Tanzania tunaendelea? Angalia takwimu hizi - Ufukara, Njaa, Udumavu, Vifo vya Uzazi na Ajira...

Hoja yako inanikumbusha wakati uliposhupaa kuwa kuna baa la njaa halafu baadaye ukayeyuka kama barafu mbele ya joto bila kuleta mrejesho!

Leo umekuja na suala la ufukara na ninajua baada ya muda utateyuka na kuibuka na suala lingine!

Zitto siku hizi ndani ya ACT-Wazalendo amekuwa Kiongozi Mkuu, Mbunge, katibu Mwenezi, Mweka hazina, Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya nchi za nje na ...

He's John Cheyo in making!

LINK>>>Je, ACT-Wazalendo ya Zitto Kabwe kuwa kama UDP ya John Cheyo


Mkuu, kwani kuna ubaya wowote Zitto kuwa na uwezo wa kufanya kazi zote hizo yeye mwenyewe? To me, that's a strength, not a weakness. Jibuni hoja, kwanini tunaonekana kurudi nyuma kimaendeleo ktk maeneo ambayo ameyataja Zitto?
 
Mkuu Zitto umenikumbusha uliposema tuna baa la njaa.......hahahahaha
 
Japo ni kweli hatuendelei ila Jiwe halitaki kusikia hizi habari.

Sijui kwa kuwa pale Magogoni ni full mapcho pocho hamnaga kulala njaa??
Jiwe yeye anasema wazungu wanatuonea wivu. Tunajenga reli kwa hela zetu wkt deni la Taifa linapanda kila leo.. Huku wapambe wake wanasema deni hilo ni stahimilivu.. Yani ni wimbo flani hivi ambao kichaa ametulia sana kuutunga.
 
Yeye katoa takwimu,wewe toa ushauri au sio mwanafikra pevu wewe?
Upinzani ni kuuza sera mbadala; hii ndio nafasi yake ya kutuambia yeye angefanya nini.

Anachofanya hapa ni kulalamika tu.

Au kulalamika ndio sera zenu??
 
Wepesi wa kulaumu kana kwamba kazi ya maendeleo ni ya serikali tu,sivyo,wapo watu matajiri kuliko hata serikali.
Kazi ya serikali ni kuweka mazingira sahihi ili wananchi wajikwamue wao wenyewe.
Lakini kama serikali ikaamua kujibebesha mzigo mkubwa kuliko uwezo wake hapo kutakuwa na walakini.
 
Upinzani ni kuuza sera mbadala; hii ndio nafasi yake ya kutuambia yeye angefanya nini.

Anachofanya hapa ni kulalamika tu.

Au kulalamika ndio sera zenu??
Mtu anatoa tafiti wewe unasema analalamika?
Tafiti hupingwa kwa tafiti na sio na mapovu mkuu. Shubaaaamit.
 
Tatizo ni kwamba aliyeshiba hamjui mwenye njaa,na mbaya zaidi watanzania wa leo wana ubinafsi sana na unafiki mkubwa, wanapenda kuona wengine wakiteseka ndio furaha yao
 
...zitto...utawala huu wala hausomi unayosema.....Na hata wakiyasoma hawayafanyii kazi...maana wao agenda yao ni kushughulika Na nyie....nashangaa sana awamu hii imejaa madaktari wa PhD tele kwenye cabinet lakini sioni hata mmoja wao anaongelea haya mambo..shame on them dogs...
 
Tunaendelea?
Tunaendelea?
Mtanzania! Usimamizi mbovu wa uchumi ndio unapelekea watu wengi zaidi wanalala na njaa, Watoto wetu wengi zaidi wanadumaa na wanawake wengi zaidi wanapoteza maisha kwa kuzaa. Usimamizi mbovu wa Uchumi chini Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ndio unapelekea ajira zaidi kutozalishwa na kuwafanya Watanzania wengi zaidi kushindwa kumudu gharama za Msingi maisha.

Tunaweza kuzuia hali hii na kurudi kwenye kujenga Uchumi shirikishi na unaozalisha ajira nyingi. Tunaweza kurudi kwenye reli ya Maendeleo na kuepuka udumavu zaidi, njaa zaidi na vifo zaidi vya kinamama.
Zitto Kabwe
Zitto, kuna msemo usemao, usipoziba ufa, utajenga ukuta, ila sio kifa lazima uzibwe, ufa ukitokea kwenue ukuta tuu ndio unaziba, lakini ufa ukitokea kwenye structures au kwenye msingi, huwezi kuziba, itakubidi ubomoe tuu kisha ujenge upya.

Magufuli ameikuta nchi kwenye ufa Mkubwa kwenye structures, hivyo anachofanya sasa ni kubomoa kwanza, halafu ndio tutatenga.

Tanzania ni nchi inayotegeme kilimo, na Mifugo, hivyo Tanzania ya viwanda vya ukweli ni vitakavyoleta maendeleo ya kweli ya taifa, ni agro processing industries, ili kuwa na viwanda vya chakula na mazao, sekta yenye priority No. 1 kuendelezwa ni sekta ya kilimo, ili izalishe malighafi ya viwanda!, Tajiri Mkubwa number 1 wa viwanda vya chakula Tanzania ni SS Bakhresa, ngano yake yote 100% ni imported!, yale mashamba ya ngano, West Kilimajaro na Aldadawi kule Karutu, Wasukuma wanalishia Mifugo!. Zile juices ni 80% imported pulp, wakati machungwa yanaozea mitini pale Lushoto!. Tumefungua kiwanda cha magari pale Kibaha, hadi nati inatoka kwao!. Reli ya SGR, bidhaa pekee ya Tanzania inayotumika ni chakula tuu cha mama mtilie!, huku chuma cha Liganga kikidoda!. Hii Tanzania ya viwanda, ni Tanzania ya viwanda gani?, Mchina?!. Where is the blue print ya Tanzania ya

Kuna haraka gani kujenga SGR kama meter gauge railways zilizopo tumeshindwa kuzitumia!, This is the biggest White elephant we have ever had, kama tungeimarisha tuu kwa hii reli iliyopo na kuitumia to the full capacity na hizo Fedha tukazipeleka kwenye sekta ya kilimo, ingekuwa na multiplied effects kubwa kiasi gani kulinganisha na SGR na Flyovers?.

Acha tuu tuendelee kubomoa, tukijenga upya, tutajenga uchumi imara kuliko huu, Tanzania ya uchumi wa kati, uchumi wa gesi na Tanzania ya viwanda.

Mungu ibariki Tanzania.
P
 
Mhe. ZITTO Mkoa wako wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa yenye Watu maskini zaidi (kipato duni, makazi mabovu, elimu zero, uharibifu mkubwa wa Mazingira NK NK) umefanya nin so far kama mbunge wao hadi sasa?. Anza kwanza kutoa bolt jichon mwako ndio utoe kibanz jichon kwa mwenzako. Mbaya zaid Ukabila umewatawala na kumeza chama chako cha ACT maana kimegeuka chama cha WAHA na WAHUTU.
 
Tunaendelea?

UFUKARA
64% ya Watanzania hawakuweza kumudu maisha mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania wasiomudu gharama za msingi za maisha ni 76%

NJAA
22% ya Watanzania walikuwa wanashinda au kulala na njaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watanzania 27% wanashinda au kulala na Njaa

UDUMAVU
34.4% ya Watoto wa Tanzania walikuwa wamedumaa mwaka 2014. Mwaka 2018 Watoto 34.7% nchini wamedumaa

VIFO VYA UZAZI
Wanawake 438 kati ya wanawake 100,000 waliojifungua walikufa mwaka 2014. Mwaka 2018 Wanawake 556 walipoteza maisha kati ya wanawake 100,000 waliojifungua

AJIRA
43% ya Watanzania walikuwa na imani kuwa Serikali itatengeneza ajira mwaka 2014. Mwaka 2018 ni 31% tu ya Watanzania wana imani na Serikali kutengeneza ajira.

Tunaendelea?
Kama Watanzania zaidi hawawezi kumudu gharama za maisha kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania zaidi wanalala njaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watoto wengi zaidi wanadumaa kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Wanawake wengi zaidi wanakufa kwa kubeba mimba kuliko miaka 2 iliyopita. Kama Watanzania wengi zaidi wamepoteza imani kupata ajira kuliko miaka 2 iliyopita; Tunasemaje tunaendelea au kuna tafsiri mpya ya Maendeleo? Kwamba Maendeleo ni kulala na njaa zaidi, kudumaa zaidi, kina mama kufa zaidi?

Mtanzania! Usimamizi mbovu wa uchumi ndio unapelekea watu wengi zaidi wanalala na njaa, Watoto wetu wengi zaidi wanadumaa na wanawake wengi zaidi wanapoteza maisha kwa kuzaa. Usimamizi mbovu wa Uchumi chini Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ndio unapelekea ajira zaidi kutozalishwa na kuwafanya Watanzania wengi zaidi kushindwa kumudu gharama za Msingi maisha.

Tunaweza kuzuia hali hii na kurudi kwenye kujenga Uchumi shirikishi na unaozalisha ajira nyingi. Tunaweza kurudi kwenye reli ya Maendeleo na kuepuka udumavu zaidi, njaa zaidi na vifo zaidi vya kinamama.

Zitto Kabwe
Lakini Mbuzi wanakunywa soda pia mwaka 2017
 
Back
Top Bottom