na nchi inataka mtu mwenye maamuzi. Wanaosema hafai wanasema hana maadili ya uongozi kutokana na kashfa za kimaadili ya uongozi wa umma na nchi inataka mtu mwenye maadili. Mimi binafsi nafikiri yote ni muhimu yaani mchapa kazi na mwenye maadili na huyu ni mtu mgumu kumpata kusema ukweli na sasa naona imefika hatua ya kumshauri huyu front runner namna ya kulainisha wasiomsapoti au hawa wanamaadili kwa yeye kufanya na pia kuahidi kufanya yafuatayo;

1. Kutuambiia ukweli wa Richmond na Kuomba radhi kwa Watz wote, kumbuka hii ilifanywa na Mathieu Kerekou wa Benin na ilimsafisha vilivyo kiongozi anayekiri na kusema ukweli ni kiongozi wa kweli kuliko anayetaka kuficha na kusafishwa kwa njia zozote zile. vile vile hii itajenga imani kwa wananchi na kumuonea huruma mkubwa wetu huyu

2.Mheshimiwa wetu huyu inabidi aanze kuchukua midahalo muhimu ya kitaifa kama katiba mpya na kuahidi kwamba akifika magogoni atazifanyia kazi katika kipindi xx cha utawala wake bila kujali vigogo wengine wa CCM wana fikiria nini

3. Aseme ataweka serikali itakayoundwa na watu wenye uwezo wa kazi kutoka vyama vyote na makundi yote bila kujali uhusiano na wahusika.

4. Atangaze mali zake na aseme amezipataje ili aondoe mawingu juu ya mali zake binafsi. Hii vile vile itasiaidia kuondoa kile alichosema Mwalimu 1995 na vile vile itamuweka kuonekana atapambana na wasiokua na maadili ndani ya serikali yake

5. Aache kutafuta wachawi katika siasa za chama na aanze kujihusisha zaidi na matatizo ya jamii. Kama raia anayeipenda nchi hii atoe misaada kwa vikundi vyote vya kijamii na atembelee maeneo mengine ya nchi.

kuna mengine nafikiri anaweza kuyafanya ili kulainisha image yake ya kua power angry, arrogant, fisadi, wrong sense of entitlement, etc pragmatic politics pekee ndiyo zitamkomboa mbele ya doubters wake.
 
The answer is nooo! Hii ni mentality ya watu waliokwisha kata tamaa. Watanzania hatujakata tamaa. Nani kakuambia kuwa CCM ni maarufu vijijini? Ikiwa ni hivyo CCM ingepata 80% Igunga. Hakuna mahali palipo nyuma kimaendeleo kama Igunga. Tanzania tunahitaji uongozi utakaotuondoa kwenye hili limbwi la ufisadi na ufukara ambao Lowassa ni kinara wake. The answer is noooo!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kuna watanzania kibao ambao hawajawi kushutumiwa na wana uwezo mzuri wa kuongoza,tukimpa lowassa tunarudia makosa,,aende kwa joshua mnijeria ampe huo urais
 
lowasa, Lowasa, Lowasa, Lowasa, lowasa.... Ivi mnalipwa... CRAP
 
The answer is nooo! Hii ni mentality ya watu waliokwisha kata tamaa. Watanzania hatujakata tamaa. Nani kakuambia kuwa CCM ni maarufu vijijini? Ikiwa ni hivyo CCM ingepata 80% Igunga. Hakuna mahali palipo nyuma kimaendeleo kama Igunga. Tanzania tunahitaji uongozi utakaotuondoa kwenye hili limbwi la ufisadi na ufukara ambao Lowassa ni kinara wake. The answer is noooo!

Kule Magamba simuoni yoyote yule anayestahili kupewa nchi. Si Magufuli, Hussein Mwinyi, Membe, Lowassa, Migiro wala Tibaijuka. Sijui labda siku za usoni atatokea mmoja ndani ya magamba ambaye anastahili kupewa nafasi hiyo lakini kwa sasa simuoni yoyote ndani ya magamba.
 
Mkuu umenikumbusha habari za Mathieu Kerekou. Alishindwa na wapinzani kwenye uchaguzi wa vyama vingi wapinzani wakatawala kipindi kimoja kisha mzee akashinda uchaguzi uliofuata!! Huenda hii ndiyo unasema ilifuatia kuomba kwake msamaha.

Twende mbele turudi nyuma Lowassa ni mtendaji na akipewa nchi tutaona mabadiliko makubwa. Huyu ni miongoni mwa wale watu ambao wakisema mlima huu uondoke basi unaondoka. Nakumbuka machache tu aliyofanya wakati wa u PM wake:
  1. Kuna siku alimwamuru injinia wa DAWASCO kuingia kwenye bomba na suit yake. Kulitokea kukatika kwa maji Dar kutokana na kuharibika kwa bomba kubwa huko bunju basi PM akaenda kuangalia maendeleo ya matengenezo ati na injinia wa DAWASCO akaja na suit badala ya overall, PM akamuamuru azame. Ilichukua muda mfupi maji kurejea ktk hali ya kawaida. Uthubutu
  2. Kulikuwa na usuasuaji wa ukarabati wa barabara ya Shekilango. PM akaingia Makamba (RC) akatetemeka muds si muda barabara ikawa tayari. Uthubutu
  3. Kukawa na giza akaingilia kati kuhusu kununua mitambo. TANESCO na wizara wakakosea PM akajiuzulu! Uthubutu
  4. Wakati akiwa waziri wa maji Misri walikuwa wakikatalia maji ya Nile ati sisi hatuwezi kutumia maji ya ziwa victoria. Mzee akasema hakuna mkataba wa mwaka 1910 hapa maji ni yetu akayapeleka shinyanga na Kahama!! Uthubutu
  5. Nchi haikuwa na vyumba vya madarasa. Wakakubaliana kwamba kila kata na iwe na sekondari. EL akasimamia. Watu wakalazimishwa kuchanga na wengine wakachanga wa hiari yao. Wakuu wa mikoa na wilaya wakatetema. Kila kata ikapata sekondari. Uthubutu
  6. etc
 
kuna watanzania kibao ambao hawajawi kushutumiwa na wana uwezo mzuri wa kuongoza,tukimpa lowassa tunarudia makosa,,aende kwa joshua mnijeria ampe huo urais
ujinga ni kufanya jambo lile lile halafu utegemee matokeo tofauti.
 
Mkuu umenikumbusha habari za Mathieu Kerekou. Alishindwa na wapinzani kwenye uchaguzi wa vyama vingi wapinzani wakatawala kipindi kimoja kisha mzee akashinda uchaguzi uliofuata!! Huenda hii ndiyo unasema ilifuatia kuomba kwake msamaha.

Twende mbele turudi nyuma Lowassa ni mtendaji na akipewa nchi tutaona mabadiliko makubwa. Huyu ni miongoni mwa wale watu ambao wakisema mlima huu uondoke basi unaondoka. Nakumbuka machache tu aliyofanya wakati wa u PM wake:
  1. Kuna siku alimwamuru injinia wa DAWASCO kuingia kwenye bomba na suit yake. Kulitokea kukatika kwa maji Dar kutokana na kuharibika kwa bomba kubwa huko bunju basi PM akaenda kuangalia maendeleo ya matengenezo ati na injinia wa DAWASCO akaja na suit badala ya overall, PM akamuamuru azame. Ilichukua muda mfupi maji kurejea ktk hali ya kawaida. Uthubutu
  2. Kulikuwa na usuasuaji wa ukarabati wa barabara ya Shekilango. PM akaingia Makamba (RC) akatetemeka muds si muda barabara ikawa tayari. Uthubutu
  3. Kukawa na giza akaingilia kati kuhusu kununua mitambo. TANESCO na wizara wakakosea PM akajiuzulu! Uthubutu
  4. Wakati akiwa waziri wa maji Misri walikuwa wakikatalia maji ya Nile ati sisi hatuwezi kutumia maji ya ziwa victoria. Mzee akasema hakuna mkataba wa mwaka 1910 hapa maji ni yetu akayapeleka shinyanga na Kahama!! Uthubutu
  5. Nchi haikuwa na vyumba vya madarasa. Wakakubaliana kwamba kila kata na iwe na sekondari. EL akasimamia. Watu wakalazimishwa kuchanga na wengine wakachanga wa hiari yao. Wakuu wa mikoa na wilaya wakatetema. Kila kata ikapata sekondari. Uthubutu
  6. etc
kama ni ishu ya uthubutu basi magufuli anatufaa zaidi
 
Ndugu director 1,kwa hiyo hizo sifa 6 ulizozitoa unaona anafaa kua Rais?Shame on you.Nyie wote ni wa KUNYONGWA tu na huyo EL wenu,nyie ngojeni tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom