SoC01 Tanzania ya Maendeleo

Stories of Change - 2021 Competition

Haymayn Anzuan

New Member
Sep 8, 2021
1
1
Tanzania ni nchi huru ambayo inaongozwa kwa utawala wa Sheria kwa kuzingatia demokrasia ,ambapo viongozi hupatikana kwa kuchaguliwa na wananchi kila baada ya miaka mitano,akiwemo raisi,wabunge,na madiwani.

Nchi ya Tanzania inapita katika Sera mbalimbali katika kila awamu ya uongozi ,lengo tu kusonga mbele kimaendeleo katika nyanja zote ikiwemo uchumi,biashara ,afya,Sayansi na teknolojia,utawala bora, haki za binaadamu,na maendeleo ya jamii.Miongoni mwa Sera hizo ni uchumi huria ,hapa kazi tu,kazi iendelee,ari mpya nguvu mpya Kasi mpya .

Katika kuleta maendeleo nchini Tanzania wamegawa sekta mbalimbali miongoni mwa sekta hizo ni hizi zifuatavyo-

Uchumi ,ni jumla ya shughuli zote za binaadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao,katika uzalishaji,usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma .Uwekezaji katika sekta mbalimbali umesaidia kukuza uchumi kwa kiasi,lakini hali si shwari mtaani kwani asilimia kubwa wanaishi katika mazingira magumu ndani ya giza la umasikini .Kwa mintarafu hiyo serikali iangalie kwa kina hali na maslahi ya wananchi wao hususani tabaka la chini ikiwemo suala la ajira,pia utumiaji nzuri wa rasilimali ikiwemo madini ili Kodi zisizo za lazima ziweze kuepukika, ili walalahoi hao waweze kukidhi mahitaji yao na kuongeza uzalishaji katika vipato vyao.

Afya, afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili ,kiakili bila kusumbuliwa chochote .Uongozi wa nchi yetu kwa kiasi kikubwa unajitahidi kuboresha afya za watanzania , kwa kulitambua hilo wameongeza idadi ya hospitali kubwa kwa kila wilaya na Sasa kila kata kujengwa hospitali kubwa zitazowezesha hadi operesheni.Hili ni jambo kubwa lakini kujenga tu hospitali hakujaleta ufanisi wa huduma kwani vituo vimeongezeka lakini huduma ni finyu husasani vijijini wazee wanateseka huduma bure lakini inashangaza unapata maandishi bila dawa ,hivyo basi Kuna haja ya kukagua mahospitalini kwa nini dawa zinakosekana lakini ajabu nje tu ya hospitali utakuta duka na dawa zote unapata hapo kwa kununua ,pia viongozi husika wafanye ziara mara kwa Mara mahospitalini ili Kuona hali halisi ,mbali na ziara ifanyike mikutano Kati ya viongozi na raia kwa kila eneo ili kujua kero zinazowakabili.

Kilimo, Sayansi na Teknolojia ,ni wazi kuwa jitihada mbalimbali zimefanywa katika kuleta mapinduzi ya kilimo na Sayansi na teknolojia ,ikiwemo kuboresha viwanda ,matumizi ya mitandao katika shughuli mbalimbali.Kwa upande wa teknolojia hatua imesogea lakini kwa upande wa kilimo bado mbinu na wataalamu wanahitajika Kama vile kuwezeshwa wakulima kwa pembejeo za kilimo ,kutoa elimu hususani ukanda wa Pwani bado asilimia kubwa wanatumia kilimo cha mikono,vile vile Kuna haja ya kuongezwa masoko na kuwekwe uhakika wa bei za mazao ,itapendeza kila wilaya kuwe na soko maalumu la kuuzia mazao ,ambapo watu kutoka nje na serikali wawe wananunua hapo bidhaa kutoka kwa wakulima.

Maendeleo ya jamii,utawala Bora na uwajibikaji,katika kuleta maendeleo lazima kupatikane utawala bora na uwajibikaji ,hivyo basi viongozi wanatakiwa wawajibike hasa wabunge majimboni mwao kwa kuongea na raia wao katika kila vijiji na vitongoji kujua changamoto na kuzitatua.

Demokrasia, ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya Sheria na wanshiriki kufanya maamuzi juu ya masuala ya umma.Ili kujenga maendeleo ya kweli kuwe na uhuru wa vyombo vya habari ,uhuru wa kufanya mikutano na makongamano kwa vyama pinzani sawa na vyama tawala kwa utaratibu wa Sheria ,pia Sheria kuhusu masuala ya Kodi na tozo za ziada kabla hazijapitishwa kila mbunge arudi jimboni mwake kupokea maoni ya raia wake ili kuondoa lawama kwa raia .

Kwa ujumla ili kuleta maendeleo hatuna budi serikali ishirikishe raia katika masuala mbalimbali,mbali na hayo viongozi pia wapite kila mitaa kujua kero za raia na kuzitafutia ufumbuzi ,vilevile Kuna tafiti nyingi za wasomi mbalimbali wa vyuo vikuu katika fani mbalimbali,hivyo basi ipo haja ya tafiti hizo kutolewa maktabani na kupitiwa kwa kina kwani zitasaidia kuleta maendeleo na mapinduzi makubwa nchini hususani katika kilimo , biashara , demokrasia ,uchumi na hata utawala pia.
 
Back
Top Bottom