Tanzania tunaendelea? Angalia takwimu hizi - Ufukara, Njaa, Udumavu, Vifo vya Uzazi na Ajira...

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Tunaendelea?

UFUKARA
64% ya Watanzania hawakuweza kumudu maisha mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania wasiomudu gharama za msingi za maisha ni 76%

NJAA
22% ya Watanzania walikuwa wanashinda au kulala na njaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania 27% wanashinda au kulala na Njaa

UDUMAVU
34.4% ya Watoto wa Tanzania walikuwa wamedumaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watoto 34.7% nchini wamedumaa

VIFO VYA UZAZI
Wanawake 438 kati ya wanawake 100,000 waliojifungua walikufa mwaka 2014. Mwaka 2018 Wanawake 556 walipoteza maisha kati ya wanawake 100,000 waliojifungua

AJIRA
43% ya Watanzania walikuwa na imani kuwa Serikali itatengeneza ajira mwaka 2014. Mwaka 2018 ni 31% tu ya Watanzania wana imani na Serikali kutengeneza ajira.

Tunaendelea?
Kama Watanzania zaidi hawawezi kumudu gharama za maisha kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania zaidi wanalala njaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watoto wengi zaidi wanadumaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Wanawake wengi zaidi wanakufa kwa kubeba mimba kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania wengi zaidi wamepoteza imani kupata ajira kuliko miaka 2 iliyopita; Tunasemaje tunaendelea au kuna tafsiri mpya ya Maendeleo? Kwamba Maendeleo ni kulala na njaa zaidi, kudumaa zaidi, kina mama kufa zaidi?

Mtanzania! Usimamizi mbovu wa uchumi ndio unapelekea watu wengi zaidi wanalala na njaa, Watoto wetu wengi zaidi wanadumaa na wanawake wengi zaidi wanapoteza maisha kwa kuzaa. Usimamizi mbovu wa Uchumi chini Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ndio unapelekea ajira zaidi kutozalishwa na kuwafanya Watanzania wengi zaidi kushindwa kumudu gharama za Msingi maisha.

Tunaweza kuzuia hali hii na kurudi kwenye kujenga Uchumi shirikishi na unaozalisha ajira nyingi. Tunaweza kurudi kwenye reli ya Maendeleo na kuepuka udumavu zaidi, njaa zaidi na vifo zaidi vya kinamama.

Zitto Kabwe
 
Tunaendelea?

UFUKARA
64% ya Watanzania hawakuweza kumudu maisha mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania wasiomudu gharama za msingi za maisha ni 76%

NJAA
22% ya Watanzania walikuwa wanashinda au kulala na njaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania 27% wanashinda au kulala na Njaa

UDUMAVU
34.4% ya Watoto wa Tanzania walikuwa wamedumaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watoto 34.7% nchini wamedumaa

VIFO VYA UZAZI
Wanawake 438 kati ya wanawake 100,000 waliojifungua walikufa mwaka 2014. Mwaka 2018 Wanawake 556 walipoteza maisha kati ya wanawake 100,000 waliojifungua

AJIRA
43% ya Watanzania walikuwa na imani kuwa Serikali itatengeneza ajira mwaka 2014. Mwaka 2018 ni 31% tu ya Watanzania wana imani na Serikali kutengeneza ajira.

Tunaendelea? Kama Watanzania zaidi hawawezi kumudu gharama za maisha kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania zaidi wanalala njaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watoto wengi zaidi wanadumaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Wanawake wengi zaidi wanakufa kwa kubeba mimba kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania wengi zaidi wamepoteza imani kupata ajira kuliko miaka 2 iliyopita; Tunasemaje tunaendelea au kuna tafsiri mpya ya Maendeleo? Kwamba Maendeleo ni kulala na njaa zaidi, kudumaa zaidi, kina mama kufa zaidi?

Mtanzania! Usimamizi mbovu wa uchumi ndio unapelekea watu wengi zaidi wanalala na njaa, Watoto wetu wengi zaidi wanadumaa na wanawake wengi zaidi wanapoteza maisha kwa kuzaa. Usimamizi mbovu wa Uchumi chini Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ndio unapelekea ajira zaidi kutozalishwa na kuwafanya Watanzania wengi zaidi kushindwa kumudu gharama za Msingi maisha.

Tunaweza kuzuia hali hii na kurudi kwenye kujenga Uchumi shirikishi na unaozalisha ajira nyingi. Tunaweza kurudi kwenye reli ya Maendeleo na kuepuka udumavu zaidi, njaa zaidi na vifo zaidi vya kinamama.

Zitto Kabwe
Tangu ulipotoa takwimu zako na kusema 2017 Tanzania imekumbwa na baa lanjaa tena misuli ya shingo umekaza, Alafu ulicho kiongea tukagundua ni uongo sina imani tena na wewe . Kwa sasa nahisi Dishi litakua limecheza.
 
Hoja yako inanikumbusha wakati uliposhupaa kuwa kuna baa la njaa halafu baadaye ukayeyuka kama barafu mbele ya joto bila kuleta mrejesho!

Leo umekuja na suala la ufukara na ninajua baada ya muda utayeyuka na kuibuka na suala lingine!

Zitto siku hizi ndani ya ACT-Wazalendo amekuwa Kiongozi Mkuu, Mbunge, katibu Mwenezi, Mweka hazina, Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya nchi za nje na ...

He's John Cheyo in making!

LINK>>>Je, ACT-Wazalendo ya Zitto Kabwe kuwa kama UDP ya John Cheyo
 
Back
Top Bottom