Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 1,842
- 1,700
Mkuu ni kweli walizuia mahindi na mambo mengine hapo nyuma na siwatetei ila naweka preamble facts hapa.Mbona hao hao wakenya wamekuwa wakizuia na kuweka vikwazo kwa mahindi yetu kuingia kwao?
Mkuu tuuwe wa kweli kabla hatujaanza kuwanyooshea kidole, tujitizame sisi kwanza na tuseme ukweli; Tuliwafanyia mangapi kabla ya wao kufikia kuchukua hatua hiyo.
Hivi unajua hata hizi nchi jirani mathalan Malawi, Zambia Congo, Burundi, Rwanda na Uganda tunazifanyia vituko sana ila haziwezi kureteriate equally kama Kenya kwa sababu hawana Bandari, ni dependant kwa Tanzania, kwa hiyo inawalazimu kuwa wa pole.
Kenya ana guts na muscles kwa sababu sio tegemezi kwa Tanzania.
Kwa taarifa yako Kenya ndio power house wa Jumuiya ya Afrika mashariki, ni second world country with the most skilled labour na ndio nchi ya pili kwa uwekezaji nchini wetu!
Reactions zake zina repercussions kubwa kwetu hata kama tutashupaza shingo! Na kumalizia kufungua mpaka ni utaratibu rasmi wa kuwezesha urahisi wa watu kufanya shughuli za uzalishaji na biashara bila vikwazo!
Mkuu ondoa mashaka, mbona Zanzibar tuliungana nao tukafungua mipaka na hakuna madharra yoyote yaliyo wahi kutufika?
Tuwe objective na optimistic kwenye mambo yenye manufaa mapana kwetu!