Nikiangalia safu ya juu ya viongozi wa tume ya uchaguzi sioni dalili za uchaguzi huru na haki naona wizi utakaowakwaza wenye njaa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Najaribu kutafakari mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, kisiasa na tume ya uchaguzi dhidi ya uchaguzi huru na haki, Najaribu kuoanisha na nguvu kubwa ya umma iliyo nyuma ya CHADEMA, Nazingatia pia usaliti mkubwa uliofichwa kwenye miyoyo ya wana ccm, Nasema hakuna namna tutakuwa na uchaguzi huru kwa safu ile pale kileleni mwa tume.

Wote waliokaa pale juu ni wana ccm na kibaya zaidi wote wanaishi kwa mishahara hakuna hata mmoja aliyekamilisha taratibu za kujitegemea. Kwa mantiki hiyo ukiwapa dalili za kuwanyima mshahara umesumbua mfumo wao wa maisha. watu hawa hawawezi kuwaza kuhusu uchaguzi huru bali wataihshi kwa kumtumikia aliyewateua.

Kama watu wa sampuli hii ndio wataendelea kukaa pale juu kwa ujumla tutegemee machafuko maeneo mengi nchini hasa yanayotokana na wizi wakura. Bila wizi hakutakuwa na ushindi. kinyume chake tuombe hali ya uchumi ibadilike na gharama za maisha zipungue. hali hii ya uchumi ikiendelea kuwa hivi kuelekea uchaguzi vCCM watajua wazi kwamba mwenye njaa hana cha kupoteza.

Tumeona maandamano yalivyo na umati wa watu, hawa watu wangekuwa na shibe wasingeandamana. Na Ikumbukwe miaka yote chadema wanafanya siasa za kisomi. Wameona maisha magumu wameamua watu waaandamane na kwa kuwa njaa ni ya wote hata Dr. Slaa naye ameungana na watesi wake na sasa wanatumia jukwaa moja.


Ndugu zangu ccm natambua hakuna viongozi huru wa tume ya uchaguzi ila pia natambua ubaya wa kumdhulumu mtu mwenye njaa na asiye na ajira, Ni rahisi sana watu wa aina hii kufanya vurugu wanapoaminishwa wameibiwa. Mkitaka msilete machafuko punguzeni gharama za matumizi ya serikali mpeleke neema ya chakula na ajira kwa vijana kupunguza hasir zinazopandwa ndani yao na chadema.

Msitegemee tume maana kutegemea wizi wa kura kwa hali hii nikutengeneza machafuko. Kuna nchi imewahi kupata maandamano na kupelekea vifo kwa sababu ya mkate. wapeni wananchi mikate washibe acheni kutegemea mifumo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom