Tanzania tunayo malighafi ya kutosha kuendesha viwanda vyetu?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Wakati tunajipanga kuelekea uchumi Wa viwanda je hali yetu ikoje kwenye uwekezaji Wa kupata malighali ya kutosha viwanda tutakavyojenga?

Nijuavyo mimi malighafi iliyoko sasa ni ile ya mtindo wa kuokoteza kutoka kwa raia binafsi wasiokuwa na ujuzi wala mitaji ya kuzalishia.

Kipi kianze kwanza kati ya uwekezaji katika uzalishaji Wa malighafi na uwekezaji kwenye viwanda?
 
Hatuna, na ndio sababu viwanda vinakufa automatically.

Leo TBL wanaagiza malighagi ya bia (malt) kutoka nje, kiwanda chao cha moshi washakifunga.

Gharama za uzalishaji hasa shamban kwa Tz ni kubwa sana, kutokana na inputs bei juu sana.
 
Naona hili jambo liko wazi kwa namna hii;huwezi kujenga viwanda na usijue nini unaenda kuzalisha au upatikanaji wake wa malighafi ni 0 au mdogo saana,.pengine unajua kiwanda kitakuwa cha kuzalisha nguo kwa mfano, je, upatikani wa malighafi za kutengeneza hizo nguo upo?mashamba yapo lakini hayazalishi au ya kizalisha hayakidhi mahitaji sasa bora kipi "kuwekeza kwenye kuzalisha malighafi" kwanza au "kuwekeza kwenye uzalishaji viwanda"?

Hata historia ya " industrial revolution " ukiisoma vzr utajua kilianza kipi kikafuata kipi.
 
Chuma tunayo ya kutosha. Na chuma ndiyo mama wa mapinduzi ya viwanda. Ngozi tunazo za kutosha kuendesha viwanda vya viatu na bidhaa za ngozi. Kahawa ipo nyngi tu. Madini ya phosphate kwaajili ya viwanda vya mbolea yapo. Samaki kwaajili ya viwanda vya samaki wapo wa kumwaga. Malighafi zipo za kutosha.
 
Lazima kuwe na plantations za watu wanaozalisha kibiashara sio peasants wanaolima kwa hiari bila utaalam wala mitaji, pembejeo na ruzuku. Mh. Kaijage sio kwamba halijui hili ila kuna sheeda
 
Chuma tunayo ya kutosha. Na chuma ndiyo mama wa mapinduzi ya viwanda. Ngozi tunazo za kutosha kuendesha viwanda vya viatu na bidhaa za ngozi. Kahawa ipo nyngi tu. Madini ya phosphate kwaajili ya viwanda vya mbolea yapo. Samaki kwaajili ya viwanda vya samaki wapo wa kumwaga. Malighafi zipo za kutosha.
Uko serious? Ngozi zetu ni rejects
 
Back
Top Bottom