Tanzania tuna Rais asiyejua majukumu yake na wajibu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tuna Rais asiyejua majukumu yake na wajibu wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hakikwanza, Dec 26, 2011.

 1. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kwangu mimi binafsi kwa jinsi nchi yangu inavyokwenda na kuendeshwa vibaya,Jk na mwona ni Rais asiyejua majukumu yake na nini anakifanya hapo magogoni na hii yote ni makusudi kubwa, Rais ni baba mwenye nyumba ktk nchi, Hivyo anapaswa kuilinda nyumba yake dhidi ya uvamizi wa ndani au nje ya nyumba yake lakini Jk kama baba wa nchi hii kiukweli majukumu yanamshinda kwa kiwango kikubwa.Ameshindwa kutoa maamuzi ya maswala magumu yanayoikabili nchi kama Richmond,EPA,MEREMETA,Wizi wa wanyama wetu,skendo za kina Luhanjo na Jailo,Posho zisizo stahili, kupanda kwa bei za vitu, wizi wa madini yetu na uzembe mwingine mwingi anaoufumbia macho.Je tutafika?
   
 2. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Tatizo si kutojua majukumu yake bali ni kujikuta yuko katika kila mduara wa kashfa za ufisadi. Unadhani ataweza kata mikono yake mwenyewe? Kashfa ya EPA yumo, Meremeta yumo yeye na familia yake (Riz1) uuzwaji nyumba kule Italy yumo, ya Richmond yumo, Dowans yumo, ya Rada yumo, ya kuuza wanyama nje ili miaka ijayo watalii wasiwe wanakuja huku bali wawe wanakwenda uarabuni kuwaona twiga, chui na Tembo yumo..... ni kashfa ipi impite? Hapa tuandike maumivu hadi 2015! Na mengi yatajulikana baada ya kuachia ngazi.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mnamlaumu bure tu, wa kujilaumu ni sisi wenyewe, maana ndio tuliomweka madarakani
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ni ukweli ambao unasikitisha na kuumiza sana lakini ndio ukweli wenyewe.
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ili Rais wenu awafikishe kokote lazima ajue anakotaka kuwapeleka; lakini bahati mbaya sana Rais wenu hajui alikotoka, alipo sasa wala wapi anakwenda!! Kama hali ndiyo hivyo ilivyo, unapouliza kama mtafika ni kuelekea wapi?
   
 6. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  Atatoaje uamuzi wakati na yeye ni mshiriki wa ufisadi.
   
 7. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  U-RAIS ni taasisi.
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  je weye kama mwananchi wayajua majukumu yako..?! mpaka sasa umechukua hatua gani..?!
   
 9. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,848
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Ha! Ha! Haa! ha ha. Huyo ni chaguo la Mungu mlituaminisha tangu mwaka 2005. Acheni kulialia. Nani analia wakati mlipiga kura wenyewe?
   
 10. P

  PARAGEcTOBORWA Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzani acheni kuyumbishwa na wajinga wenye tamaa ya madaraka,, Rais yupo pale kwa mujibu wa katiba na sheria, unata achukue maamuzi gani wakati kuna vyombo vya sheria? Mna lalamika kuwa Rais ana madaraka makubwa halafu mnataka yeye huyohuyo afanye abebe majukumu ya mahakama? Huwezi kufanya maamuzi magumu kwa kuvunja sheria, maamuzi magumu ni kuhakikisha unaisimamia sheria na kuilinda katiba. Mh, kikwete ni kiongozi makini sana nina imani hamtomuingiza mtegeno hata cku moja kwa hoja zenu za njia ya mkato, mpaka amefika hapo amepitia majukumu mbalimbali na alijiandaa tena muda mrefu kuwa kiongozi wa taifa hili, haya yanayotokea sasa ni changamoto kwa cc wananchi na cy kwa yeye kama kiongozi, embu wewe jaribu kueleza maamuzi magumu ambayo hata kama mtoto wako anatabia ya kudokoadokoa nyumbani? Utamchoma moto viganja ndo tujue umechukua maamuzi magumu? Hili ni taifa tena linalotambulika na na mataifa mengine , linafanya uhusiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara na mambo mengine kwa mujibu wa sheria za kimataifa, sasa mkikalia maamuzi magumu bila kufuata utaratibu tutakuwa tumevuka mipaka na kuingilia haki za wengine. nani atabaki hapa tukichukua maamuzi magumu kila mmoja ktk nafasi yake? Hata JF itakuwepo? Maana yanayojadiliwa humu mengine yanabaki humuhumu kwa cc members yakiwafikia wenzetu ambao wapo nje ya jf ni aibu kubwa , lakini ni ka sheria tuu kanakotulinda cc na kumzuia mtu mwingine kutuingilia,, Tumpe moyo Rais wetu , tushirikiane naye katika kukabiliana na changamoto zinatolikabili Taifa letu kuelekea ktk kupata KATIBA Mpya itakayotuongoza ktk miaka mingine hamsini, na Mwenyezi Mungu atujaaliye tupate kiongozi anayeweza kuisimamia na Kuilinda katiba Hy mpya kwa moyo wake wote na Nguvu zake zote.Mungu ibariki Tanzania naWATU WAKE.
   
 11. MARUMARU

  MARUMARU JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  sio wote walio mchagua, kura nyingi waliiba kwa kumtumia mwenyekiti wa tume na tume yenyewe iliyoundwa na mafisadi na wasio na uchungu na nchi yao zaidi tamaa zao na kutekeleza majukumu wanayoagizwa na mabwana zao.
   
 12. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...Mpita Njia no,huyu ni rais wa tume ya uchaguzi...
   
 13. MARUMARU

  MARUMARU JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kiongozi bora ni yule anayesema na kuyasimamia maneno yake kuhakikisha yanatimia! Aliahidi maisha bora tangu 2005 je Watz wameyapata? na kama wameyapata tabaka ngani? acha kutetea ujinga, huyu mzee hakustahili kuwa rais amelazimisha tuu.
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Labda hakupewa JOB DESCRIPTION!!
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sawa U-Rais ni taasisi [an institution] lakini taasisi ina kiongozi anaeonesha njia; taasisi bila kiongozi sio taasisi bali ni mkusanyiko wa watu na maofisi!! Any viable institution must have credible leadership.
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hilo linajulikana ndugu zangu kuwa jk nchi haiwezi. Ni idadi kubwa tu ya wanawake waliipigia kura sura ya jk wakisema wanamtaka rais anayewavutia (Nadhani kimahaba zaidi na si kiutendaji, japo utendaji una maana nyingi). Ukichanganya na wizi ndio tumefika hapa.

  Kawaida rais anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi huwa hana muda wa kupoteza kutibu majeraha ya uchaguzi pamoja na kutafuta wachawi. Hadi leo serikali ya sasa inatafuta wachawi-kwa nini kura zilikuwa chache. Bado wanafanya utafiti huo. Hivyo mambo muhimu ya kimaendeleo yanawekwa kando kwanza.

  Kadhalika mtu kama huyu huwa na chuki kwa wale waliomnyima ushindi alioutaka, hivyo kufanya ubaguzi katika kuzigawa rasilimali za taifa sehemu husika. Sasa wanajipanga katika kutafuta mtu/product itakayouzika ifikapo 2015. Katika mchakato huo ndani yake kuna makundi mahasimu ambayo hakuna linalotaka kushindwa. Katika purukushani hizi mwananchi atakumbukwa saa ngapi? Wakiamka kidogo na kusikia wananchi wanalia shida, wanafunga mikanda kwenda kutuombea misaada ambayo huishia wanakojua wao. Mwisho wa siku tunakuwa vinara wa kuomba.

  Hayo ndio matunda ya serikali zisizo na ridhaa ya umma
   
 17. P

  PARAGEcTOBORWA Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dira ni maisha bora kwa kila mtanzania, halafu katoa uhuru kwa kila mtu katika nafasi yake, sasa nyie uhuru huo mnautumia kwa kupiga kelele, kuongea sana na kulialia mnataka muwekewe mirija mpaka kwenye matumbo yenu? Fanyeni kazi na kama mtaendekeza na huo ujinga mnaopewa na wanasiasa nchi hii itakuwa na wavivu wa kufanya kazi na wavivu wa kufikiri wapo wenye akili wameshatambua hilo lakini nyie mlienda shule kwenda kufaulu na kujifunza kaeni vivyo hivyo na kuwadanganya wengine kuwa serikali itafanya kila ki2 mwisho wa cku mtabaki na tai zenu wengine wakisonga mbele. mtu hubarikiwa kwa kazi ya mikono yake sasa nyie pigeni kelele kwa vilivyotafutwa na wenzenu mnaniudhi sana watu wa namna hii.
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  si Jk peke yake abebe mzigo wote bali na wale waliomrithisha mizigo. kati ya mizigo anayotakiwa kubeba ni wa Richmond ambao waziri Mkuu wake lowassa na mawaziri kadhaa walijiuzulu, kashfa ya luhanjo na Jairo lakini kashfa za EPA, MEREMETA, vitalu vya wanyama, madini chanzo chake ni awamu zilizopita.


   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi bila serikali kutafuta ushahidi na kufungua kesi, mahakama inaweza kufanya chochote?
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama ingekuwa ni mahakamani sheria isingebana Jk peke yake na matatizo tunayopata sasa mahakama inaangalia chimbuko/kiini/chanzo na ndipo mlolongo mzima wa wahusika kuwajibika lakini jambo la ajabu hata matatizo yote yaliyosababishwa na awamu zilizopita tunayaona kuwa ni ya JK peke yake.
   
Loading...