Serikali na Mkakati wa Kupunguza Vifo Vya Watoto Njiti Nchini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Ifakara Health Institute wameweka mkakati wa kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (njiti) ,kwa kuwawezesha watoa huduma kufanya kazi kwenye mazingira wezeshi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa pili wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi wa Mama na Mtoto Mkurugenzi Mkuu wa Ifakara Health Institute Dk Honorati Masanja amesema kitaifa wamepiga hatua kwenye kupunguza vifo vya mama ila watoto bado ni changamoto.

Amesema kazi ya taasisi hiyo ni kufanya tafiti ambazo zitaleta afua mbalimbali za kuboresha Afya ya mama na mtoto.

Aidha amesema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni upungufu wa wahudumu wa afya hususani kwenye eneo la mama na mtoto hivyo jitihada za makusudi zinahitajika katika kuongeza wahudumu wa afya.

Kwa upande wake Daktari wa watoto kutoka chuo Cha MUHAS Dkt Nahya Salim amesema Tanzania inampango wa kushusha vifo vya watoto wachanga angalau mpaka 15 kwa vizazi hai 1000 ifikapo 2025.

Amesema bado wapo nyuma hivyo kasi kubwa inahitajika mara mbili zaidi au tatu ili kuweza kushusha kasi ya vifo vya watoto wachanga kwani ripoti iliyotolewa na wizara ya Afya vifo vya watoto bado hairidhishi ambapo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita wamepunguza wa asilimia moja tu.

“ Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Oktoba 28 mwaka huu na wizara ya Afya Asilimia 1 bado ndogo sana ina maana vifo 24 kutoka vizazi hai 1000 mpaka kwenda 15 hadi kufikia 2025 inabidi kasi zaidi iongezeke,"mesema Dk Nahya.

Amesema Tanzania imetekeleza mpango huu wa kupunguza vifo vya watoto njiti kwa hospitali tano za Dar es Salaam ambazo ni hospital ya Mwananyamala,Temeke Amana na hospitali za mkoa ni Muhimbili pamoja na Mloganzila.
 
Zerikali kigeugeu.
Wana punvuza vifo vya watoto njiti lakini wanasema NHIF TOTO card ni hasara kwa serikali!! Bii ni amili au matope? Si bors wawaachd wafe ili wasije kuwa mzigo kwa serikali?
Taifa la ajabu sana hili.
 
Zerikali kigeugeu.
Wana punvuza vifo vya watoto njiti lakini wanasema NHIF TOTO card ni hasara kwa serikali!! Bii ni amili au matope? Si bors wawaachd wafe ili wasije kuwa mzigo kwa serikali?
Taifa la ajabu sana hili.
Tulia andika vizuri tukuelewe na sisi
 
Back
Top Bottom