Tanzania tusije kubali haraka wazo la kuondoa mipaka yetu ya nchi kama wanavyotaka baadhi ya MaRais wa Afrika Mashariki

Mbona hao hao wakenya wamekuwa wakizuia na kuweka vikwazo kwa mahindi yetu kuingia kwao?
Mkuu ni kweli walizuia mahindi na mambo mengine hapo nyuma na siwatetei ila naweka preamble facts hapa.

Mkuu tuuwe wa kweli kabla hatujaanza kuwanyooshea kidole, tujitizame sisi kwanza na tuseme ukweli; Tuliwafanyia mangapi kabla ya wao kufikia kuchukua hatua hiyo.

Hivi unajua hata hizi nchi jirani mathalan Malawi, Zambia Congo, Burundi, Rwanda na Uganda tunazifanyia vituko sana ila haziwezi kureteriate equally kama Kenya kwa sababu hawana Bandari, ni dependant kwa Tanzania, kwa hiyo inawalazimu kuwa wa pole.

Kenya ana guts na muscles kwa sababu sio tegemezi kwa Tanzania.
Kwa taarifa yako Kenya ndio power house wa Jumuiya ya Afrika mashariki, ni second world country with the most skilled labour na ndio nchi ya pili kwa uwekezaji nchini wetu!

Reactions zake zina repercussions kubwa kwetu hata kama tutashupaza shingo! Na kumalizia kufungua mpaka ni utaratibu rasmi wa kuwezesha urahisi wa watu kufanya shughuli za uzalishaji na biashara bila vikwazo!

Mkuu ondoa mashaka, mbona Zanzibar tuliungana nao tukafungua mipaka na hakuna madharra yoyote yaliyo wahi kutufika?

Tuwe objective na optimistic kwenye mambo yenye manufaa mapana kwetu!
 
... ifike mahala viongozi wa nchi zetu wakawa na heshima na raia wa nchi zao! ... maamuzi makubwa, na yenye athari za kudumu, kama hili la kuondoa mipaka, lisiwe jambo la kuamuliwa kisiasa na viongozi na wawakilishi wetu bali libaki kama suala la kupigiwa kura na wananchi wa nchi husika!
NB: (1) SUALA LA MIPAKA NI SUALA LA 'LAND MANAGEMENT ISSUES' ... KILA NCHI MWANACHAMA ITATUE MASUALA YAKE YA ARDHI YENYEWE!
(2) Kama watanzania hatujajifunza kutokana na 'KERO ZA MUUNGANO' basi tutakuwa 'PUNDA WA DOBI' ... yaani hatuna mioyo wala masikio!

WASITULETEE! 👁️👁️👁️👀
Mkuu usichanganye mambo kinacho zungumzwa ni kufungua mipaka, sio kuondoa mipaka.

Jumuiya Afrika mashariki imefinance na kufacilitate uwekaji wa alama za mipaka kwenye mipaka yote ya nchi wanachama.

Physical boundaries inabaki pale pale kutambua eneo la nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki!

Kwa mfano tulipoungana Zanzibar mipaka baina yetu ipo pale pale ila tulifungua mipaka, maana yake bidhaa au raia yeyote kutoka upande wowote anaingia kokote bila kikwazo! Hiyo ndio maana yake!

Mkuu tuelimishame bila kutiana hofu zisizokuwepo. Kuna manufaa makubwa katika kufungua mipaka yetu kuliko kujifungia wenyewe!
 
Anatumia makalio
Mkuu sio vyema kushambulia kwa matusi makubwa ya namna hii! Tujadili usahihi wa hoja yake, na kama hatukubalianj nayo, tupinge hoja yake kwa hoja, facts na staha.

Mkuu mara nyingi matumizi ya matusi ni ishara ya kuishiwa hoja au uelewa finyu! Unavyoonekana wewe sio mtu wa hivyo, wewe upo zaidi ya level hiyo! Usijishushe kihivyo Mkuu!
 
Japo wanakujibu nyoko ila una kitu umeongea.

Ila kwa nchi yetu watakuwa wa kwanza kwanza kusaini makubaliano.

Mkenya anautaka mlima Kilimanjaro, hadi bandari hiyo iliyouzwa itatekwa, , ziwa Tanganyika, ziwa Nyasa, ziwa Victoria yote yatachukuliwa, we will remain naked.
Mkuu Kenya tayari ni shetani ambaye hatuwezi kumuepuka! Ndiye mwekezaji namba mbili kwenye uchumi wetu!

Uwekezaji huo ndio njia laini ya kumiliki hivyo vitu vyote ulivyootaja. Swali la kujiulliza, Je sisi tumewekeza kiasi gani kwenye uchumi wao??

Na hapa ndipo umuhimu wa kufungua mipaka unapo kuja ili watanzania nao wapate fursa ya kumiliki sehemu ya uchumi wao!
 
Umaskini utaondolewa na wewe mwenyewe kwa mikono yako na juhudi zako mwenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa na kujituma kwa hali ya juu sana na siyo kungoja mtu aje ukuondolee umaskini hapo nyumbani kwako.
👍👌👏🙏🆒
 
Mkuu Kenya tayari ni shetani ambaye hatuwezi kumuepuka! Ndiye mwekezaji namba mbili kwenye uchumi wetu!

Uwekezaji huo ndio njia laini ya kumiliki hivyo vitu vyote ulivyootaja. Swali la kujiulliza, Je sisi tumewekeza kiasi gani kwenye uchumi wao??

Na hapa ndipo umuhimu wa kufungua mipaka unapo kuja ili watanzania nao wapate fursa ya kumiliki sehemu ya uchumi wao!
Hatuna ujanja wa kuwekeza chochote Kenya.

Hata wale wamama wajasiriamali hawana nafasi huko
 
Tanzania tunaplay victim yaani sisi kwenye jumuia ndo wanyonge badala ya kuwa wababe? Sisi ndo tunaonewa badala ya kuonea? Sisi ndo wakutawaliwa na majirani sio? Dharau hizi ndo zinatufanya tusitambe EAC. Hiyo ardhi wamekuja waarabu na wazungu na wamekufa wameiacha hata wakija hao majirani hawataibeba waipeleke kenya bali itabaki kuwa tz na wao watakufa wataiacha so tukomae akili, tutambe tuwe kama wanigeria popote walipo wana heshimika na sio watu lialia
👍👌👏🙏 💐 🎁 🆒
 
Yaani niliposoma mstari wa pili tu kuwa UTAJIRI TULIONAO nikakimbia kwenye comment niandike tu
Ni kwanini tunajisifia utajiri kila leo wakati asilimia kubwa hawana hata milo 2 kwa siku?
Tuna utajiri upi?
Kwa kufungua mipaka hapana maana sisi sio kama ulaya
Hao ndio wana utajiri na wanajielewa

Nilikuwa napeleka mizigo Paris kutoka London kwa truck ila unavuka channel kwa meli halafu unakatisha border kwa kupitia Belgium kidogo
Huulizwi passport wala nini na huonani na mtu cha ajabu hata border hakuna unaona nguzo ya taa ya Belgium na ya Tatu ni France
Unakunywa chai Belgium hapo hapo Tambo 20 uko nyumba ya mfaransa
Sasa sisi bila borders ni mtihani boss
 
Kwa hiyo kama iliwekwa na wakoloni ndio unataka nchi yetu iwe kama choo cha sokoo kwa kila mtu kuingia tu bila utaratibu? Ndio mawazo yako hayo?
Nakumbuka kuna watu walipendekeza kuwa Burundi isiingizwe Afrika y as Mashariki.
Walitoa hoja zao kuntu.
Kilichofuata kinafahamika.

Hoja hapa iwe manufaa ya kufanya na kutofanya hivyo.
 
Sisi siyo wanyonge lakini kumbuka ya kuwa unapofanya mashambulizi ni lazima pia ujilinde nakuwa na ulinzi wa kutosha kwako.sasa wewe unataka mipaka yetu iwe wazi tu kwa kila mdudu kuingia atakavyo? Ndio ubabe huo? Sasa unakuwa unashambulia nini wakati kwako wanazidi kupenya tu?
Mkuu Mwashambwa usiwe na hofu isiyo kuwepo na kuwatia wengine hofu yako ya kufikirika. Kwa taarifa yako kuna watanzania wengi wanaendesha shughuli zao nchini Musumbiji, Malawi, Zambia, Congo na Uganda na Kenya bila bugudha.

Je unayo taarifa kuwa kuna watanzania wachaga, wakurya, wamaasai wengi nchini Kenya wanaoishi na kuendesha shughuli zao bila bugudha!

Kenya imelikubali kabila la wamakonde na kulitambua kama moja ya makabila yake!

Mkuu hakuna anayeweza kuhamisha ardhi kwenda sehemu nyingine! Think outside the box, could be and it seems your exposure is some limited to only Tanzania!
 
Tanzania tunaplay victim yaani sisi kwenye jumuia ndo wanyonge badala ya kuwa wababe? Sisi ndo tunaonewa badala ya kuonea? Sisi ndo wakutawaliwa na majirani sio? Dharau hizi ndo zinatufanya tusitambe EAC. Hiyo ardhi wamekuja waarabu na wazungu na wamekufa wameiacha hata wakija hao majirani hawataibeba waipeleke kenya bali itabaki kuwa tz na wao watakufa wataiacha so tukomae akili, tutambe tuwe kama wanigeria popote walipo wana heshimika na sio watu lialia
Tuweke mikakati ya kuwajaza maarifa vijana wetu kufaidi mali na raslimali hizi badala ya kuwa na tabia ya mbwa kulalia nyasi nzuri.
Israel, nchi sawa na mkoa wa Mtwara inatamba duniani si kwa raslimali bali kwa akili zao za kukabiliana na changamoto.
 
Mkuu ni kweli walizuia mahindi na mambo mengine hapo nyuma na siwatetei ila naweka preamble facts hapa.

Mkuu tuuwe wa kweli kabla hatujaanza kuwanyooshea kidole, tujitizame sisi kwanza na tuseme ukweli; Tuliwafanyia mangapi kabla ya wao kufikia kuchukua hatua hiyo.

Hivi unajua hata hizi nchi jirani mathalan Malawi, Zambia Congo, Burundi, Rwanda na Uganda tunazifanyia vituko sana ila haziwezi kureteriate equally kama Kenya kwa sababu hawana Bandari, ni dependant kwa Tanzania, kwa hiyo inawalazimu kuwa wa pole.

Kenya ana guts na muscles kwa sababu sio tegemezi kwa Tanzania.
Kwa taarifa yako Kenya ndio power house wa Jumuiya ya Afrika mashariki, ni second world country with the most skilled labour na ndio nchi ya pili kwa uwekezaji nchini wetu!

Reactions zake zina repercussions kubwa kwetu hata kama tutashupaza shingo! Na kumalizia kufungua mpaka ni utaratibu rasmi wa kuwezesha urahisi wa watu kufanya shughuli za uzalishaji na biashara bila vikwazo!

Mkuu ondoa mashaka, mbona Zanzibar tuliungana nao tukafungua mipaka na hakuna madharra yoyote yaliyo wahi kutufika?

Tuwe objective na optimistic kwenye mambo yenye manufaa mapana kwetu!
Muungano wetu na Zanzibar ni tofauti ni kile kinachoweza kutokea ikiwa tutaruhusu uholela wa mambo kule mipakani.kenya imekuwa ni nchi ya chokochoko sana kule mipakani ,hasa inapoona kuwa tunakwenda kwa kasi katika kupekeka bidhaa kwao zinazofanya vyema katika soko lao la Ndani. Hatupaswi kuwachekea hovyo hovyo wakenya.wale ni mabepali waliokubuhi.ndio maana wachache wamekomba ardhi yote kwao na kuwaacha mamilioni ya wakenya wakiwa hawana ardhi ya kufanyia shughuli za kiuchumi.kenya hajawahi kuwa mwema kwetu watanzania.
 
Mkuu Mwashambwa usiwe na hofu isiyo kuwepo na kuwatia wengine hofu yako ya kufikirika. Kwa taarifa yako kuna watanzania wengi wanaendesha shughuli zao nchini Musumbiji, Malawi, Zambia, Congo na Uganda na Kenya bila bugudha.

Je unayo taarifa kuwa kuna watanzania wachaga, wakurya, wamaasai wengi nchini Kenya wanaoishi na kuendesha shughuli zao bila bugudha!

Kenya imelikubali kabila la wamakonde na kulitambua kama moja ya makabila yake!

Mkuu hakuna anayeweza kuhamisha ardhi kwenda sehemu nyingine! Think outside the box, could be and it seems your exposure is some limited to only Tanzania!
Kuwepo kwa watanzania nchi fulani siyo kigezo au hoja au sababu ya sisi kuweka uholela katika mipaka yetu na sheria zetu.kwani sisi hapa Tanzania hakuna wageni kutoka mataifa ya kigeni? Tunachotaka ni lazima sheria zetu zilifuatwe na kuzingatiwa na nilazima sheria hizo zilinde maslahi yetu ya Taifa.
 
Mkuu Kenya tayari ni shetani ambaye hatuwezi kumuepuka! Ndiye mwekezaji namba mbili kwenye uchumi wetu!

Uwekezaji huo ndio njia laini ya kumiliki hivyo vitu vyote ulivyootaja. Swali la kujiulliza, Je sisi tumewekeza kiasi gani kwenye uchumi wao??

Na hapa ndipo umuhimu wa kufungua mipaka unapo kuja ili watanzania nao wapate fursa ya kumiliki sehemu ya uchumi wao!
Kama unasema hatujawekeza kenya kwa hiyo yukifungua mipaka ndio tutaweza kuwekeza au tutakuwa Jalala tu la kila kitu?
 
Muungano wetu na Zanzibar ni tofauti ni kile kinachoweza kutokea ikiwa tutaruhusu uholela wa mambo kule mipakani.kenya imekuwa ni nchi ya chokochoko sana kule mipakani ,hasa inapoona kuwa tunakwenda kwa kasi katika kupekeka bidhaa kwao zinazofanya vyema katika soko lao la Ndani. Hatupaswi kuwachekea hovyo hovyo wakenya.wale ni mabepali waliokubuhi.ndio maana wachache wamekomba ardhi yote kwao na kuwaacha mamilioni ya wakenya wakiwa hawana ardhi ya kufanyia shughuli za kiuchumi.kenya hajawahi kuwa mwema kwetu watanzania.
Mkuu Mwashambwa napenda nikukumbushe kuwa ujamaa upo kwenye maandishi tu!

Mkuu uhalisia, Tanzania tupo kwenye ubepari sawa na Kenya! Wewe hapo unaishi kibepari sio kijamaa japo umegandana na mawazo ya kijamaa!

Kuhusu umiliki wa ardhi, Je kwa sasa hivi Tanzania, kuna tajiri au kiongozi wa serikali mkubwa asiyemiliki ardhi kubwa? Hofu yako ni kufikirika zaidi!
 
Back
Top Bottom