Tanzania tunaendelea? Angalia takwimu hizi - Ufukara, Njaa, Udumavu, Vifo vya Uzazi na Ajira...

Nashindwa kuelewa hiyo taarifa ya 2018 ni makisio au ni sahihi? Na kama ni sahihi huu mwaka 2018 ndo kwanza tuko ¼ ya mwaka na figure ni kubwa hivyo. Huoni km kuba kutupa taarifa zenye mkanganyiko hapo.
 
I guess mkuu Zitto uangalie utalisaidieje jimbo lako,

wengine watafuata wakiona umekua successful,

Tembelea na kukutana na watu wako,

utajua wapi panahitaji kupelekewa nguvu,

kama ni training,fursa za biashara kama mitaji etc

ukifanikiwa kumobilize watu,then jimbo litabaki kwa ACT,

I think new projects sometimes is interesting,

what do u think?lol
 
Tunaendelea?

UFUKARA
64% ya Watanzania hawakuweza kumudu maisha mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania wasiomudu gharama za msingi za maisha ni 76%

NJAA
22% ya Watanzania walikuwa wanashinda au kulala na njaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania 27% wanashinda au kulala na Njaa

UDUMAVU
34.4% ya Watoto wa Tanzania walikuwa wamedumaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watoto 34.7% nchini wamedumaa

VIFO VYA UZAZI
Wanawake 438 kati ya wanawake 100,000 waliojifungua walikufa mwaka 2014. Mwaka 2018 Wanawake 556 walipoteza maisha kati ya wanawake 100,000 waliojifungua

AJIRA
43% ya Watanzania walikuwa na imani kuwa Serikali itatengeneza ajira mwaka 2014. Mwaka 2018 ni 31% tu ya Watanzania wana imani na Serikali kutengeneza ajira.

Tunaendelea?
Kama Watanzania zaidi hawawezi kumudu gharama za maisha kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania zaidi wanalala njaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watoto wengi zaidi wanadumaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Wanawake wengi zaidi wanakufa kwa kubeba mimba kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania wengi zaidi wamepoteza imani kupata ajira kuliko miaka 2 iliyopita; Tunasemaje tunaendelea au kuna tafsiri mpya ya Maendeleo? Kwamba Maendeleo ni kulala na njaa zaidi, kudumaa zaidi, kina mama kufa zaidi?

Mtanzania! Usimamizi mbovu wa uchumi ndio unapelekea watu wengi zaidi wanalala na njaa, Watoto wetu wengi zaidi wanadumaa na wanawake wengi zaidi wanapoteza maisha kwa kuzaa. Usimamizi mbovu wa Uchumi chini Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ndio unapelekea ajira zaidi kutozalishwa na kuwafanya Watanzania wengi zaidi kushindwa kumudu gharama za Msingi maisha.

Tunaweza kuzuia hali hii na kurudi kwenye kujenga Uchumi shirikishi na unaozalisha ajira nyingi. Tunaweza kurudi kwenye reli ya Maendeleo na kuepuka udumavu zaidi, njaa zaidi na vifo zaidi vya kinamama.

Zitto Kabwe
Zito hilo ni taifa la wajinga
 
Back
Top Bottom